HAIBA YA SANGWINI NA MAMBO PESA

Na Mchungaji Peter Mitimingi wa huduma ya VHM

1. Sangwini sio mtu wa kufuatilia vitu kwa undani na kwa kina.
Sangwini ni mtu anayefuatilia mambo kwa juu juu na kwa haraka haraka. Sio mtu wa "details" kutopenda kufuatilia vitu kwa undani kunaweza kumsababishia Sangwini kuharibikiwa kifedha.

2. Ni mara chache sana Sangwini kuwa na BAJETI.
Unapozungumzia swala la kufanya bajeti ni la kundi lingine lakini sio Sangwini. Ni wachache sana wanaoweza kufikiria swala la bajeti. Sangwini anapata pesa sasa anaifanyia matumizi hapo hapo hata kabla hajafika nyumbani usishangae anaingia home hana kitu mkononi ameshaitumia yote.

3. Sangwini wengi sio wazuri katika matumizi na usimamiaji wa pesa.
Ni watu wanaopenda sana kutumia pesa bila kujali sana matokeo ya baadaye yatakuwaje. Pesa za ada ya watoto anaweza akaita marafiki wakaenda kula nyama choma na vinywaji na akawalipia woote waliokuja pale kumbe ni ada za watoto. Akifika home hana kitu anaulizwa na mwenzi wake zile pesa zipo wapi anaanza kutoa visingizio na kupotezea. Kama umeoa au umeolewa na Sangwini usipende kumfanya awe msimamizi mkuu wa bajeti, utaharibikiwa. Anaweza asifanye lolote au akafanya maamuzi ya hali ya chini.
4. Sangwini Anaangalia Mambo ya Leo na Hajali Kuhusu Kesho.
Sangwini hupenda kujishughulisha sana na mambo ya sasa au leo tu humfanya sangwini ashindwe kujiandaa kwa maisha ya baadae kama vile kustaafu, au ada za shule kwa wanae.
Sangwini wengi ndio wale wanaosema "ukipata tumia na ukikosa jutia" Akipata pesa anatumia bila kujali kwamba kesho kuna mambo muhimu yatakayo hitaji hizo pesa. Mfano mzuri aangalia wakati wa Sikukuu za mwisho wa mwaka. Sangwini wengi huangusha ng'ombe, mbuzi, teketeza kuku za kutosha na kula ile vijana wanaita ya kufa mtu na matanuzi makubwa katika mambo ya burudani na sherehe kubwa kubwa. Sikukuu zinaisha unakuja mwezi JANUARY ada zinatakiwa. kodi ya nyumba inatakiwa, Uniform za watoto zinatakiwa, chakula cha mwezi mzima kinatakiwa, nauli za kwenda kazini nk. Sangwini mfukoni hana hata nauli za daladala halafu kila anayekwenda kumkopa hana pesa na watu wanamshangaaa maana Disemba alialika watu na majirani ana akawa anawaambia kuleni tani yenu na hata kubeba pilau ruksa.

5. Sangwini si wazuri katika kutunza mahesabu au kulipa Ankara zao kwa wakati.
Ni Sangwini wachache sana wenye uwezo wa kutunza mahebu ya matumizi ya pesa na risiti. Mafisini ndio wanao ongoza kukorofishana na wahasibu au mabisi wao pale wanapotakiwa kutoa mahesabu na risiti ya matumizi ya pesa walizopewa.

6. Sangwini wengi Hupenda Vitu vya Hali ya Juu kwajili ya kutunza Sifa na Umaarufu Wao.
Kwa sababu hupenda sana kusifiwa na kutambuliwa au kuthaminiwa basi sangwine hufanyia sifa katika mitindo (fashions) kila mtindo usimpite na kununua magari ya kifahari, simu kalikali za gharama kubwa za kuingilia maeneo ya matukio mapafyumu ya gharama kubwa hata kama mfukoni hana hela ya mafuta wala daladala. Ukimuona unaweza kusema huyu kwenye akaunti yake anaweza kuwa na kama milioni 100 hivi kwa uchache kumbe hana hata akaunti popote kila kinachopatikana kinatumika chote.

7. Sangwini anaongozwa na Hisia Zaidi
Kwa kuwa watu hawa huongozwa sana na hisia pasipo na uhalisia, sangwini hujikuta wananaua vitu bila kufanya utafiti wala maamuzi ya kina. Anatoka nyumbani au kazini anakwenda mahali anakutana na machinga wa kwanza anamshawishi anaamua kutoa pesa amabayo haikuwa imepangiwa kununua vitu anainunulia pocho Anakwenda mbele kidogo anakutana na muuza viatu anamshawishi na kummzia anakwenda mbele kidogo anakutana na muuza simu barabarani anamshawishi kua hii galax nimeikwapua kwa muhindi ni ya milioni ila wewe nipe kilo tu anatoa pesa anaunua kufika home ana kitu mshahara umeishia kwenye vitu ambavyo waha havikuwa nitaji. Wazungu wanamsemo: . "Do you want it, or do you need it? You may want something which you really don't need it.

8. Matumizi ya Sangwini ni Makubwa Kuliko Kipato
Sangwini anamatumizi makubwa yasiyo zingatia kipato chake. Kwasababu kipato ni kidogo kuliko matumizi, basi hujikuta wakikopa sana ili kuendelea kutunza ile hali yake ya umaarufu kwa kuongeza mkopo ili kufidia kipato chake kidogo ambacho hakitosherezi.
9. Sangwini ni Wakarimu Sana na Ukarimu wao Huwagharimu.
Sangwini ni wakarimu sana na wengine ukarimu wao umepitiliza.
Kwa kuwa ni mtu mkarimu sana jambo hili linaweza kumfanya awe na matumizi makubwa kwa ajili ya kuwapa watu zawadi, kuwapa watu ofa mbalimbali ambazo wakati mwingine hawajaziomba.
10. Sangwini ni Mtaalamu wa Kukopa lakini ni Mgumu sana Katika Kulipa Alichokopa.
Sangwini anaweza kwenda kumkopa mtu huku akijua kabisa hatamlipa. Mara nyingi Sangwini amekuwa akigombana sana na waliomkopesha kuwa kuwa msumbufu kulipa madeni ya watu. Tatizo linakuja kwasababu kama nilivyosema kuwa Sangwini anaishi kwa matumizi makubwa kuliko kipato na hakopi kwa mtu mmoja anakopa kwa watu kibao na ukweli hana uwezo wa kulipa hayo madeni.
Mpendwa sijui kama umenielewa hapo.
Endelea kufuatilia nitakueleza namna ya kumsaidia Sangwini ambaye anatatizo katika mambo ya pesa.
Kama umebarikiwa sema AMEN...

Comments