IDARA NDOGO SABA (7) ZA ROHO MTAKATIFU


Idara hizi saba, ni ofisi ndogo saba zilizo chini ya Roho Mtakatifu Ufunuo4:5
Hizi ni roho saba za Mungu aliye hai roho hizi saba za Mungu aliye hai ni muhimu sana, kwa uhai na maendeleo ya kanisa la Yesu Kristo hapa duniani.
Ndugu msomaji wangu fahamu neno hili kadri unavyoendelea kusoma kitabu hiki, Roho Mtatakatifu ataumba neno jema ndani yako, ufahamu wako utaangaziwa nuru Efeso 1:18 karama na huduma zitachipuka ndani yako. Kumbuka kujitakasa na kuufungua moyo wako maana yako mambo mapya mazuri yataumbika ndani yako.
Vile vile usiache kuniombea na mimi, ili nisonge mbele na kusudi la Roho Mtakatifu kwa bara la afrika na dunia litimie.
Idara hizi ndogo saba 7 za Roho mtakatifu zina anza kwa mtiririko huu ufuatao:-


1. Roho wa neema
2. Roho wa uzima
3. Roho wa kufanywa wana
4. Roho wa utakatifu
5. Roho wa maombi
6. Roho wa kweli
7. Roho wa utukufu


Idara hizi ndogo kutoka ofisi ya Roho Mtakatifu ni muhimu sana kwa kanisa la kristo Yesu hapa duniani; maana zinasaidia kuinua kiwango cha wakovu na kiroho ndani ya watumishi ili kukua na kupiga hatua
Roho hizi zinaimarisha sana wokovu na kulifanya kanisa kuwa hai kiroho. Vile vile zinasaidia kuimarisha utukufu katika huduma
Natoa wito kwa watumishi wote kumlilia na kumsihi sana Yesu ili alete tena hizi roho saba maana kwa kweli, zimepotea na udhihirisho wake haupo katika makanisa mengi, hasa yale yanayo jiita “madhehebu ya kipentekoste.


UFAFANUZI WA ROHO SABA 


1.ROHO WA NEEMA waebrania 10;29
Roho hii kutoka kwa Roho Mtakatifu huleta yafuatayo kanisani;
(a) Huleta neema ya wokovu mioyoni mwetu ili tumwamini Yesu kristo
(b) Huvuta watu waje kwa Yesu na waingie ndani ya wokovu


2. ROHO WA UZIMA Rumi 8;2
Roho wa uzima hufanya kazi ya kuleta
• Uhai wa kiroho
• Uhai wa kimwili
• Hufanya kazi ya ufufuo


3. ROHO WA KUFANYWA WANA
Rumi 8:15-20
Roho au idara hii ndogo ya Roho Mtakatifu hutusaidia kututhibitishia kuwa; sisi tu wana wa Mungu aliye hai. Kwa kupata haki ya kuwa warithi, wa mambo matukufu ya mbinguni.


4. ROHO WA UTAKATIFU
Rumi 1:4
Roho hii hufanya yafuatayo:-
Kufichua dhambi
Husababisha watu kujitakasa sana ili kuuhifadhi utakatifu ndani yetu
Ofisi hii hutumika sana na manabii, na watumishi wengi wa madhabahuni
Roho hii huleta hofu ya Mungu mtakatifu kanisani


5.ROHO WA MAOMBI
Zekaria 12:10 Roho hii, huleta kiu na shauku ya maombi
Roho hii ikikaa ndani yako utakuwa mwana maombi sana na unakuwa na uwezo wa kuomba muda mrefu bila kuchoka.


6.ROHO WA KWELI . Yohana 16:13
Roho hii hufanya kazi ifuatayo katika mwili wa Kristo Yesu. Roho hii hutumika na walimu wa mbinguni na kulifundisha kanisa na kulifikisha katika kweli yote; yaani elimu ya mbinguni, inayofundishwa na Roho Mtakatifu.
Roho hii husaidia watumishi kujua siri za ufalme wa Mungu vile vile roho hii huleta ufunuo wa neno kwa wanadamu.


7.ROHO WA UTUKUFU
1 PETRO 4:14, 2:19,20
Idara hii ndogo katika ofisi ya Roho mtakatifu hufanya kazi zifuatazo
i. Hudhirisha uwezo wa Mungu aliye hai ndanye yetu
ii. Husaidia kushinda majaribu
iii. Huleta stamina ya wokovu
iv. Roho hii hubeba utukufu uwepo na upako wa Roho Mtakatifu na kuuleta wakati wa ibada kama watu, wamejitakasa vizuri.
Roho hii huleta kufurika na Roho Mtakatifu katika ibad

Comments