VUA VAZI LA KIGENI, VAA WOKOVU.

Na Godfrey Miyonjo.

“Naitakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa wafalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni” SEFANIA 1:8.
BWANA YESU asifiwe sana,
Atukuzwe Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo,
Wapendwa katika imani, kila mmoja wetu sharti ajue kuwa vazi rasmi kwa watu rasmi walioalikwa na BWANA YESU kuingia katika makao ya Mungu ni WOKOVU.
Wokovu huu ulio katika Kristo Yesu ndiyo utambulisho wetu mbele za Mungu,
Katika dunia hii kumekuwa na mavazi rasmi katika shughuri maalumu, watu huyavaa mavazi hayo kama utambulisho wao.
Kwa mfano, Wauguzi wana mavazi yao rasmi, madaktari nao wana mavazi yao, majaji, sare za harusi, n.k.
Mtu aliye na imani isiyokiri WOKOVU/ASIYOKIRI KUOKOKA dunian, huyo mbele za Mungu anahesabika amevaa vazi la kigeni.
Wengi husema kuwa imani zetu ndizo zitakazotuokoa, wanasema hivi pasipo kujua kuwa kusema hivi ni kumpinga YESU kuwa ndiye KRISTO.
Niwaulize hao wasemao hivvyo kuwa wataokolewa na imani zao: “Imani gani hiyo ambayo yaweza kumwokoa mwanadamu ambayo inapingana na KRISTO?”
Huu ni ukweliusiopingika kuwa imani isiyokiri wokovu haiwezi kumwokoa mtu, Imani hiyo itampelekea mtu huyo kutupwa JEHANAM.
Kwa sababu imani hiyo ni kama vazi la kigeni mbele za Mungu, na imeandikwa;………..nitawaadhibu wakuu, na wana wa wafalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni………. SEFANIA 1:8.
..

Katika siku hiyo, siku ya kutisha siku ya ghadhabu ya Mungumtu, siku ya hukumu mwanadamu awaye yote asiyejali WOKOVU hakika hatapona.
Kwa maana imeandikwa “sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali WOKOVU mkuu namna hii?.........” EBRANIA 2:3.
Kama wewe umeokoka basi yakupasa utunze sana vazi lako, na kama wewe bado haujaokoka
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaa………………………..!
………..VUA VAZI LA KIGENI VAA WOKOVU…………

Comments