BWANA HUUTAZAMA MOYO

Na Godfrey Miyonjo.

……..BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu hutazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo………… 1SAMWELI 16:7.
BWANA YESU asifiwe sana.
Wapendwa asomaye na afahamu maana ya neno hili “BWANA HUUTAZAMA MOYO”
Imezoeleka kuwasikia maharamia wa IMANI (wapagani/wachukizao) wakilitumia neno hili kuhalalisha uovu wao.
Mtu anapofanya madudu (mambo yasiyompendeza Mungu/uovu) hujificha chini ya andiko hili.
Unakuta mtu analewa kila siku ukimwambia Mungu hapendezwi na tabia hii anasema “BWANA HUUTAZAMA MOYO”
Mtu anatembea uchi (anavaa mavazi yasiyomsitiri nyeti zake) ukimwambia utamsikia “BWANA HUUTAZAMA MOYO”
Mtu anaabudu na kuyatumikia masanamu, ukimwonya anasema “BWANA HUUTAZAMA MOYO”
Mtu mzinzi/mwasherati ukimwonya anasema
“BWANA HUUTAZAMA MOYO”

Mtu mtukanaji na msengenyaji ukimwonya anasema “BWANA HUUTAZAMA MOYO”
Yaani hili neno “BWANA HUUTAZAMA MOYO” limekuwa kichaka cha waovu.
Wengi hujificha chini ya neno hili huenda kwa kujua au kwa kutokujua kuwa wanamchukiza Mungu.
Ni kweli kuwa Mungu hatazami sura ya mtu bali HUUTAZAMA MOYO, Kwa sababu kila tendo linalofanywa na mtu asili yake ni ndani ya moyo wake.
Yaani mtu akitenda mema, hayo mema chanzo chake ni moyoni mwake, na mtu anapotenda mabaya (machukizo) nayo yametoka ndani ya moyo wake.
Ndiyo maana neno linasema “Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu” MATHAYO 5:8.
Kinyume cha mstari huu ni “ole wenye moyo mchafu maana hao hawatamwona Mungu”
Huu ndiyo ukweli kwamba:
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa unawaza kutembea uchi.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa unafanya ibada ya sanamu.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa mwizi.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa mzinzi.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa mtukanaji.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa msengenyaji.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa mlevi.
Huwezi ukawa na moyo safi halafu ukawa mzushi.
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa……………. Ni kweli “BWANA HUUTAZAMA MOYO” lakini waovu nao hutazamwa kwa jinsi ya uovu wao, na hakuna aliye mwovu mwilini akawa msafi moyoni.
Ndiyo maana imeandikwa “Linda moyo wako kuliko yote ulindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” MITHALI 4:23.
Kama wewe uliruhusu mabaya yatawale moyo wako, amua leo kuusafisha kwa damu ya YESU, YESU atakusamehe kabisa, kwamaana alisulubiwa kwa ajili yako.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu).

Comments