BAADHI YA HAIBA YA SIFA ZA SANGWINI

Na Mchungaji na Mwalimu Peter Mitimingi, Huduma ya VHM.

1. Hajui kununa na mara nyingi haishiwi na maneno ya kuweka hali ya changamko.
2. Hapendelei kujitenga hasa katika kufanya kazi. Anafanya kazi vizuri mahali penye watu wengi.
3. Kwa asili si mtu wa kujiamini sana ila kutokana na hali yake ya uchangamfu huwafanya wengi kumwamini na kumpa nafasi katika utendaji hata kama nafasi hiyo hana uwezo nayo.
4. Ni mtu wa kupenda hafla na tafrija, kwa Sangwini, ni kusema maisha yawe ni hafla bila vipindi vya huzuni.
5. Ni mtaalamu wa kuanzisha na kuendeleza mazungumzo na kuwafanya wengi washiriki.
6. Anapenda sana kukaa na watu, kwa ufupi ni mtu wa watu na watu wengi humkubali.
7. Ni muongeaji na mchekeshaji sana. Mahali alipo Sangwini hapo kucheka ni lazima hata wale wenye tabia ya kutocheka wakikutana na Sangwini lazima wacheke tu.
8. Ana nafasi kubwa sana katika jamii kwani hupokelewa kwa urahisi sana hasa na watoto.
9. Ni mburudishaji mzuri sana, akiwepo furaha ni lazima iwepo.
10. Anakasirika kwa haraka sana na hasira zake huisha kwa haraka pia tofauti sana na haiba ya Melankoli ambaye akikasirika unaweza hata usijue lakini kidonda hicho kikabakia moyoni kwa miaka mingi sana.
11. Anaongozwa na hisia na misisimko zaidi. Ni mwepesi sana kujiinga na vikundi mbali mbali bila hata kuchunguza na kutafakari kwa kina kwamba vimetoka wapi na vinakwenda wapi.
12. Ni mwepesi katika kuwachochea watu wengine kufanya kazi au jambo Fulani mahali popote.
13. Ni wepesi pia katika kuwachochea watu wafanye vurugu au migomo au maandamano. Na taflani inapotokea wao ndio huwa wakwanza na kuwaacha wengine wakipata mkongoto wa polisi. Hasa kundi la Fregmatik ndio huwa wanyonge wa kina Sangwini.
14. Wanapenda sana umaarufu na kutambulika katika jamiimahali popote wanapokwenda.
15. Maelezo ya ujumla.Ni mtu wa kupenda kutoka. Ni mtu wa kupenda hafla na tafrija, kwao ni kusema maisha yawe ni hafla bila vipindi vya huzuni. Ni mburudishaji mzuri sana, akiwepo furaha ni lazima iwepo.
Kesho nitakuelezea Tabia za Sangwini katika mambo yanayohusu Pesa huwa wakoje
Kama umebarikiwa sema amen.

Comments