IJUE THAMANI YA DAMU YA YESU NA UITEGEMEE DAMU HIYO IKUPE UZIMA.


Na Emmanuel Kamalamo.
Shalom, shalom!
Na Mungu kwa kutupa kuiona siku ya leo, pia namshukuru Mungu kwa ajili yako pia kukupa uzima siku ya leo.
Najua hakuna asiyeijua damu ya Yesu, kila mmoja anaifahamu. Lakini neno la Mungu ni jipya kila siku.
THAMANI YA DAMU YA YESU NI NINI?
>Thamani yake ni kutununua.
Ufunuo 5:9 "..Ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa"

Pesa ikipoteza THAMANI haina uwezo wa kununua vitu vya gharama, kwa hiyo, DAMU ZA WANYAMA hazikuwa na thamani kuwanunua wanadamu walioshikiliwa dhambi, ndyiyo maana Kuhani alipokuwa anakwenda mbele za Bwana na damu za wanyama dhambi zao hazikuondolewa bali zilifunikwa.Maandiko yanasema......"MAANA HAIWEZEKANI DAMU YA MAFAHARI NA MBUZI KUONDOA DHAMBI" Waebrania 10:4.
Maana yake ni nini anaposema,..."HAIWEZEKANI" ni kwa sababu thamani yake haitoshi. Ndiyo maana mwanadamu akashindwa kuñunuliwa akabaki chini ya kifungo cha dhambi, deni likabaki pale pale,.......... kama natania kasome biblia yako utaambiwa.."LAKINI KATIKA DHABIHU HIZO LIKO KUMBUKUMBU LA DHAMBI KILA MWAKA" Waebrania 10:4.
Mtu akikwambia"WEWE UNA DHAMBI" mwambie..."MIMI SIKO CHINI YA DENI LA DHAMBI" mimi sasa ni kanisa la Kristo nimenunuliwa kwa damu isiyopungua THAMANI yake maandiko yananiambia..."...Mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenywe" Mdo 20:28.
(A) DAMU YA YESU INAONDOA
DHAMBI.

1 Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
(B) DAMU YA YESU INATUHESABABIA
HAKI.

Warumi 5:9 "Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye"
(C) DAMU YA YESU INATUPA UJASIRI
WA KWENDA MBELE ZA MUNGU.

Waebrania 10:19 "Basi, ndugu, kwa kuwa tunaujasiri wa kupangia patakatifu kwa damu ya Yesu".
MUNGU AKUBARIKI SANÀ.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA
MAANA BAADA YA KUFA NI HUKUMU
Waebrani 9:27.

Comments