HAKUNA UZIMA WA MILELE PASIPO KUOKOLEWA NA BWANA YESU.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze jambo la muhimu sana yaani Wokovu.
Leo sitaki niongee sana bali nataka tu Biblia ndio iongee yenyewe kuhusu WOKOVU wa BWANA YESU.
Maisha ya wokovu ni maisha wanayoishi watu waliookoka kikweli kweli.
Kama hujaokoka tambua kuanzia leo kwamba anayeokoa ni BWANA YESU peke yake.
Karibu uone uthibitisho wa Biblia Takatifu.

1.  Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. - Yohana 3:16.
-YESU alikuja ili tu wewe usiende jehanamu bali uende uzima wa milele, ni wajibu wako kumpokea leo.
2.  kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa MUNGU; Warumi 3:23.

-Hakuna anayeweza kujikamilisha na kuwa safi ila ukamilisho hufanya na YESU KRISTO.
3.  Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu. - Warumi 6:23.

-Uzima wa milele ni katika KRISTO YESU.
4.  YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. - Yohana 14:6.

-hakuna mwanadamu hata mmoja anayeweza kwenda uzima wa milele kwa njia yeyote nje na YESU KRISTO.
5.  Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; - Yohana 1:12.

-Kumpokea YESU na kuliishi neno lake ndio kibali cha uzima wa milele
6.  YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa MUNGU. - Yohana 3:3.

-Bila kuzaliwa mara ya pili kwa kumpokea BWANA YESU huwezi kuingia ufalme wa MUNGU. Bila kuzaliwa kwa maji na kwa ROHO MTAKATIFU huwezi kuingia uzima wa milele.
7.  Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. - Waebrania 9:22.

-Pasipo damu hakuna ondoleo la dhambi, dhamani damu ya kondoo ilitumika kufunika dhambi lakini kwa sasa Damu ya YESU wala haifuniki dhambi bali inafuta dhambi zote baada ya kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yako.
8.  akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. - Mathayo 18:3.

-Bila kujikana na kuacha majukizo na viburi vya uzima huwezi kuingia uzimani.
9.  Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. - Ufunuo wa Yohana 3:20.

-Leo BWANA YESU anagonga kwenye mlango la moyo wako, ukifungua mlango kwa kumpokea utapata uzima. ni kazi yako kumruhusu BWANA YESU aingie moyoni mwako.
10.  Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. - 1 Yohana 1:9.

-Ukitubu leo kwa MUNGU katika KRISTO YESU hakika jina lako litaandikwa mbinguni kwenye kitabu cha Uzima.
11.  Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. - Warumi 10:9,10,13.

-Unapata haki ya uzima kwa kinywa chako kupitia kumkiri BWANA YESU na kumpokea kama Mwokozi binafsi ya maisha yako.
12.  Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. - Waefeso 2:8,9.

-Uliyeokoka tambua kwamba hujajiokoa mwenyewe bali umeokolewa na BWANA YESU kwa neema yake kwa njia ya imani kwake.
13.  si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na ROHO MTAKATIFU; - Tito 3:5.

-ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana kwa kila mwenda mbinguni, kama kuna kanisa hawamtaki ROHO MTAKATIFU usije ukajiunga na kanisa hilo maana ni kanisa la shetani.
14.  Wakamwambia, Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. - Matendo ya Mitume 16:31.

-Kuokoka ni halisi ukiwa duniani. wanaosema hakuna kuokoka duniani ni kwasababu wao hawajaokoka hivyo wanawazuilia na waumini wao kuokoka.Ukimwamini BWANA YESU kwa kumpokea na kuliishi Neno la MUNGU hakika unakuwa umeokoka. kumbuka hakuna kuokoka baada ya kufa, Wokovu ni sasa, baada ya kifo ni hukumu.
15.  Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU inamkalia. Yohana 3:36.

-Kumkataa BWANA YESU ni kukataa uzima wa milele.
16.  Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. - Yohana 10:28.

-Hakuna anayeweza kukutoa kwa YESU labda tu ujitoe wewe mwenyewe kwa kwenda kwa shetani.
17.  Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. - 2 Wakorintho 5:17.

-Ukiwa ndani ya KRISTO umefanyika kiumbe kipya kilichoumba na MUNGU kiroho ndio maana unaitwa mwana wa MUNGU.
-USIKUMBUKE YA ZAMANI NA WALA USIIFUATISHE DUNIA.

Naamini umejifunza kitu kizuri sana ambacho ni Wokovu.
-Kabla watu hawajampokea BWANA YESU huwa wanahesabika kwamba ni watenda dhambi na wamepungukiwa na utukufu wa MUNGU.
-Ukiokoka hakuna hukumu tena juu yako.
-Pasipo damu ya YESU KRISTO huwezi kusafishwa dhambi 
-Tunaokoka baada ya kumkiri BWANA YESU kwa vinywa vyetu kwamba awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu.
-Hakuna anayeweza kukutoa kwa YESU.
-Ukiwa ndani ya KRISTO unakuwa kiumbe kipya, ya kale yanafutwa na sasa unakuwa mwana wa MUNGU.
-Hakuna anayeweza kwenda uzima wa Milele pasipo kuokolewa na BWANA YESU.

-Soma Biblia kila siku ili ujifunze kusudi la MUNGU juu ya maisha yao.
-Soma Biblia ili ukue kiroho.
-Soma Biblia ili upate mamlaka zaidi ya kimungu.
-Soma Biblia ili adui akuogope.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments