MAADUI NI WENGI LAKINI HAKIKISHA UNAISHI KWA AMANI NA WATU WOTE.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Kama mteule wa BWANA YESU najua kuna baadhi ya changamoto unakutana nazo, jifunze ujumbe huu utakusaidia sana.
Maana kuwa mteule tu wa MUNGU maana yake ni kutangaza vita na shetani pamoja na mawakala wake wote. Lakini ta,nua jambo hili ya kwamba, Aliyeokoka Anatakiwa Aishi Kwa Amani Na Watu Wote(Warumi 12:18-21, Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya MUNGU; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena BWANA. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. ).
Ushinde ubaya kwa kutenda wema na tena lazima uwe na amani na wote.

Hilo la kuishi kwa amani na watu wote Liko Wazi Kabisa kwa kila mteule wa KRISTO  Ila Kuunganika Kwake Na YESU KRISTO Kutasababisha Watu Wengine Wamchukie tu, Na wakimchukia Sio Kwamba Wanamchukua Yeye Mkristo Bali Wanamchukia KRISTO Aliye Ndani Yake. Aliyeokoka Huku Familia Yao Au Ukoo wao Kuna Wachawi Na Waganga Wa Kienyeji Atanielewa Vizuri Zaidi.

-Kama mteule wa MUNGU Kuna Wakati Maadui Wa Mkristo Ni Maadui Wa MUNGU Lakini Sio Atakavyo Mwanadamu Bali MUNGU Maana Sio Kila Anayekukwaza Atakuwa Adui Wa MUNGU, Kutoka 23:22 (Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.)
-Lakini  Maadui  Wa MUNGU Wanatakiwe Wawe Maadui Wa Mkristo, hakikisha hauwi upande wa maadui za MUNGU maana ''  Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.- Zaburi 37:20''
-Kama mtoto wa MUNGU uliyezaliwa mara ya pili kwa ROHO MTAKATIFU lazima dunia ikuchukie maana wewe sio wa dunia hii. BWANA YESU analithibitisha jambo hilo la kuchukiwa kwa kusema '' Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka -Mathayo 10 :22''
-Watu wengi wanakatishwa tamaa na kuona Wokovu ni mgumu kwa sababu tu ya kutaka kuwapendezesha ndugu, jiulize wewe ulikuwa mlevi na kila siku ulikuwa unashinda bar, baada ya muda BWANA YESU amekuokoa na sasa uko kwenye kweli ya MUNGU, kwa sasa unapita katika bar hiyo hiyo ukiwa umeshika Biblia na kuwaambia walevi wenzako wa zamani mwende kanisani. Nakuhakikisha yule muuzaji atakuchukia sana maana unataka kumuondolea wateja wake, kumbuka pombe ni dhambi na wewe lengo lako ni kutaka waliokuwa rafiki zako wasiende jehanamu lakini unakutana na chuki hata matusi kwa sababu watu wa dunia hii wanakuchukia, wao ni maadui zako kwa sababu hawamhitaji YESU wako maana ndiye aliyekubadilisha. Ndugu maadui kama hao hawaepukiki lakini Biblia inasema tusiwachukie. hawakuchukii wewe bali wanamchukia KRISTO aliyeko ndani yako na kwa hilo hao pia ni maadui wa MUNGU.
 Binafsi ni mara nyingi sana nimetukanwa na hata kutishiwa na watu ambao naamini hawanichukii mimi bali wanamchukia KRISTO aliye ndani yangu, Hawataki injili iokoayo na meseji nyingi za matukano wametuma. Ukikaa vibaya imani yako inayumba na hakika unaweza kujikuta uko mwilini badala ya rohoni. ni mbaya na BWANA YESU anaendelea kusema
'' Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka -Mathayo 10 :22''
-Hata Hivyo Mkristo Anatakiwa Awapende Maadui Zake Na Kuwatendea Mema Wanaomchukia. Mathayo 5:44 '' lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,''
-Kuna wateule hadi wameitwa  wachawi kwa sababu tu mchawi halisi alikuja kumroga mteule akakutana na moto wa MUNGU na kuumia hivyo kuanza kuzusha kwamba Mkristo yule ni mchawi, kumbe amejaribu na kushindwa.
- Kuna wateule hadi wameitwa wajinga kwa sababu tu ya kukataa mila na desturi zinazomtukuza shetani, Ndugu yangu wewe sio wa dunia hii, ungekuwa wa dunia hii dunia ingekupenda lakini sasa dunia inakuchukia maana wewe sio wake.
Luka 6:27-28 '' Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.   ''). 
 Mteule wa MUNGU lazima awe na maadui
-Kuna Maadui Wanadamu.
-Kuna Adui shetani.
- Na Kila Mamlaka  na nguvu za Giza. 

YESU Aliwashinda Maadui Wote Hawa Kwa Njia Ya Kufa Na Kufufuka Kwake, Na Siku Ya Mwisho Atawaangamiza Milele 
 -Wewe Mteule; Hao Waokudharau Leo Waambie Wakupige Picha Kabisa Maana Utakavyokuwa Kesho Sio Kama Ulivyo Leo. Picha Hizo Zitakuwa Ushuhuda Wakati Ukishuhudia Matendo Makuu Ya MUNGU Kwako. 
-Ng'ang'ania Wokovu Kama Pesa, 
-Usiache Kuomba Na Pia Enenda Kwa ROHO. 
-Mshike KRISTO Utaishi, 
Kataa Dhambi Na Ikimbie Dhambi. 
Baraka Yako Ni Yako Tu, Na Hakika Itakuja Na Kufika Kwako. Dumisha Utakatifu, Utoaji Na Maombi Maana Hakuna Njia Mbadala Ya Baraka.
-Leo wateule Tunadharaulika na kuteswa sana lakini siku ile tutang'aa kama jua katika ufalme wa BWANA wetu.
Ufunuo 3:10-11 ''  Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. ''

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments