Karibu
tujifunze jukumu la kufanya kwa wanafunzi wa YESU KRISTO.
Wanafunzi wa
YESU KRISTO wa zamani walitimiza jukumu lao la uanafunzi na ndio maana kwa
kupitia wao Injili ambayo maana yake ni habari njema ilitufikia sisi. Baada ya
sisi kufikiwa na injili tunatakiwa pia injili hiyo ya YESU KRISTO iwafuate na
wengine kupitia sisi.
Yohana
4:39-42 ‘’ Na katika mji
ule Wasamaria wengi walimwamini(YESU) kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia
kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. Basi wale Wasamaria walipomwendea(YESU),
walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu
ya neno lake. Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya
maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu
ndiye MWOKOZI wa ulimwengu. ‘’.
-Kushuhudia
hakuhitaji karama bali watu wote waliookoka wanatakiwa kuwashuhudia na wengine
habari za YESU, Mama huyu msamaria alishuhudia na ndio maana wote
aliowashuhudia walimwendea YESU na wengi sana wakaokolewa. Mama huyu ni mfano
wa wote waliookoka maana BWANA YESU ametuokoa sisi ili yeye YESU akaguse na
maisha ya wengine kupitia sisi.
-Ndugu
hujaokolewa ili uende mbinguni bali umeokolewa ili uende duniani kugusa maisha
ya wengine nao waokoke. Kama ungeokoka ili uende mbinguni basi ungekuwa umeshaenda
baada tu ya kuokoka. Lakini sasa mbinguni utaenda tu maana umeokoka lakini kwa
sasa BWANA aliyekuokoa anataka awaokoe na wengine kupitia wewe.
Mathayo
22:14 ‘’ Kwa maana waitwao ni wengi,
bali wateule ni wachache. ‘’
-Wateule ni
wachache kwa sababu ni wachache tu wanaopenda kutenda mambo ya MUNGU.
Injili
ambayo YESU KRISTO sio sehemu ya injili hiyo basi haina mpango wa kuwapeleka
watu mbinguni.
-Mahubiri
yeyote ambayo YESU KRISTO sio sehemu ya mahubiri hayo, hayo hayalengi watu
wapate uzima wa milele.
Makanisa
mengi siku hizi watumishi wako busy kuhubiri Baraka, mafanikio, siku mfano
sabato, kumhubiri Mariam n.k. Lakini ndugu zangu tambueni kwamba Anayeokoa ni
BWANA YESU pekee(Yohana 14:6, Matendo 4:12).
Hakikisha YESU anakuwa sehemu ya mahubiri yako kila siku. Malaika
mbinguni hawafurahi kwa sababu kuna mtu kabarikiwa gari, kafunga ndoa au kasali
siku Fulani bali malaika wanafurahi kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja akitubu
na kumpokea BWANA YESU.
Warumi 12:1
‘’ Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake MUNGU, itoeni miili yenu iwe
dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza MUNU, ndiyo ibada yenu yenye
maana. ‘’
-Mwanafunzi
lazima afuate mafundisho ya mwalimu wake. Kama kuna mwanafunzi basi na Mwalimu
pia yuko. Sisi ni mwanafunzi wa YESU KRISTO.
Mathayo
28:19-20 ‘’ Basi, enendeni, mkawafanye
mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO
MTAKATIFU; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi
nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. ‘’
-Wanafunzi
wa YESU ni wale waliofundishwa na YESU.
-Wanafunzi
wa YESU ni wale wanaojifunza Neno la MUNGU na kulitendea kazi.
-Wanafunzi
wa YESU ni wale ambao hawasikilizi neno tu bali wanatendea kazi kile
walichojifunza. Yakobo 1:22 ‘’ Lakini
iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
‘’
-Wanafunzi
wa YESU huliishi neno la MUNGU.
Mwalimu
alisema kwamba wanafunzi wake waende duniani kote wakaihubiri injili kwa kila
kiumbe. Kazi yao ni kuhubiri, kazi ya kuokoa ni ya MUNGU. Jukumu la wanafunzi
ni kusema tu ila atakayeamini na kutii na kumpokea BWANA YESU ataokoka.
-Tumeambiwa
‘’twende’’ hiyo sio ombi ila ni amri tumepewa.
Ndugu yangu,
naomba ujiulize swali hili ya kwamba je wewe ni mfuasi wa YESU? au ni
mwanafunzi wa YESU?
Kuna tofauti
ya mfuasi wa YESU na mwanafunzi wa YESU.
-
Mfuasi
wa YESU Biblia inamtaja hivi Luka 9:57-62 ‘’ Nao walipokuwa wakienda njiani,
mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata ko kote utakakokwenda. YESU akamwambia, Mbweha wana pango, na
ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa
chake. Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, BWANA, nipe ruhusa kwanza niende
nikamzike baba yangu. Akamwambia
Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa MUNGU. Mtu
mwingine pia akamwambia, BWANA, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza
nikawaage watu wa nyumbani mwangu. YESU akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake
kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa MUNGU. ‘’
Ndugu kama wewe ni mfuasi tu wa YESU lazima utakuwa na udhuru
mwingi. Wafuasi hukwepa majukumu ya kushuhudia habari njema, wafuasi hudhani
kwamba aliyeitwa ashuhudie ni mchungaji tu na wazee wake wa kanisa. MUNGU
hataki wafuasi basi wanafunze kweli kweli.
-Mwanafunzi ni tofauti na mfuasi. Yohana 8:31-32 ‘’ Basi YESU akawaambia wale Wayahudi
waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli
kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. ‘’
Wanafunzi wanatakiwa wakae ndani ya YESU tena wakae katika
kusudi lake la injili.
YESU peke yake ndiye wa kumsikiliza. Nje na YESU hakuna
uzima, BABA wa mbinguni anamshuhudia hivi ‘’
Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu,
Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. -Marko 9:7‘’.
Ndugu zangu uzima
una YESU KRISTO pekee, Wafilipi 2:5-9 ‘’ Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu
ambayo ilikuwamo pia ndani ya KRISTO YESU; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna
ya MUNGU, naye hakuona kule kuwa sawa na MUNGU kuwa ni kitu cha kushikamana
nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana
mfano wa wanadamu; tena,
alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,
naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena MUNGU alimwadhimisha mno,
akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
‘’ .
Ndugu zangu hakuna jina kama jina la YESU KRISTO.
-Kwa jina la YESU KRISTO tunaokolewa na kufunguliwa kutoka
kwenye vifungo vya shetani.
-Kwa jina la YESU tumeokolewa.
-Kwa jina la YESU tunashuhudia habari njema za wokovu.
-Hakuna jina kama jina la YESU KRISTO.
-Jina la YESU ndilo jina pekee ambalo shetani anaogopa.
Kama umeokolewa hakikisha tu unawashuhudia wengine habari
njema za ufalme wa MUNGU. Ni jukumu lako wala usinyamaze na wala usiogope.
Usikubali kuwa mfuasi bali hakikisha unakuwa mwanafunzi wa
YESU aliye kamili kumtii Mwalimu wake. MUNGU aliwapenda wanadamu ndio maana
akamtuma Mwanaye YESU KRISTO ili kila anayemwamini asipotee bali awe na uzima
wa milele.
Yohana 3:16-21 ‘’ Kwa
maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma
Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu
hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru
imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao
yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye
nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye
nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. ‘’
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Comments