WAKATI GANI PEPO HUMWINGIA MTU?

Na mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Efatha ministry.

Pepo haliwezi kumwingia mtu kwa urahisi akiwa na fahamu zake yaani akiwa hajalala bali humwingia mtu akiwa amelala. Wakati wa usiku ufalme wa giza hufanya kazi sana kuliko wakati mwingine wowote.

Dhambi ndiyo mlango mkubwa unaoruhusu pepo kumwingia na kufanya uharibifu.Watu wanapofanya dhambi na kulala pasipo kutubu, ndipo mapepo huingia, maana shetani anaelewa Mungu amesema "Usilale na hasira yako haijaisha", yaani mtu asilale huku hukumu ya Mungu inamkalia. Tunasoma "Mwe na hofu wala msitende dhambi, tafakarini vitandani mwenu na kutulia" ZAB 4:4
Unapoenda kulala tafakari uliyotenda siku nzima tubu, unapotubu unaruhusu damu ya Yesu kufuta dhambi zako. Watu wangeelewa umuhimu wa toba shetani na mapepo yake yasingepata nafasi ya kuwatesa watu.

Mtume na Nabii : Josephat Elias Mwingira.

Comments