IJUE HUDUMA YAKO NA ANAYTOA HUDUMA KATIKA MWILI WA KRISTO NA INAVYOTENDA KAZI (SEHEMU IV)

Na Emmanuel Kamalamo

Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru kwa siku ya leo tena kutupata uzima tele katika mwili na roho, utukufu apewe Mungu.
Leo namalizia kazi za Mtume katika mwili wa Kristo na kisha tutaangalia Huduma ya Nabii. Jana tumeangalia makundi ya mitume na sifa zao.
KAZI ZA MITUME.
1.KUPANDA MAKANISA.
Huwezi ukajiita mtume kama huna sifa za kitume.Mtume kazi yake nikwenda MJINI na VIJIJINI kufungua Kanisa/Makanisa, na kuyasimamia mpaka yanukua.
Atalifundisha kanisa kama MWALIM katika MSINGI wa Imani ya Kristo na kulichunga kama MCHUNGAJI na kuhakikisha anapata Mchg.wa kulichunga kanisa hilo kisha yeye huondoka. (Mdo 14:21-23)
Na anapoondoka kwenda kwingine ni lazima arudi kuangalia makanisa aliyoyafungua yanaendrleaje.

2.KUWAENDELEZA VIONGOZI WAPYA KATIKA MAFUNDISHO.
3.MTATUZI WA MATATIZO (MIGOGORO) KATIKA KANISA.
4.HUANDAA UTARATIBU KATIKA HUDUMA.
Kwa mantiki hiyo unaposema umeitwa katika Huduma ya KITUME hakikisha zile SIFA na KAZI za kitume unazo na zinafanya kazi. Huwezi kusema wewe ni mtume alafu unakaa kwe kanisa miaka 15 hutoki huachi wachungaji mahari ukaenda kwengine. Paulo aliwaacha watumishi mahari alipofungua kanisa miongoni mwao ni Timotheo,Etasto,Gayo,Alistarko hawa walikuwa watumishi wa Mtume Paulo.
.HUDUMA YA NABII
Na bii ni Mtu mwenye UFAHAMU wa ndani zaidi sana katika mambo ya Kiroho.Ana uwezo kusikia toka kwa Mungu moja kwa moja, na kupewa mambo yajayo.
JE, KILA ANAYETOA UNABII NI NABII?
Hapana, si kila anayetoa unabii kanisani ni nabii.Kuna tofauti ya UNABII NA NABII.
>UNABII -Anatao mtu yeyote kwa kutumiwa na ROHO MTAKATIFU kwa wakati huo kutoa ujumbe. Ni karama ya Roho Mtakatifu.

>NABII -Ni mtu anayetumika katika Huduma ya Nabii, ni kama ofisi yake. Mfano, si kila anaye shika chaki nakuandika ubaoni ni Mwalimu.
Nabii lazima aambatane na karama zifuatazo.
>NENO LA HEKIMA
.Karama hii umsaidia kuwa na HEKIMA na UFUNUO wa ki-Ungu kupitia Roho Mtakatifu.

>NENO LA MAARIFA
.Karama hii umsaidia kuwa na UFUNUO wa Mungu kupitia Roho Mtakatifu kujua mambo yaliyopo au yajayo.Pia kuona katika maono saa hiyo iyo wakati jambo linatendeka.

3.KUPAMBANUA ROHO.
.Karama hii umsadia kujua na kupambanua ROHO WA KWELI NA ROHO WA SHETANI. Mtu anaweza akatoa unabii ndani ya kanisa lazima hii karama ipambanue huo unabii ni wa....
ROHO WA MUNGU
ROHO YA SHETANI
ROHO YA MTU.(Mdo 8:19-24; 13:6-12.)

-Nabii upewa ujumbe saa yoyote na mahari popote.Na
-Nabii usaidia kujua Mungu anayeabudiwa ni wa kweli.

ALAMA ZA KUMTHIBITISHA NABII.
1.Nabii uzungumza jambo lijalo na Mungu ulithibisha.
2.Nabii ana uwezo wa kiroho kumtambua mtu .
3.Nabii akitoa ujumbe unagusa roho za watu na si kuchonganisha watu.
4.Nabii utangaza hukumu ya kiungu pale inapohitajika.
HUDUMA YA MWINJILISTI.
Tunaendelea fuatana nami mpaka mpaka mwisho wa somo hili nawe utabarikiwa.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA LEO BAADA YA KUFA NI HUKUMU. Waebrania 9:27
MUNGU WANGU AKUBARIKI.

Comments