Mfalme yeyote anaweza kumpa mtu yeyote nguvu na mamlaka ya kiutawala au kutawala chochote ambacho kipo katika himaya au milki ya Mfalme huyo,yaani kipo katika himaya au milki ya kiutawala ya huyo Mfalme.

Marais wengi wa dunia hii,wanateua watu wa kushika nyadhifa mbalimbali katika sehemu tofauti tofauti ili wawakilishe huko walipo hata kama wao hawapo.
Kwakuwa hao watu walioteuliwa na Rais,wamepewa mamlaka hivyo basi chochote watakachokisimamia inakuwa ni kama Rais anasimamia hicho kitu kwa wakati huo,kwasababu ule uwepo wa Rais unaenda sambamba na yule mtu aliyepewa hayo mamlaka na Rais,kwa wakati huo.
Kwasababu popote atakapoenda kwa kutumia jina la Rais basi na ile mamlaka ya kiutendaji wa jina hilo utaambatana nae.
Turudi sasa kwa Mfalme Yesu,ambaye ni zaidi ya marais na wafalme wote
wa duniani.Kwanini Yeye ni zaidi kwasababu anasema "Nimepewa mamlaka
YOTE mbinguni na duniani" ( Mathayo 28:18).
Kwasababu wale wote walioamua kuwa chini ya himaya yake Yesu Kristo mwenyewe yaani WALIOKOKA wanapewa nguvu na mamlaka ya kiutendaji na Yesu Kristo mwenyewe.
Hivyo wanapolitumia jina la Yesu kama Mfalme wa wafalme na ile mamlaka iliyokuwa ndani ya jina hilo inaambatana pamoja nao.
Ndio maana katika agano jipya tunaambiwa tutu
mie jina la Yesu( Mfalme wa wafalme).
Kwasababu Yesu alituahidi atafanya chochote kupitia jina lake pale tutakapomuomba ( Yohana 14:14).
Kwahiyo jina la Mfalme linabeba mamlaka kama aliyokuwa nayo Mfalme mwenyewe,na wote wanaolibeba au kulitumia jina lake wanatawala katika ile mamlaka aliyokuwa nayo Mfalme kwa kipindi hicho.
Tamani leo hii kutumia jina la Yesu likuletee matokeo mazuri katika maisha yako.
Mungu na akubariki katika Kristo Yesu.

Comments