KUNA MADHARA KUPANDA KWENYE MADHABAHU YENYE UWEPO WA NGUVU ZA ROHO MTATAKATIFU. KAMA HAUKO SAHIHI.

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Nafahamu kila mmoja anajua nini maana ya MADHABAHU. Na kama ulikuwa hujui fahamu ya kwamba "MADHABAHU" ni mahari pa mtu kukuta na Mungu anaye mwabudu.
Kuna madhabahu za iana nyingi na hizo zinaongozwa na shetani. Mimi nazungumzia madhabahu ya Mungu aliye hai. "MADHABAHU" ya Mungu ni ile imewekwa "WAKFU" kwa ajili ya Bwana.
Hesabu 7:10-11 "Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu,....Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Watasogeza matoleo Tao, kila Mkuu kwa siku yake, kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu "

NUHU ANA MSIKIA MUNGU KUPITIA
MADHABAHU ALIYOJENGA

Mwanzo 8:20-21 "Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa kila mnyama aliyesafi, na kila ndege aliyesafi, akavitoa sad aka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha..."
Lengo la Nuhu kujenga madhabahu ni kutaka akutane na Mungu na aseme naye, na hiyo ni baada ya kupona kwenye GHARIKA ya maji.
Je, Nini nini kilimvuta Mungu aseme na Nahu alipotoa sadaka? Ni ile. "HARUFU NZURI YA SADAKA"......... Kama uamini kasome biblia yako KAINI anakataliwa na HABILI anakubali, chanzo ni nini?...."SADAKA ZAO"

Nakupa mfano huo ili tunapoendelea mbele ujue kabisa MADHABAHU yenye uwepo wa Mungu si mahari pa kuchezea. Si kila madhabahu zilizoko makanisani zina Mungu. (UWEPO WA MUNGU) utasema Emma unataka kusema nini? Nataka kusema kaangilie wanaochukua "VYOMBO VYA MADHABAHUNI" (Watumishi/wahudumu/praise and worship team/) wanaweza kufanya uchafu na siku zote wakapanda kwenye madhabahu. Je Mungu haoni? Anaona, lakini ni kwa sababu hayupo kwenye hiyo madhabahu wanajingoza wao.
Lakini kama ni MADHABAHU ya Mungu aliye Hai, na uwepo wake uko mahari hapo, ambapo Daudi anasema.."HIVYO NITAKWENDA MADHABAHUNI KWA MUNGU" Uwe na uhakika utatoka na KICHAPO cha Mungu, usiulize ni kichapo gani wewe kajaribu uone.
WALIOPIGWA KWENYE MADHABA YA MUNGU ALIYE HAI.
Maandiko yanatwambia wana wawili wa Haruni NADABU na ABIHU walifia madhabahuni. Ni kwa sababu wapanda kwenye "MADHABAHU" ya Mungu aliye hai na kuanza kutoa huduma za kikuhani isivyo sahihi. Law. 10:1-12.
MAMBO WALIYOFANYA WANA WA HARUNI WAKAFIA MADHABUHINI.
(1). Hawakuwa watu SAHIHI wa kuweka uvumba, Na uvumba waliokuwa NATO haukuwa SAHIHI wa kuuweka mbele za Bwana. Sheria ya madhabahu inasema..."HAMTAFUKIZA UVUMBA JUU YAKE USIO SAHIHIH.." Kutoka 30:1-9. Na aliyeruhusiwa ni Haruni tu.
(2) Walitumia vyombo visivyo SAHIHI kwa matakwa yao wenyewe badala ya kuhani MKUU..Vyombo sahihi vilikuwa VIMETAKASWA kwa upako maalumu. Ndivyo ilivyoagiza sheria...."KISHA UTAYATWAA MAFUTA YA KUTIWA, NA KITIA MAFUTA HIYO MASIKANI, NA KILA KITU KILICHO NDANI YAKE, NA KUIWEKA IWE TAKATIFU, NA VYOMBO VYAKE VYOTE; NAYO ITAKUWA TAKATIFU" Kutoka 40:9
(3) Walifanya kwa wakati usio sahihi kwa sababu ilikuwa siku moja kwa mwaka.Kuhani mkuu alikuwa anaruhusiwa kupeleka uvumba PATAKATIFU PA PATAKATIFU. Kutoka 30:10.
(4) Walitumia MOTO usio SAHIHI moto wa kigeni.(Moto ambao haukuwa umekubaliwa) Kuhani Mkuu aliruhusiwa kuchoma uvumba kwa mkaa uliokuwa umetoka kwenye madhabahu. Lakini Nadabu na Abihu walileta moto wao na Mungu skaukataa.
(5) Walitenda kwa nia zao mbaya, hawakutafuta UTUKUFU WA MUNGU lakini wakatenda kwa kiburi chao na kujiinua wao wenyewe ili waonekane wao.
(6) Walitegemea NGUVU zao ambazo si sahihi , walikuwa wameongozwa na MVINYO (POMBE) Law 10:9 "Using we Dubai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo muingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife..." Ndiyo maana mtumishi wa MADHABAHU ya Mungu aliye hai hapaswi kunywa POMBE.(Wefeso 5:18)
Ndiyo maana tunasema usijaribu kuitumia MADHABAHU ya Mungu kwa mazoea, au kwa sababu wewe ni mtoto wa Mchungaji. Ndicho kilicho wakuta hawa watoto wa Haruni Kuhani wa Mungu.
Na hiki ndicho kiliwakuta wa Eli wakufa kwa sababu walikuwa wakichezea MADHABAHU na SADAKA zake, walifia vitani. (1 Samweli 4:1-22.)

Vivyo hivyo ANANIA na SAFIRA walifia kwenye MADHABHU yenye uwepo wa Mungu aliye hai. (Mdo 5:1-11.)
HIVYO USIJARIBU KUPANDA MADHABAHU YENYE UWEPO WA MUNGU UKIWA HAUKO SAHIHI.

MUNGU AWABARIKI

Comments