MAMLAKA YA ROHONI

Na Mchungaji Adriano Makazi, Ufufuo na uzima morogoro.

Utangulizi:  Somo letu leo linaitwa Mamlaka ya Rohoni”. Mamlaka huweza kumfanya mtu afanikiwe au  asifanikiwe. Zipo  mamlaka za rohoni upande wa Mungu na zipo nyingine za rohoni upande wa shetani. Kuna enzi au  mamlaka zinazowashikilia watu kiasi kwamba wanapotaka kwenda au kupiga hatua,  wanakuwa wamenaswa na kushikiliwa wasiondoke kiasi kwamba hawawezi kamwe kujikwamua.
Imeandikwa WARUMI 13:1-7…[Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 6 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.]…
Tena imeandikwa YOHANA 19:8-11…[Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa. 9. Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. 10 Basi Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha? 11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.]…. Pilato alitaka kujiridhisha kwa kumuuliza Yesu maswali kadhaa kadhaa ili aweze kutoa hukumu. Yesu aliamua kumpa majibu rahisi, kwa kumwambia Pilato kuwa mamlaka aliyo nayo Pilato imetoka kwa Baba yake aliye mbinguni. Kwa hiyo aliye kwenye mamlaka anaweza kumfunga mtu au kumfungua, na anao uwezo wa  kumuachia mtu huru au kumsulubisha. Kwa mujibu wa Yesu, shetani ndiye aliyemtia mikononi mwa Pilato, kwa kuwa ndiye aliyemuingia Yuda Iskariote. Kama Yesu alimwambia Pilato mamlaka aliyo nayo imetoka  juu (mbingunni) ujue kuwa zipo mamlaka ambazo zinatoka chini (kuzimu).
MITHALI 8:15…[Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki.]… Ndiyo maana wana wa Israeli walipomlilia Mungu ili awape mfalme sawa na mataifa mengine, Mungu alimwambia SAMWELI, hawajakukataa  wewe bali wamenikataa mimi (Mungu).
1 SAMWELI  10:1- …[1 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake. 2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?]…. Sauli kabla ya kuwa mfalme alimiminiwa mafuta na nabii wa Bwana (Samweli) ili aweze kuwaongozana kuwatawala watu wa Mungu. Kumiminiwa mafuta kwa kipindi cha Agano la Kale ni sawa  na kujazwa Roho Mtakatifu) katika Agano Jipya).
Sauli alipewa maelekezo ya kipi kitakachotokea baada ya kumiminiwa yale mafuta:
1 SAMWELI 10:3-9…[Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wanambuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; 4 nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. 5 Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri; 6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. 7 Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. 8 Nawe utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya. 9 Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote zikatukia siku ile ile.]…. Ipo mamlaka ya rohoni   ambayo mtu hupokea na baada ya hapo angeuzwa nakuwa kitu cha tofauti kuliko hapo awali. Ndiyo maana hata Petro hakuwa ana ujasiri wa kuongea mbele za watu, lakini baada ya kujazwa Roho Mtakatifu, aliwaeza kusimama kwa ujasiri na kuwahubiria maelfu ya watu juu ya Yesu Kristo.
LUKA 20:20….[Wakamviziavizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali.]…Biblia inawazungumzia watu waviziao. Yamkini hata wewe wapo wapelelezi wamekuja kwako wakijifianya watu wa haki (wapendwa, walokole, wakristo n.k) kwa namna ya kutaka kukunasa, na wewe hujui.
Wakati fulani Herode aliwahi kumchinja Yakobo na jambo kama hilo likawafurahisha sana Wayahudi, na kipindi hiki kanisa lilikuwa limelala, hawaombi.  Hata hivyo majira yale yale, Herode alitaka pia kumchinja Petro, hapo ndipo kanisa lilipoingia katika maombi, na malaika wa Bwana akaja kumfungua Petro, na na vile vikosi vinne vya maaskari wanne wanne waliokuw wakimlinda hawakuweza kumzuia  Petro.  Hata wewe, yale ambayo kwako yamekuwa magumu, kifungo kisicho na mlango kitakavyokuachia, na hatimaye uone kama  vile ni maono.
MWANZO 1:3…[Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.]… Kila anachosema mtu yeyote kinakuwa na unakiona baadae. Hii haijalishi  itapita muda gani,kwa kuwa hii ni sheria katika ulimwengu wa roho. Pengine umesema vingi na kwamba  hujaona matokeo yake, lakini ukumbuke kuwa ipo siku yakuviona vile  ulivyowahi kuvisema.
MWANZO 1:31….[Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.]… Hitimisho la yale ambayo Mungu alivisema, ni pale ambapo Mungu aliona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema. Kabla Mungu hajafanya huwa anasema sema kwanza. Vivyo hivyo,  chochote asemacho mtu kinakuwa kama alivyosema.
MITHALI 18:20-21...[Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake;  Atashiba mazao ya midomo yake. 21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;  Na wao waupendao watakula matunda yake. ]…. Kumbe uweza wa uzima na mauti vimo kwenye kinywa chako mwenyewe. Shetani huitumia mbinu  hii ya ulimi/kinywa cha mtu ili kumnasa, hasa pale amabppo ameshindwa kukukamata kwenye mambo mengine.
LUKA 20:1…[Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula;]…. Lengo la hawa watu  kuja kwa ghafla kwa Yesu, lilikuwa kujua ni kitu gani Yesu anafundisha,ili  wamnase kwa maneno ya kinywa chake. Imeandikwa ISAYA 42:22….[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo,wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]… Kumbe hata maneno anayotamka mtu yaweza kumfanya akafukuzwa kazi,  kuachika katika ndoa n.k. Wapo watu ambao kutokana na maneno waliyowahi kuyatamka, walijikuta wamenaswa kwa maneno ya vinywa vyao.

1 WAFALME 22:7-8….[Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hayupo hapa nabii wa Bwana tena, ili tumwulize yeye? 8 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza Bwana kwa yeye, yaani Mikaya mwana wa Imla; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema, ila mabaya. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.]….  Unaweza kumchukia mtu ambaye ndiye  mwenye  muujiza wako. Mtu yeyote ambaye akionywa huchukia,ujue huyo mtu hayupo vizuri.
1 WAFALME 22:9-13 ….[Ndipo mfalme wa Israeli akamwita akida, akamwambia, mlete hima Mikaya mwana wa Imla. 10 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wakikaa kila mtu katika kiti chake cha enzi, wamevaa mavazi yao, katika sakafu langoni pa Samaria; na manabii wote wakafanya unabii mbele yao. 11 Na Zedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, Bwana asema hivi, Kwa hizo utawasukuma Washami, hata waharibike. 12 Na manabii wote wakasema hivyo kwa unabii, wakisema, Kwea RamothGileadi, ukafanikiwe; kwa kuwa Bwana atautia mkononi mwa mfalme. 13 Na yule mjumbe, aliyekwenda kumwita Mikaya, akamwambia, akasema, Angalia sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja husema mema kwa mfalme; neno lako na liwe, nakusihi, kama neno la mmojawapo wao, ukaseme mema.]….. Wapo manabii wenye mbwembwe kama Zedekia mwana wa Kenaana, hata kwa kuvaa pembe za chuma, ili kufuata mkumbo.
1 WAFALME 22:14-16…..[Mikaya akasema, Kama Bwana aishivyo, neno lile Bwana aniambialo, ndilo nitakalolinena. 15 Na alipokuja kwa mfalme, mfalme alimwambia, Je! Mikaya, tuende RamothGileadi kupiga vita, au tunyamaze? Akamwambia, Kwea, ufanikiwe; kwa kuwa Bwana atautia mkononi mwa mfalme. 16 Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana?]….Maana yake yapo majira ya kkupigana vita na majira ya kutopigana vita. Daudi kabla ya kwenda vitani alikuwa anamuuliza Bwana kwanza. Ukitaka kufanya biashara, muulize Bwana kwanza. 
1 WAFALME 22:17-24…[Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. Bwana akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani. 18 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema, ila mabaya? 19 Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto. 20 Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. 23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako. 24 Ndipo akakaribia Zedekia, mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Roho ya Bwana alitokaje kwangu ili aseme na wewe?]…. Alichokifanya Zedekia, mwana wa Kenaana ni sawa na yale  yanayofanyika kwa baadhi ya watumishi wa Mungu kwa kuwasema watumishi wengine  kwenye madhabahu zao.
1 WAFALME 22:25-28…[Mikaya akamwambia, Angalia, utaona siku ile utakapoingia katika chumba cha ndani ili ujifiche. 26 Mfalme wa Israeli akasema, Mchukueni Mikaya, mkamrudishe kwa Amoni mkuu wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme; 27 mkaseme, Mfalme asema hivi, Mtieni mtu huyu gerezani, mkamlishe kwa chakula cha shida, na maji ya shida, hata nitakaporudi kwa amani. 28 Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, Bwana hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.]…. Ahabu aliitumia mamlaka yake vibaya, kwa kuwaachia huru wasiostahili na kuwafunga wasiostahili kufungwa. Ndiyo maana hata wewe hupati unachotaka kupata kutoka kwa Bwana, ni  kwa sababu ipo mamlaka rohoni yenye kuwafanya watu wapate, na wale wasiostahilikupata wapate. Mikaya anagandamizwa kwa  kutenda haki. Hupaswi kuridhika na hali uliyo nayo.
Hata kama baba na babu yako hawakuwahi kumiliki hata baiskeli,  lakini yale yalitokea kwa sababu ya vifungo  walivyovopitia. Wewe unapaswa kujitoa humo kifungoni na kumimliki,kutiisha na kutawala sawa sawa na mapenzi ya Bwana kwa Jina la Yesu. Shetani hana chochote alichowahi kukifanya au kuumba, bali hata yeye aliumbwa. Mwanadamu ndiye aliyepewa vitu vyote avimiliki hapa duniani,na shetania akaja kwa ujanjaunjanja akamwibia mwanadamu ile mamlaka. Je, utaweza je kumnyang’anya shetani vile alivyokuibia? Ni  kwa kupigana. Leo tunawafuata mawakala wa shetani (wachawi na waganga wa kienyeji) huko huko waliko, na kuwapiga mbele ya familia zao kwa Jina la Yesu. 
UKIRI
Bwana Yesu naomba leo iwe siku  ya ufumbuzi wa shida yangu. Kwa dama yamwanakondoo, ninaamuru kila mamlaka katika taifa, na ukoo wangu zinzonishikilia ili niwe maskini, nasema achia ufahamu wangu,  achia akili yangu kwa Jina la Yesu. naharibu mamlaka zote za giza zinazofanya kazi kwenye maisha yangu, kwa damu ya mwanakondoo.
 
LUKA 20:20….[Wakamviziavizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali.]…. Waviziaji hawaji moja kwa moja kukukabili. Mikaya hakuwa amekosea kwa maneno yake, na Ahabu mfalme alimtia gerezani nakupewa chakula cha shida. Ina maana hata wewe, yamkini ipo shida inayokukabili kutokana na mwenye mamlaka ambaye aliamua kufanya hayo yatokee. Yamkini wapo watu wanaofuatilia maisha yako,ili wakunase kw amaneno yako. Ndiyo maana Biblia inasema, maneno yako yawe ndiyo ndiiyo  na siyo siyo. Usiwe mtu wa kusitasita. Shetani   na mawakala zake (wachawai  na wahanaga wa kienyeji) hawachoki kumfuatilia mtu.  Endapo leo hii  wamekukosa,bado wataendelea kukufuatilia hadi wakunase.
Samsoni ni mfano mwingine wa watu waliokuwa wakiviziwa viziwa sana katika  Biblia. Ndugu  zake walipomfunga kwa kamba  na kumkabidhi kwa Wafilisti ili kujiokoa, Samsoni alijitoa kwa kuzikakata kamba na kuwapigakwa taya la punda zaidi ya watu 2,000 na kuwashinda wote. Ukipigana na kushinda rohoni unatumia pia akili za mwilini.
WAAMUZI 16:1-5…[Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua. 3 Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni. 4 Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila. 5 Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi,   na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.]….. Hapa ni kuwa, Wafilisti walijua ili kuweza kumpata Samsoni, njia rahisi ni ya kujua siri na asili ya nguvu zake.
WAAMUZI 16:15-19…[Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu,  wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. 16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. 17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe;  maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. 19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.]….Delila alifanya kazi ya kumtega Samsoni kwa maneno ya kinywa chake. Kuanzia mara ya kwanza hadi ya tatu,  Delila alimwambia Samsoni asimdanganye kama kweli  anampenda, kwani kama anampenda asingemficha siri ya nguvu zake. Delila alimlaza Samsoni magotini,  na kumnyoa nywele zote  hasa baada yakujua siri ya nguvu za Samsoni. Wapo watu  waliolazwa magotini mwa Delila hata leo.  Wachawi wamekunyoa nywele zako. Ni wakati wa kujua kanuni ya kuzifanya nywele ziote tena. Leo hii Samsoni anasaga ngano ya Wafilisti. Adui zako wakeshakunasa kwa maneno ya kinywa chako wanakutoboa macho na kukufanya usage ngano zao. Kiu yako ya kumtumikia Bwana inakuwa imetoweka. Hata hivyo, bado  lipo tumaini, kwa sababu nywele za Samsoni zilianza kuota tena.  Wale waliokutesa ni wakati  wa kujiliipizia kisasi kwa Jina la Yesu.
LUKA 4:5-6…[Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.]… Yesu alikuwa anaongea na shetani kabla hajaenda msalabani.  Yesu aliyeenda msalabani ni tofauti na wakati ambao alikuwa bado hajaenda msalabani.
UFUNUO 1:17…[Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,]….  Maana yake, ile mamlaka ya kuwafungulia watu waliokuwa magerezani ipo mikononi mwa Yesu. MATHAYO 28:18…[Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.]…. Yesu anayo ‘mamlaka yote’ duniani hapahapa na mbinguni. Hata kama ipo shida kubwa sana maishani mwako, mpelekee Yesu kwa sababu mamlaka ya kuiondoa ipo mikononi  mwa Yesu baada ya kufufuka.
UKIRI
Bwana Yesu, biashara yangu iliyofungwa leo ifunguliwekatika Jina la  Yesu. nipe ufahamu Bwana
 

Comments