ELIMU ANAYOTUMIA SHETANI ILI KUJIPATIA MATEKA

Na Mtumishi Alex Simion Makuli.
Bwana YESU asifiwe. 
Hakuna kitu kibaya kama kuwa mateka/mtumwa wa shetani. 
Elimu ya mateka ni elimu ambayo shetani anaitumia kupitia majenti/watumishi wake ktk kupotosha kweli ya MUNGU. 

Hii ni elimu ambayo haitokani na Neno la MUNGU, hii ni elimu ya mpinga KRISTO. Mara nyingi watu wamejikuta wakinaswa na elimu hii aidha kwa kujua au kwa kutokujua. Lakin MUNGU wetu anatupenda sana ndio maana anatupa angalizo/tahadhali juu ya elimu hii. "KOL 2:8 ANGALIENI MTU ASIWAFANYE MATEKA KWA ELIMU YAKE YA BURE NA MADANGANYO MATUPU, KWA JINSI YA MAPOKEO YA WANADAMU, KWA JINSI YA MAFUNDISHO YA AWALI YA ULIMWENGU, WALA SI KWA JINSI YA KRISTO". 

 Mtu wa MUNGU, Neno la MUNGU ndio kweli yote na kitu chochote ambacho hakitokani na Neno la MUNGU basi hii ndiyo elimu ya dunia hii, elimu ya mapokeo ya wanadamu, elimu ya mafundisho ya wanadamu, elimu ya kipagani. MUNGU atusaidie sana na atupe macho ya Rohoni. Kumbaka "YESU NI MWOKOZI" kama hujampokea, huu ndio wakati wako sasa.

  "UONGO" ni mojawapo ya elimu/mbinu ambayo shetani huitumia katika kujipatia mateka. Hii ndiyo mbinu/elimu kubwa kuliko zote ambayo adui amejikita ktk kujipatia mateka.

 Shetani ndiye baba wa uongo, "YOH 8:44" Biblia inasema "NINYI NI WA BABA YENU IBILISI, NA TAMAA ZA BABA YENU NDIZO MPENDAZO KUZITENDA, YEYE ALIKUWA MUUWAJI TANGU MWANZO, WALA HAKUSIMAMA KATIKA KWELI, KWA KUWA HAMNA HIYO KWELI NDANI YAKE, ASEMAPO UONGO HUSEMA YALIYO YAKE MWENYEWE, KWA SABABU YEYE NI MWONGO NA BABA WA HUO". Shetani kupitia majenti/watumishi wake hutumia mbinu hii ya uongo katika kupotosha kweli ya MUNGU, shetani anajaribu kutungeneza uongo ili ufanane na ukweli, lakin ndani yake kuna siri kubwa ya kujipatia mateka. 
Wakati mwingine shetani hutumia manabii wa uongo huku wakitumia welevu na uzushi wa kupoteza na kufundisha maneno waliyojitungia wenye ili kujipatia mateka(2PET 2:1-3). 
Barikiwa sana na tafakari hii. 
By Alex Simion Makuli

Comments