MAONO YA SIKU ZA MWISHO NA RACHEL MUSHALA

USIKUBALI KUACHA KUSOMA USHUHUDA HUU MPAKA MWISHO.

Rachael Mushala
Disemba 2011, Bwana aliturudisha Kwake mimi na ndugu zangu. Ingawa baba yetu ni mchungaji, sisi wote tulikuwa tumerudi nyuma na kumuacha Bwana. Tulijifanya Wakristo mbele ya wazazi wetu na kanisa, lakini tuliishi maisha ya dhambi shuleni na wakati walipokuwa mbali na nasi. Tulidanganya na kutenda tuliyopenda. Lakini Mungu alifanya muujiza. Dada zangu wawili, kaka na mimi tukatubu na kumgeukia Mungu tena. Tulipojitoa tena kwa Mungu, tuliamua kumtafuta kwa maombi mazito. Tulitaka tuwe na uzoefu wa nguvu zake. Tulihisi kwamba kama tutamtafuta kwa bidii, atatujibu na kusema na sisi pia. Tulitaka sana ubatizo wa Roho Mtakatifu.





Siku moja tulipokuwa tukiomba, mdogo wangu, Lois, aliyekuwa na miaka 10 wakati huo, alisema anaona malaika! Uwepo wa Roho Mtakatifu ulijaza chumba na mdogo wangu mwingine Zipporah akaanza kunena kwa lugha! Ilikuwa ajabu lakini mimi nilihisi nimeachwa kwa sababu ingawa tulikuwa tukiomba, kaka yangu na mimi hatukubatizwa na Roho Mtakatifu usiku ule. Ilikuwa kama Mungu yuko kimya kwetu. Nilimlilia Mungu, nikimuomba asinipite. Kisha akampa ujumbe dada yangu Zipporah akisema, “Mwambie Inonge (jina langu jingine), Nasikia maombi yake. Mwambie azidi kuomba na asikate tamaa.”
Kubatizwa na Roho Mtakatifu
Baadaye tuliamua kuendelea na maombi ya siku tano ya kufunga na kumtafuta Mungu. Katika kipindi hicho, tulisoma Biblia, tuliimba sifa na kuabudu, na kuomba pamoja, sisi wote wanne. Nilisoma mistari yote niliyoweza kuipata inayozungumzia Mungu anavyojibu tukiomba. Nilisoma mistari yote inayozungumzia kuhusu ubatizo wa Roho Mtakatifu. Nilimuomba Mungu kwa ajili ya Roho Mtakatifu. Moyo wangu ulikuwa wakati wote ukimlilia kwa ajili hiyo. Lakini alikuwa kimya. Sikumpata hadi siku ya tano ya saumu yetu ndipo ilitokea. Kama saa 9 hivi alasiri, tulishakata tamaa, na kudhani Mungu amekataa kutujibu, ingawa awali tulipanga kufungua ifikapo saa 10 jioni ya siku hiyo. Tulimaliza kuomba pamoja, lakini baadaye nikajisikia kuendelea na maombi, hivyo nikaenda chumba kingine kuendelea na maombi. Nilipoomba na kumsihi Mungu anijaze sifa kwa ajili yake, nikaanza kunena kwa lugha! Sikuamini! Alikuwa amejibu. Niliendelea kumsifu kwa lugha muda mrefu na tukafungua dakika kadhaa baada ya saa 10 jioni.
Kutengwa na Ulimwengu
Baadaye usiku huo, nikaingia kuomba peke yangu. Nilikuwa naomba kwa lugha wakati Bwana alipoanza kusema nami. Alisema tunatakiwa kuwa mbali na utumwa wa aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mazoea mabaya ya TV, kwa sababu anataka awe wa kwanza katika maisha yetu. Kisha akasema wakati wowote tunapomuita kwa dhati , anasikia. Nikaenda kuwapa ndugu zangu ujumbe huo (wazazi wangu walikuwa wameenda nje ya mji wakati huo). Kisha tukaanza kuomba pamoja na Bwana akaanza kutupa jumbe nyingine zaidi. Alianza kusema na mimi na dada yangu Zipporah. Akasema, “Naja upesi, na nitakuja kama mwizi usiku, hivyo nitamjua ambaye kweli ni Wangu. Watu hawajali tena mtu akiwaambia kwamba ninakuja, kwa sababu nimechukua muda mrefu. Kuja kwangu hakutachelewa tena. Ninakuja upesi kuliko mnavyodhani, lakini swali ni je mtakuwa tayari? Kwa sababu ninakuja tu kwa ajili ya watu watakatifu, na kama unaishi maisha matakatifu nitakuchukua. Ninakuja tu kwa ajili ya wale wanaoishi maisha matakatifu. Wakristo wengi hawatakuwa tayari nitakapokuja, na watabaki.”

Akasema, “Kwa sasa mlango uko wazi lakini muda si mrefu utafungwa. Ingia kabla mlango haujafungwa. Nakungojea (mwanadamu) nikiwa nimefungua mikono yangu ya upendo.”

Akasema, “Nilitoa uhai wangu kwa ajili yenu, wanadamu kwasababu ya upendo Wangu kwenu. Humjui mbingu ni tukufu kiasi gani. Akili zenu za kibinadamu ni ndogo sana kulielewa hili. Lakini niliacha mbingu tukufu ili nitembee kwenye dunia hii chafu ya dhambi ili niwaokoe, niwafie. Hamjui niliteseka kiasi gani kwa ajili yenu. Yalikuwa mateso makali kuliko mnavyoona kwenye TV – mabaya kuliko wanavyoonyesha kwenye filamu yoyote. Hivyo ndivyo nilivyowapenda. Niliacha kila kitu kwa ajili yenu. Mnanipenda kiasi hicho pia? Mko tayari kutoa sadaka kila kitu kwa ajili yangu? Kwa vile hivyo ndivyo upendo Wangu ulivyo mkuu kwenu. Niliacha kila kitu kwa ajili yenu. Hamjui maumivu kiasi gani mnasababisha kwangu mnapoenda mbali nami. Kama mngejua, hamngefanya hivyo.”
Nilitambua maumivu aliyokuwa nayo moyoni mwake aliposema hivi. Niliweza kuhisi maumivu ya Yesu.

Bwana alituambia kuna mambo tunatakiwa kuacha kwa ajili Yake. Alituambia tunatakiwa kuuacha ulimwengu na kuishi kwa ajili ya utukufu Wake. Alisema, “Lazima mjitenge, kwa sababu ninyi ni nuru ya ulimwengu. Nuru inawezaje kuitwa nuru, kama inafanana na giza? Lazima muwe tofauti ili muwe nuru ya ulimwengu.”

Uasi na Manabii wa Uongo

Bwana Yesu alisema, “Uasi umeenea duniani. Manabii wengi wa uongo wameenea ulimwenguni wakifundisha mafundisho ya kuzimu na kupeleka roho nyingi kuzimu. Muwe waangalifu na msifuate miujiza. Sikuwaonya katika Neno Langu kwamba manabii hawa wa uongo watakuja? Na sasa wako hapa wakihubiri tu kuhusu utajiri na kamwe hawaihukumu dhambi. Wahubiri wanachozungumzia sasa ni utajiri na fedha, lakini fedha ina maana gani kama nafsi yako inaungua kuzimu? Sikusema muuze vyote mlivyo navyo na kuwapa masikini fedha na kisha mnifuate? Fedha ni shina la uovu wote. Msivutiwe nayo. Imewashawishi wahubiri wengi. Wanachojali tu ni kujaza mifuko yao na kujaza makanisa yao, lakini kamwe hawahubiri toba. Najua kwamba mkiwa bado duniani mtahitaji fedha nami nitawapa kiasi mnachohitaji. Hazina yenu iliyobaki itakuwa salama mbinguni. Utajiri wote mnaoutamani utatunzwa mbinguni ambako nondo hawawezi kuharibu. Dunia hii itaharibiwa kwa moto, na hakuna kitakachobaki.”

Alisema, “Moyo wangu unauma ninapoona roho zinapelekwa kuzimu na manabii wa uongo. Wako wengi; wachungaji wachache sana wanahubiri Neno Langu. Wachache sana wanahubiri toba. Haijalishi kama wana wafuasi wengi au wanatenda miujiza. Hata shetani anaweza kutenda miujiza. Msifuate miujiza. Ndio maana nilisema katika Neno Langu kwamba wengi watakuja kwangu siku ya mwisho na kusema, ‘Tulifanya miujiza katika Jina Lako,’ lakini nitajibu, ‘Siwajui’”

Mungu Anasikia Maombi Yako

Yesu pia alituambia kamwe tusiogope kuomba kwa sababu hakuna jambo kubwa kwa Mungu. Alituambia tuwe wajasiri kwamba tunapoomba Bwana anasikia. Wakati mwingine tunapoomba, shetani atakuja na aina zote za uongo akisema, “Mungu hakusikii. Mungu hasikilizi maombi yako.” Lakini msimsikilize. Wakati mwingine Mungu anaweza kuwa kimya, lakini anasikia mnapoomba.

Alituambia, “Mnapoomba, wakati fulani jibu linaweza kuja maramoja, lakini wakati mwingine inaweza kuchukua muda kwa sababu Mungu anataka muwe na subira na kumtumaini. Wakati wote jibu litakuja kwa sababu ni ahadi Yangu kwamba yeyote anayeomba hupokea.”

Hatari ya Ibada ya Sanamu

Bwana alituambia hatari ya ibada ya sanamu.

Mdogo wangu alikuwa anasoma shule ya Kikatoliki. Ni moja ya shule bora sana katika nchi yangu lakini walilazimishwa kuabudu sanamu. Wote walitakiwa kushiriki misa na kusujudia sanamu. Yesu alituambia kwamba kaka yangu anapaswa kuondoka shule hiyo na kutubu kwa kuabudu sanamu. Kama unaabudu sanamu kwa namna yoyote, tafadhali tubu. Kama hutafanya hivyo, utaenda kuzimu. Usipende au kutoa ibada yako kwa kitu chochote zaidi ya Mungu. Hiyo ni sanamu. Bwana anataka awe wa kwanza katika maisha yako.

Pia alituambia kwamba mpinga Kristo yuko karibu na atadanganya wengi. Yesu alisema mpinga Kristo atafanya mambo mengi ya kufuru lakini Bwana atamseta. Alisema, “Mpinga Kristo tayari yuko hapa na watu wengi tayari wanamfuata. Hawajui ni mpinga Kristo na mamilioni wanamfuata bila kujua. Atainuka mara, lakini na Mimi pia naja upesi.”

Hubirini Waliopotea

Kisha Bwana akasema ni wajibu wa kila Mkristo kuwahubiri waliopotea. Alisema wengi wamepotea na wanakwenda kwenye laana ya milele kuzimu na ni wajibu wetu kuwaonya na kuwaacha wenyewe wafanye uamuzi wanataka kwenda wapi.

Bwana Yesu Kristo alisema tusimhukumu yeyote na tusiseme, Hata kama tutawahubiri Injili hawawezi kamwe kutubu. Alisema, “Mnajuaje hawawezi kutubu? Sio kazi yenu kuhukumu.”



Yesu alituambia, “Lazima muwaonye watu watubu na msiogope kumuonya yeyote kwa kuona kwamba atawachukia. Wengi watawachukia, hata wengi katika familia zenu watawachukia, lakini lazima muwaonye. Msiogope kupoteza upendo wa mtu yeyote, kwa sababu upendo Wangu utakuwa badala ya upendo wote ambao wangewapa. Upendo wangu ni safi kuliko dhahabu.”

“Kuzimu ni mahali pabaya sana. Kama kweli unampenda mtu utapenda aumie sasa kwa maonyo yako na kuepuka kuzimu. Usimhukumu yeyote. Mwamuzi (hakimu) ni mimi peke Yangu. Lazima umuonye kila mtu ili afanye maamuzi yake mwenyewe. Waambie ukweli. Waonye, wanaoamini watakuja kwangu na wasioamini watahukumiwa, wakati watakapojuta kuzimu milele.”

Waonye Wanadamu kuhusu Kuzimu

Kisha Bwana alituambia kwamba ni Yeye alimwonyesha Angelica Zambrano, mbinguni na kuzimu na kwamba ushuhuda wake ni kweli. Alisema, “Watu wengi wanasema hakuna kuzimu kwa sababu Bwana ni Mungu wa rehema. Ni kweli kwamba Mungu ni wa rehema, lakini anaadhibu wanaogeukia mbali Naye. Wanawezaje kuzungumzia hukumu Zangu, wakati hata hawanijui? Hawajawahi kamwe kujua nguvu Zangu? Kuzimu kweli ipo na unapaswa kuwaonya watu. Waache wafanye uamuzi wao wenyewe.”

“Nimepeleka watu wengi mbinguni na kuzimu na kuwarudisha ili watoe ushuhuda, lakini kwa nini watu hawaamini? Kwa nini mnatilia mashaka shuhuda zangu? Kuzimu panatisha na sitamani kwamba yeyote aende huko.”

Bwana aliposema hivi, nikahisi maumivu Yake, nikahisi maumivu ya moyo Wake kwa ajili ya kudanganywa kwa dunia, huruma Yake kwa watu Wake wanaodanganywa na manabii wa uongo ambao wanazungumzia utajiri tu.

Mmoja wa rafiki zangu alifariki miezi michache iliyopita na Bwana akaniambia yuko kuzimu. Aliishi maisha ya dhambi na sikujali kumshirikisha Habari Njema. Iliniumiza sana kusikia hilo, nikamlilia Yesu anisamehe kwa kutomuonya katika maisha yake ya dhambi. Bwana alisema, “Usiogope kumuonya yeyote.”

Kama una wapendwa wako wanaoishi katika dhambi, nakuambia ni bora uwaambie ukweli hata kama watakuchukia kwa ajili hiyo. Utakuwa umewapa fursa wafanye uamuzi wao wenyewe. Fanya hivyo kwa upendo na huruma ili wamgeukie Mungu.

Vyombo vilivyo Tayari na Vinavyotii Vinahitajika

Bwana alituambia hajali kanisa ni kubwa au dogo kwa sababu anachoheshimu ni Neno Lake, Anajali tu kuhusu Neno Lake. Alisema, “Naweza kumtumia yeyote, hata jiwe. Ninachotaka ni moyo ulio tayari.”

Alituambia, “Niliahidi katika Neno Langu kwamba wote wanaoniamini watafanya mambo makubwa kuliko niliyofanya. Neno Langu halibadiliki. Natafuta vyombo vya kutumia. Ninachohitaji tu ni moyo ulio tayari na nitautumia.”

Pia alitutahadharisha na kiburi. “Ninapoanza kumtumia yeyote, mtu huyo kamwe asifikiri ni wa pekee sana. Watu wote ni sawa Kwangu na ninatumia chombo chochote kilicho tayari. Kamwe usijivune nisije nikakuseta.”

Bwana akatuambia shetani hana nguvu mbele Yake, ni kama mdudu tu. Ndio maana hatupaswi kumuogopa. Nguvu pekee aliyo nayo ni ile tu aliyowahi kupewa. Ameruhusiwa kuwajaribu ili Bwana ajue nani ni wa Kwake hasa.

Kisha Bwana akanionyesha upanga na akasema tutamshinda adui kwa kutumia upanga huo.

Ufunuo wa Kuzimu

Kwa wakati ule, hizi ni jumbe alizotupa kwa ajili ya ulimwengu, lakini baadaye Septemba 2012 tukiwa kwenye maombi, Bwana alijidhihirisha Mwenyewe mbele yetu tena. Tulikuwa na maombi nyumbani na wapendwa kadhaa wa kanisani na tulimlilia Mungu siku nzima. Tuliomba hadi usiku wa manane. Dada yangu Zipporah na mimi, tulikuwa tumepiga magoti karibu tukiomba kwa mioyo yetu yote ambapo ghafla mwanga mkubwa sana ulishuka kutoka mbinguni. Wengi wa watu waliokuwepo chumbani waliuona. Mara mwanga huu ukashuka na kufika pale dada yangu na mimi tulipokuwa tumepiga magoti. Ilikuwa kama kifuniko cha kuzimu kimefunguka!

Ghafla, tukasikia sauti za mayowe, mabilioni na mabilioni ya sauti zikipiga yowe kwa uchungu! Kila aliyekuwepo chumbani aliweza kusikia sauti. Tuliogopa kwa sababu tulijua zilikuwa sauti za kuzimu. Sijui tulifahamuje hilo, lakini katika ulimwengu wa roho, unajikuta tu unaelewa mambo ambayo hukuyajua…. Unashangaa tu unayajua.

Tulianza kumwomba Mungu, tukiomba rehema. Nilipofunua kinywa nilianza kunena kwa lugha. Kisha Bwana akaanza kusema na mimi na dada yangu, akitupa jumbe za kumpa kila mtu pale chumbani, kwa kanisa Lake na ulimwengu.

Wakati huu, mimi na dada yangu ndio tu tuliweza kusikia mayowe na maombolezo. Kulikuwa na mabilioni na mabilioni…..wasiohesabika. Walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa. Wengine walisikika wakilia kama wanaonyongwa. Wengine walikuwa wanapiga kelele, “Moto!Moto!”

Bwana akasema, “Wengi wa hawa watu walioko kuzimu walikuwa Wakristo walipokuwa duniani. Waliimba, waliabudu, waliomba, lakini wakaishia kuzimu kwa sababu hawakufanya toba ya kweli. Walienda kanisani lakini bado waliishi maisha ya dhambi wakiwa nyumbani. Wengi wataingia mahali hapa. Ombeni rehema kwa ajili ya ulimwengu.”

Tukaanza kulilia rehema, kuombea ulimwengu, tukiomba kwa mioyo yetu yote. Kisha Yesu akatuambia jinsi shetani alivyoweka mitego mingi ili awanase watu waende kuzimu. Alisema, “Kuzimu haitosheki. Shetani anataka kunasa watu wengi awezavyo waende kuzimu.”

Uchafu wa Kimapepo Ulioenea Duniani

Yesu alituambia kuna vitu vingi vinavyotumiwa duniani ambavyo vinatengenezwa na ufalme wa shetani kwa kusudi la kuwafanya watu wamilikiwe na kutawaliwa na mapepo. Alituambia kuna vitu vingi ikiwa ni pamoja na vyakula, vinywaji, nguo, (shetani amejipenyeza kila mahali. Ndiyo maana Wakristo wanatakiwa sasa kuamka katika maombi) vyenye mapepo yaliyopewa kazi ya kumiliki watu na kuwashawishi kutenda dhambi. Ndiyo maana ni muhimu kuombea na kukabidhi mikononi mwa Mungu chochote tunachonunua na kuharibu nguvu za kishetani zilizokuja nacho.

Alituambia kwamba televisheni ni moja ya chambo kikuu cha shetani cha kuwanasa watu waende kuzimu. Bwana alisema, “Vipindi vinavyoonyeshwa kwenye TV havikusudii kuwaburudisha watu bali kuwapeleka kuzimu. Wengi wako kuzimu kwa sababu ya TV. Filamu nyingi zimeandaliwa na shetani na kuigizwa na mawakala wake ili tu kuwanasa watu waende kuzimu. Moyo wangu unavunjika kuona jinsi wanadamu wanavyozipenda. Msiangalie TV ya kidunia. Itawapeleka kuzimu.” Alisema, “Ni chambo cha shetani kuwafanya mtende dhambi, kuharibu nafsi zenu. Mnapaswa kusulibisha mwili. Msitii tamaa za mwili. Mtiini Roho Mtakatifu.”

Bwana alituonyesha mapepo yanayofanana na waigizaji wa katuni; mengine yalifanana na katuni za Kikristo! Hili lilitushtua lakini Bwana akatuambia sio vipindi vyote vya “Kikristo” ni vya Kikristo kweli. Vingi si vya kweli na utambulisho wa “Kikristo” ni ili kuwanasa Wakristo waviangalie wakati vimekusudiwa kutangaza dhambi na kupeleka watu kuzimu.

Bwana alituonyesha filamu nyingi, vitabu na hata katuni za watoto ambazo zimeandaliwa na shetani na kuletwa duniani na mawakala wake. Majina ya katuni za kimapepo na madoli (wanasesere) ambayo alitufunulia ni Mudpit, Barbie®, Scooby Doo®, Ben 10®, Avatar, Pixel pinkie®, na the Walt Disney® versions of Cinderella, Beauty and the Beast, na the Little Mermaid. Bwana akasema katuni hizi zote zina mapepo yaliyopewa kazi ya kuwatawala watoto. Yesu akaniambia, “Unaona shetani alivyo katili? Anataka kuwanasa hata watoto waende kuzimu.” Nikaona pia pepo lililofanana na muigizaji wa katuni ya Kikristo kuhusu Musa iliyotengenezwa na Nest Entertainment®. Pepo lilifanana na mtoto Musa kutoka katika filamu hiyo, na lilikuwa linacheka likisema limedanganya Wakristo! Pia niliona pepo lililofanana na Aang kutoka katuni ya Avatar! Tulikuwa na katuni hizi nyingi nyumbani na Yesu akatuambia tuzichome.

Yesu alisema, katuni zote nilizoorodhesha hapa zimetengenezwa na sura za mapepo (yaani, kuna mapepo yanayofanana nazo kabisa) lakini nataka kubainisha kwamba Yesu alinionyesha baadhi tu na sio zote. Zaidi ya katuni za kimapepo nilizoona, ambazo nimezitaja, Yesu hakunionyesha katuni zingine. Alizitaja tu akasema ni za kimapepo.

Ningependa kusema kwamba sikuona tu mapepo yanayofanana na katuni za Barbie®, lakini niliona pia madoli ya Barbie®. Kusema kweli, niliona madoli ya Barbie® katika maono mengi katika nyakati tofauti. Katika maono mojawapo niliona vitu kadhaa kwa ajili ya kuuzwa stendi ikiwa ni pamoja na madoli ya Barbie®. Moja ya hayo madoli likageuka na kunitazama na kuanza kusema kwa dhihaka kwamba mapepo yamewadanganya wanadamu. Baadaye likasinyaa na kufanana na doli la kawaida la plastiki!

Yesu alisema hata baadhi ya vitabu vya watoto vina mapepo maalum. Alitaja kitabu cha watoto kinachoitwa "Rattlesnake." Hatujawahi kukiona au kukisoma hiki kitabu Yesu alichokizungumzia, lakini alisema hiki kitabu cha watoto kinatoka kuzimu. Ndivyo ilivyo kwa baadhi ya vitabu vinavyoitwa vya Kikristo. Yesu alitufunulia kwamba hata magazeti ya "Watchtower and Awake” yanayotolewa na Mashahidi wa Yehova, ni ya kimapepo na hataki watoto wake wayasome. Bwana alifunua baadhi ya magazeti ya kidunia yanayopaswa kuepukwa pia. Baadhi yao ni magazeti ya "Drum”, “You” na “People”.

Yesu alituambia kwamba haya yote yana misheni ya kupeleka watu kuzimu, sio kuwaburudisha. Alisema, “Dunia imekuwa mahali pa giza na ndiyo maana nataka muongozwe na Roho katika kila jambo mnalofanya.” Alituambia, “Hivi vitabu, filamu, drama za mvutano wa kijamii na katuni havijakusudiwa kuwaburudisha watu bali kuwapeleka kuzimu. Ni chambo cha shetani. Msivutiwe navyo.”

Bwana alituambia shetani ameweka mapepo kwenye stika za watoto pia. Hizi ni katuni na stika zingine kama Hannah Montana na Barbie® stickers.

Alituambia muziki wa kidunia pia utawapeleka kuzimu na kwamba nao pia ni mtego wa shetani.

Ondoeni Vitu Bandia

Alituambia hataki wanawake Wakristo wawe bandia kwa namna yoyote. Alisema hataki watumie nywele bandia, mapambo ya vito (hereni, bangili nk.), kope bandia, kucha bandia, rangi za kucha, rangi ya mdomo (lipstick), wanja au vipodozi vya aina yeyote.

Anataka wabaki vile walivyoumbwa. Wajivunie jinsi alivyowaumba. Hicho ndicho kinachompendeza.

Aliposema hili, kulikuwa na hasira katika sauti Yake. Alisema, “Kwa nini mnajaribu kubadili nilichokiumba? Sitaki vitu hivyo kwa watoto Wangu. Kama mnataka vitu hivyo, kwa nini hamtengenezi watu wenu wenyewe ili mviweke vitu hivyo kwao. Msibadilishe nilichotengeneza!”

“Vitu hivi vyote bandia vinatoka kwa shetani. Sivitaki kwa watoto wangu.” Yesu havitaki. Viondoeni na kutubu. Vitawapeleka kuzimu.

Bwana alinionyesha kitu cha kushtua sana; niliona pepo katika namna ya mwanamke na lilikuwa limevaa vitu hivi vyote: kope bandia, rangi za mdomo, na nguo inayobana sana. Hapo ndipo nikatambua vitu hivi vinatoka wapi; kwa shetani mwenyewe. Alituambia vitu hivi vyote vimetoka kuzimu na shetani amevileta kuwadanganya watu.

Sitii chumvi katika ujumbe huu. Nasema kama Bwana alivyosema nami. Ni jukumu langu kuwaonya kuhusu hili kwa sababu wote tutasimama mbele za Mungu siku moja.

Nawaambia ukweli. Yesu hapendi vitu hivyo. Anapendezwa tukibaki vile alivyotuumba; hiki ndicho alichotuambia.

Staha na Utakatifu

Alituambia hataki wanawake Wakristo kuvaa suruali au mapambo. Bwana aliruhusu dada yangu kumsikia shetani akitoa maelekezo kwa mapepo. Alikuwa akisema, “Hakikisheni wanaandika 'SURUALI ZA WANAWAKE' (kwenye utambulisho [label]) ili wanawake wazivae na kuja kuzimu.”

Bwana pia alinionyesha pepo katika mfano wa mwanamke aliye uchi, amesimama juu ya ukuta mrefu. Ingawa lilikuwa uchi kabisa na juu ya ukuta mrefu, hili pepo liliendelea kujaribu kuuficha uchi wake kwa kufunika sehemusehemu kwa kutumia mikono yake na kuchuchumaa. Lakini halikuwa limevaa nguo yoyote! Yesu akaniambia, “Hili ni pepo la utupu linalotawala wanawake duniani na ndiyo maana wanatembea hadharani uchi na kufunika sehemu tu za miili yao.” Yesu akaniambia tena kitu kingine. Akasema, “Hili pepo la utupu limeingia kwenye makanisa mengi.”

Yesu aliniambia shetani anajua kwamba wanawake Wakristo wengi hawavai tena mapambo ya vito kama bangili, hivyo amebadilisha aina ya mapambo ili kuwanasa. Sijui kama hizi saa ziko kila mahali lakini katika nchi yangu kuna saa-bangili. Zimetengenezwa kabisa kama bangili, lakini zina kitu kidogo katikati ambapo unaweza kuona muda. Lakini Yesu aliniambia ni hila tu ya shetani ili wanawake waseme, “Ni saa tu.” Pia niliona roho za nyoka kwenye hizi saa-bangili.

