HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YA WALIOMWAMINI YESU KRISTO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze.
-Neno "Hukumu" Katika Biblia Limetafsiriwa Kutoka Kwa Neno La Kiyunani "Krisis" Ambalo Ni Shina Ya Neno La Kiingereza "Crisis" Maana Yake Ni Maonjo Ya Kusimama Hukumuni Pamoja Na Wasioamini. 
-Cha Ajabu Ni Kwamba WALIOOKOKA Hawatasimama Kwenye Hiyo Crisis Maana Kesi Yao Ilishafutwa Tangu Siku Ile Wamempokea BWANA YESU Kama BWANA Na MWOKOZI Wao. 
-Kuokoka Ni Muhimu Sana Ndugu Zangu. Biblia Inafafanua Hivi Kuhusu Crisis Niliyoisema Hapo Juu, Wakolosai 2:13-17 " Na Ninyi Mlipokuwa Mmekufa Kwa Sababu Ya Makosa Yenu Na Kutokutahiriwa Kwa Mwili Wenu, Aliwafanya Kuwa Hai Pamoja Nae, Akiisha Kutusamehe Makosa Yote; Akiisha Kuifuta Ile Hati Iliyoandikwa Ya Kutushitaki Kwa Hukumu Zake, Iliyokuwa Na Uadui Kwetu; Akaiondoa Isiwepo Tena, Akaigongomea Msalabani; Akiisha Kuzivua Enzi Na Mamlaka, Na Kuzifanya Kuwa Mkogo Kwa Ujasiri, Akizishangilia Katika Msalaba Huo. Basi, Mtu Asiwahukumu Ninyi Katika Vyakula Au Vinywaji, Au Kwa Sababu Ya Sikukuu Au Mwandamo Wa Mwezi Au Sabato. "
 -Ndugu Hakisha Unampokea BWANA YESU Leo.

 Kwa wateule,Baada Ya Kuokoka Hakimu Wa Roho Zetu Anasema "Dhambi Zao Na Uasi Sitaukumbuka Tena Kabisa-Waebrania 10:17". 
-Kuokoka Ni Muhimu Sana Kwa Kila Mwanadamu. 
-Kuokoka Ni Kumpokea BWANA YESU Kama BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako(Warumi 10:9-11,  Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. ) Kisha baada ya kuokoka unatakiwa kuanza Kuliishi Neno La MUNGU na kujifunza neno la MUNGU (Yohana 8:31-32, Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
-Kweli inaweka huru na kweli ni Neno la MUNGU.
-Kuokoka Ni Muhimu Sana,Na Biblia inasema kwamba  "Kila Atakayeliitia Jina La BWANA Ataokoka-Warumi 10:13.
-Kila atakayeliitia jina la BWANA YESU ataokoka.
-Jina la YESU KRISTO ni jina muhimu sana kwa ajili ya kila mwanadamu, ni jina la msaada mkuu na ni jina la uzima wa milele, kujitenga na YESU ni kujitenga na uzima wa milele na kumkataa YESU ni kukataa mbinguni.

-Usikubali Tu Kuishi Kwa Sababu Unaishi Bali Ishi Kwa Sababu KRISTO Anaishi Ndani Yako.
Kuna watu na baadhi ya dini na madhehebu huwa wanaenda kwa kubahatisha wakisema kwamba hakuna kuokoka duniani.

Watu hao  Wanaongojea Siku Ya Mwisho Ndipo Wapate Kufahamu Ikiwa Wameokoka Au Wamelaaniwa. Hao Wanakuwa Bado Hawajauelewa Wokovu Hata Kidogo. Hakuna Hukumu Juu Ya Wateule(warumi 8:1, Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU. )
-Kama hakuna hukumu kwa aliyempokea YESU na kuanza kuliishi neno la MUNGU kwanini tena kuogopa na kupelekea kutokuwa na uhakika wa uzima? Biblia sehemu kubwa imehakikisha kabisa kwamba ukizingatia taratibu za wokovu hakika umeokoka, sio tukio la baadae bali la muda huu huu, BWANA YESU alisema ''Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani-Yohana 5:24'' . Biblia inatoa uhakika wa Wokovu baaya ya wewe kumwamini YESU.
Kumwamini YESU ni 
1. Kumkubali kama Mwokozi.
2. Na Kumtegemea kama BWANA mshindi wako. 

Biblia inasema ''MUNGU alitupa uzima wa milele sio kwamba MUNGU atatupa baadae bali sasa, pale tu tunapompokea BWANA YESU''  1 Yohana 5:11-12 '' Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba MUNGU alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa MUNGU hana huo uzima. ''
-uzima wa milele ni halisi kabisa ukiwa na Wokovu wa BWANA YESU, Sio ule uzima wa kujifariji tu huku unatenda maovu ambao uzima huo ni batili, bali ni ule uzima wa milele ambao unatokana na kumtii MUNGU .

BWANA YESU Anasema Ajaye Kwake Hatamtupa Nje Kamwe(Yohana 6:37,Wote anipao BABA watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. ) Na Ndio Maana ROHO MTAKATIFU Hushuhudia Pamoja Na Roho Zetu Kwa Tumeokoka Na Tu Watoto Wa MUNGU(Warumi 8:16,ROHO mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa MUNGU;   )
-Wokovu ni muhimu sana.
-Wokovu ni kwa ajili yetu na watoto wetu.
-Maisha ya Wokovu ni maisha ya washindi.
-Ishi maisha ya wokovu siku zote za maisha yako.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments