KWA YESU HAKUNA WOKOVU NUSU, YEYE ANAOKOA KABISA.

Na Godfrey Miyonjo

“Naye kwa sababu hii aweza KUWAOKOA KABISA wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee” WAEBRANIA 7:25.
BWANA YESU asifiwe.
Mpendwa wangu ninachotaka ujue ni kwamba YESU KRISTO anao uwezo wa KUMWOKOA KABISA mwanadamu awaye yote.
YESU KRISTO ninayemjua na kumwamini mimi hakuna jambo la kumshinda yeye.
Yeye alisulubiwa, akauawa, akazikwa, na siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu, na sasa yu hai, na uhai wake hauna mwisho hata milele.
Huyu YESU ninampenda kwasababu ukiwa ndani yake hakuna mwingine awezaye kukuhukumu adhabu, kama ilivyoandikwa:
“Ni nani atakayewahukumu adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anayetuombea” WARUMI 8:34.
Huyu YESU hana ahadi za uongo kama ilivyo miungu ya dunia hii.
Kwa maana miungu ya dunia hii hutoa ahadi za uongo, lakini YESU ahadi zake ni za kweli.
Miungu yaweza kuahidi vitu vilivyo juu ya uwezo wao lakini YESU anao uwezo na mamlaka yote.
YESU Mwokozi hakuwahi kutangaza wokovu nusu, na wala hatakuja tokea atangaze wokovu nusu, bali alichokitangaza yeye ni kwamba watu wote wamwendee Yeye naye atawapumzisha. MATHAYO 11:28.
Anapotutaka twende kwake hamaanishi kwamba atatupumzisha nusu, bali atatupumzisha kabisa.
Kutokana na maandiko mimi binafsi huwa Napata shida sana ninapoomwona mtu ameokoka nusu.
Ninapata shida ninapoomwona mtu anakiri udhaifu kuwa yeye hajakamilika.
Ninapata shida ninapomwona mtu anasema hatma ya wokovu wake ataijua siku ya mwisho.
Ninapata shida ninapomwona mtu anatafuta mwombezi mwingine nje ya YESU.
Ooooh! Ninatamani kila mmoja AOKOKE KABISA leo.
Wapendwa Ninasemaaaaaaaaaaaaaaa………………
Wewe ndugu uliye na nusu wokovu acha mawazo finyu, KWA YESU HAKUNA WOKOVU NUSU, YEYE ANAOKOA KABISA, amua kubabilika leo.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu).

Comments