Alisema anataka utakatifu kamili na lazima tuitii Biblia yote. Bwana alisema, “Fuateni Neno Langu.”

Pia alisema, “Dunia imeingia katika kanisa Langu. Watu kanisani sasa wanavaa kama watu wa duniani. Wameingiza muziki wa shetani kanisani; rock, hip hop. Umewahi kusikia malaika wakiimba kwa kutamka (rapping)? Unaweza ku-rap na kusema unamwimbia Mungu?” Bwana aliposema hili, kulikuwa na hasira kwenye sauti Yake.

Bwana aliruhusu pia mimi na dada yangu kuwasikia malaika mbinguni wakitoa sifa na heshima kwa Bwana wetu. Walikuwa wanaimba, “Hosana, Hosana kwa Mungu aliye juu,” na ilipendeza sana. Sijawahi kusikia namna hiyo duniani.

Wiki chache zilizopita Yesu aliniambia, “Waambie watu wangu, ‘Muda ni mfupi sana na saa inafika mwisho. Usipende kubaki nitakaporudi kukusanya bibi arusi Wangu. Mkono Wangu wa kuzuia utainuliwa na mateso yasiyoelezeka yataijia dunia. Jiandae kwa vile kuja Kwangu ni kwa utukufu!’”

Lazima Mlinzi Awaonye

Mara ya kwanza kusikia Mungu akisema nami ilikuwa 2010. Nilitaka sana kumsikia Mungu na nilikuwa nikimuomba aseme nami. Nilisikia sauti ya Bwana na alisema tu “Ezekieli 33:6-7”. Nilipoisoma ilisema, “Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo. Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.

Bwana aliponipa andiko hili, sikuelewa lina maana gani kwangu, lakini Bwana akasema ananiandaa na dada yangu tuwe walinzi. Alisema, “Niliwapa mstari huo kwa sababu najua kazi ninayotaka kuwatumia kuifanya. Popote nitakapowaambia muende, mtakwenda, popote nitakapowaambia msiende, hamtakwenda. Huu ni mwisho wa maisha yenu ya kibinafsi na kuanzia sasa mtaishi kwa ajili Yangu. Nitawatumia kuwatoa wengi gizani na kuwaingiza nuruni. Lazima mseme ukweli na msimuogope yeyote. Kama nawaambia mumuonye mtu fulani na hamumuonyi kwa sababu mnaogopa, damu yao itamwagwa juu yenu. Nitawapa ujasiri na hamtashindwa.”

“Wengi watainuka kinyume chenu, hata wengi katika familia zenu watawainukia. Wengi watawapinga na hata kutumia maandiko kuwapinga. Watawapa majina. Wengine watasema mna mapepo lakini msivunjike moyo. Msikate tamaa kwa sababu niko pamoja nanyi. Sitawaacha wala sitawatupa kamwe. Lazima mseme ukweli kama ulivyo bila kumuogopa yeyote kwa sababu niko pamoja nanyi. Wengi watawahukumu na kudhani wanamfanyia Mungu huduma, lakini lazima muwe shujaa na hodari na kusema wazi.

“Kutakuwa na mateso mengi, lakini msikate tamaa kwa sababu thawabu yenu ni kubwa na thawabu ni kubwa kwa yeyote anayefanya kazi ya Mungu.”

Miezi kadhaa baadaye wakati mimi na dada yangu tulipokuwa tukiomba, Bwana alituonyesha maono ya watu kwenye tamasha la muziki. Lilikuwa tamasha la muziki wa dunia na wengi niliowaona hapo walikuwa vijana. Walikuwa wote wakifurahia lakini nilipotazama niliona kwamba kwa juu kulikuwa na mkono mkubwa uliowafunika. Bwana akanifunulia kwamba huu ulikuwa mkono wa shetani. Ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kuwafunika wote lakini walionekana kwamba hawana habari. Mkono ulitoa mafuta fulani uliyoyaacha kwa wote walioko pale. Na Bwana akaniambia hiki ndicho kinatokea kwenye matamasha ya muziki. Mkono wa shetani unafunika kila mtu katika matamasha haya na kuacha kitu fulani juu yao.

