MWAKA WA MABADILIKO KATIKA MAISHA YA KIROHO NA KIMWILI.


BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze.
Ni miezi ya mwanzoni kabisa ya mwaka, ombi langu Ufanye Mwaka Huu Kuwa Mwaka Wa Maombi Kwako. MUNGU Anautaka Mwaka Wako Kwa Matumizi Yake Na shetani Naye Anauhitaji Mwaka Wako Huu Autumie Kwa Matumizi Yake. Ni Heri Mwaka Wako Huu Ukamkabidhi MUNGU Ili Autumie. Siri Kuu Ya Ushindi Wako Mwaka Huu Iko Waefeso 6:18 '' kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; ''. 

Amka Ndugu Maana Wachawi Wanautafuta Mwako Wako Ili Wautumie Wao Kwa Kukuletea Magonjwa, Ajali Na Majanga. Ndugu Yangu BWANA YESU Anataka Umkabidhi Mwaka Wako Huu Ili Akushindie.Kumbuka kwamba BWANA YESU huwa haji kutusaidia bali huja kutushindia tu.
''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Mathayo 11:28-30. 

 Adui Huja Pindi Mtu Anapoacha Kuheshimu Sheria Ya MUNGU. Haki Hutoa Mamlaka Lakini Dhambi Huleta Kupotea Kwa Mamlaka. Kumbuka Adamu Alifukuzwa Na MUNGU Baada Ya Dhambi. Ndugu Hakikisha Unaishi Kwa Unyoofu.
''Na amani ya MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISTO YESU. Wafilipi 4:7. 

 Usiache Kulitaja Jina La BWANA YESU Maana Umo Ushindi Mkubwa Ndani Ya Jina Hilo.''Umngoje BWANA, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA. Zaburi 27:14.''
 -Mngoje BWANA Katika Maombi. 
-Usiache Kuomba. Omba Na Utangaze Utawala Wa YESU KRISTO Katika Maisha Yako Na Maisha Ya Watoto Wako, Familia Yako, Marafiki Zako Na Ndugu Zako. Usiishi Kwa Hisia Bali Mtegemee MUNGU. 
-Weka Mpango Mzuri Wa Maisha Yako Na Imalisha Mambo Uliyopewa Na MUNGU. 

BWANA YESU Anakupenda Sana Mpe Nafasi Maishani Mwako Ili Akushindie.  ''Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. Kumb 31:8. ''
 Jina La YESU Ndio Password Ya Baraka Zote Unazozihitaji. Unaweza Ukaumwa, Baada Ya Kuumwa Ukatembea Hospital Zote Lakini Hujapona, Unaweza Ukatumia Dawa Ambazo Wengine Wamezitumia Hospitalini Wakapona, Lakini Wewe Dawa Hizo Hizo Zimeshindwa Kukuponya. YESU anasema   ''ROHO wa BWANA yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Na kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa. -Luka 4:18-19  
''


Ndugu Yangu Uzima Wako Unapatikana Kwa YESU KRISTO, Ukihitaji Kupona Kimbilia Maombezi Maana Uko Ushindi Wa Kila Jambo Ndani Ya Jina La YESU KRISTO.
''Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Mithali 3:5-6.
 Neema Ya BWANA YESU Imetufunika, Neema Ni Mwavuli Ili Sisi Wateule Tusipigwe Na Jua Na Pia Neema Ni Mwavuli Ili Mvua Ya shetani Isitunyeshee. 1 Samweli 2:8 '' Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.   ''

 Nampenda Sana BWANA YESU Kwa Upendo Huu. BWANA Hutuimalisha, Ukimtegemea Yeye Utashinda Na Kushinda. Ndugu Yangu, Hakikisha Unavaa Haki Ya MUNGU Pia iishi Haki Ya MUNGU.
''Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na MUNGU huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 1 Yohana 5:4.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments