BIASHARA YA MIILI NA ROHO ZA WANADAMU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Na Godfrey Miyonjo.
“Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” 1kor 6:20.
“Basi Bwana, MUNGU asema hivi, Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, name nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; name nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege” EZEKIELI 13:20
BWANA YESU asifiwe sana.
Ninatamani kila mmoja wetu afahamu siri hii ambayo ni ya ajabu sana.
Ninatamani kila mmoja atambue kuwa katika ulimwengu wa roho kuna biashara inaendelea, na miongoni mwa bidhaa zinazouzwa ni MIILI NA ROHO ZA WANADAMU.
Kuna wafanya biashara wakubwa wawili walio katika uhindani, ambao ni YESU KRISTO na Shetani.
Shetani yeye ni mwivi (mwizi), anafanya biashara kwa njia ya unyang’anyi, ubabe, uvamizi, ulaghai, N.K.
Hata sasa bado anamiliki BAADHI YA MIILI NA ROHO ZA WANADAMU kwa njia hii ya Uvamizi.
Amewateka baadhi ya watu wa Mungu (watu walioumbwa na Mungu) na kuwatumikisha katika kampuni yake ya UPOTEVU inayoongozwa na mapepo.
Katika ulimwengu wa roho wana wa upotevu humtumikia shetani kwa jinsi ya rohoni au mwilini.
Wanafanya biashara ya kuuza na kununu bidhaa mbalimbali ikiwemo na MIILI NA ROHO ZA WANADAMU.
Ninayasema hayo kwasababu imeandikwa katika kitabu cha UFUNUO kuwa ipo siku biashara yao itafungwa, nao watamboleza kwakuwa bidhaa zao zitakosa soko.
UFUNUO 18:11-13.
11 “Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwambolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;”

12 “bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na Hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba na cha chuma, na cha marimari;”
13 “na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, farasi, na magari, na MIILI NA ROHO ZA WANADAMU”
MIILI NA ROHO ZA WANADAMU ni bidhaa adimu sana katika ulimwengu wa roho.
Kwakuwa hakuna mtu anayeweza kumtumikia Mungu akiwa nje ya mwili, ndiyo maana nasema ni bidhaa adimu.
Lakini atukuzwe Mungu kwa upendo wake mkuu na wa ajabu kwa wanadamu, kwakuwa anayafunua haya.
Mungu kupitia kampuni yake ya WOKOVU inayoongozwa na YESU KRISTO ameikomboa (ameinunua) MIILI NA ROHO kwa DAMU YA THAMANI iliyomwagika pale msalabani.

Kupitia DAMU ya BWANA YESU, gharama yote juu ya ukombozi (ununuzi) wa miili na roho za wanadamu wote imelipwa.

Naye YESU KRISTO yuko kazini kila siku, kila saa, kila dakika, kila sekunde ili kuhakikisha wanadamu wote wanakombolewa (wananunuliwa) kutoka upotevuni.
Mungu haokoi (hanunui) ROHO peke yake, bali anaokoa (ananunua) na MWILI pia.
Mungu akijifunua kwa mwanadamu awayeyote anakomboa (ananunua) vyote, yaani MWILI NA ROHO vyote vinatumika kwake.
Kama wewe ulikuwa bado haujalijua hili,
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaa……………………………………………………………..

Salimisha MWILI WAKO NA ROHO YAKO kwa BWANA YESU leo ili usiendelee kuwa bidhaa ya shetani.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu)

Comments