Pia alitupa maonyo kwa ajili ya Wakristo. “Hata tu kusengenya kunaweza kumpeleka mtu kuzimu. Usiwaseme ndugu zako katika Bwana. Usimseme mtu yeyote. Jali mambo yako mwenyewe. Kama unaona mtu amekosea, sema naye kuhusu kosa hilo na kumuombea. ”Bwana akasema, “Msifanye makosa ambayo wengi walioko kuzimu waliyafanya ya kudharau vyombo ambavyo Mungu anavitumia kwa sababu ya umri au sababu nyingine yoyote. Mungu anaweza kutumia kitu chochote na yeyote anayetaka kumtumia.”

Wiki mbili zilizopita, nilikuwa nyumbani nikiomba. Mara nikafunga macho yangu ili kuanza kuomba. Bwana akanionyesha shimo refu sana lenye giza. Lilikuwa refu sana, refu kuliko kina chochote ambacho nimewahi kuona pamoja na giza nene. Nilipofungua macho yangu sikuweza kuona kitu lakini nilipofunga macho niliweza kuliona tena. Chini kwenye shimo hilo niliona moto wa majimaji kama unaoonekana kwenye volkano. Ulikuwa moto mwekundu. Nilijua ni kuzimu. Maono yakakoma.

Sikia Maonyo na Ingia Kupitia Mlango Mwembamba

Siku iliyofuata usiku nilikuwa kitandani nikiongea na Yesu ambapo nikiwa katikati ya kuamka na kuota ndoto hivi nilimuona Yesu na akaniambia anataka kunivuta Kwake. Nikajikuta niko Kuzimu, peke yangu (Sikuona nikiwa na Yesu Kuzimu). Palikuwa mahali penye giza sana ingawa kulikuwa na miali mingi na joto kali. Niliweza kuhisi kuungua moto kutoka katika miali na kusikia sauti ambayo inasikika ukiwa karibu na moto mkubwa. Kisha nikaona mtu; alikuwa uchi kabisa na alionekana akiteseka sana.

Mara nikasikia mayowe ya uchungu, “Saidia! Saidia! Nilikuwa Muislamu duniani na sasa najuta sana. Nisaidie!” Ilikuwa inaumiza sana kumuona huyu mtu na kusikia kilio chake kiasi kwamba nilitamani kutoka mahali hapo. Nilijaribu kuamka lakini sikuweza. Baada ya muda nikaweza kuamka na kujikuta nimerudi kitandani kwangu. Kwa muda niliendelea kuhisi joto kwenye ngozi yangu, na kisha likatoweka.

Baadaye nikapata maono mengine peke yangu, sio kwa kipindi kimoja tulipata haya mafunuo niliyoyashuhudia. Nilikuwa chumbani kwangu usiku mmoja wakati Bwana aliponionyesha sehemu ya kuzimu ya wale wanaopiga punyeto (wanaojichua). Hii sehemu ilikuwa inasikitisha. Niliona mwanamke kwenye kiti. Alifungwa kwa minyororo mikubwa kwenye kiti alichokuwa amekalia na hakuweza kusogea kabisa! Huyu mwanamke alikuwa amechomwa kiasi cha kutotambulika. Kilichokuwa kimebaki katika mwili wake ni kama majivu. Alikuwa kijivu kabisa, ameungua kama mkaa, na alionekana akiteseka sana. Kisha nikawezeshwa kujua kwamba alikuwa pale kwa sababu ya kujichua katika maisha yake duniani. Naamini Mungu alinionyesha hilo kwa sababu anataka kuwafikia waliotawaliwa na dhambi hii.

Sikiliza Neno la Mungu. Usidharau chombo chochote anachokitumia Mungu kusema na wewe. Badala yake, tubu na kumrudia Mungu. Nakusihi sasa utubu na kuja kwa Yesu. Usiweke imani yako kwa mtu. Weka imani yako kwa Mungu. Tubu dhambi zako na jitahidi kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa vile wengi watajaribu kuingia wasiweze.











Yesu anatuonyesha jinsi ya kuingia lango hilo kupitia maonyo haya anayotupa katika hizi nyakati za mwisho. “Jitahidi kuishi maisha matakatifu, kwa vile bila utakatifu hakuna mtu atamwona Bwana.” Yesu Mwenyewe alituambia maneno haya; alisema anarudi tu kwa ajili ya watu watakatifu.

Biblia inasema usifanye moyo wako kuwa mgumu unaposikia sauti Yake; mtafute Mungu maadamu anapatikana kwa sababu kesho utakuwa umechelewa. Hakuna kati yetu anayejua lini tutakufa, na mara tutakapoiacha hii dunia itakuwa haiwezekani kutoa maisha yako kwa Kristo na kupita toka mautini kwenda uzimani.

Ufu 21:8. “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”



1 Kor 6:9-11. “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.”

Mungu akubariki.
Rachael Mushala

Comments