NA UJE BWANA YESU

BWANA YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibuni tujifunze nikianza na maswali matano(5) kwako.

-Je Unatamani YESU Arudi? 
-Je Uko Tayari Kwa Kuja Kwa YESU Mara Ya Pili? 
-Je YESU Akirudi Ataikuta Imani Sahihi Duniani? 
-Je Wanaomkataa YESU Leo Wataenda Wapi? 
-Je Wanaomsema Vibaya Na Kuikataa Injili Yake, Je Siku Hiyo Watafanyaje? 
 BWANA YESU alipokuwa akiondoka duniani kuelekea mbinguni aliwaambiwa wanafunzi wake wakaihubiri injili yake kwa kila mwanadamu, yule mwanadamu atakayeamini ataokoka (Mathayo 28:19-20 , Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. )
Baada ya BWANA YESU kuondoka kwenda mbinguni huku mitume wakishuhudia kwa macho yao malaika walitoa tahadhari hii kwetu ''   .... Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu YESU aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.   -Matendo 1:10-11''.
-Kama  BWANA alivyoenda ndivyo atakavyorudi. 
Kurudi kwa YESU kutaambatana na matokeo ya maisha aliyoishi  kila mwanadamu aliyepata kuishi duniani.

Haya yafuatayo ni moja katika yale atakayoyafanya BWANA YESU.
      1.   BWANA YESU Yuaja Na Ujira Mkononi Mwake Ili Kumpimia Kila Mwanadamu Kipimo Chake Stahiki Sawasawa Na Matendo Yake, BWANA YESU anasema ''Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.-
Ufunuo 22:12-13).
-BWANA yuaja kumlipa kila mwanadamu kama kazi yake ilivyo.
-Watumishi waliofanya kazi yao kwa ulegevu watalipa sawa sawa na kazi yao.
-Waliokuwa wakijiita na kuitwa watakatifu kumbe sio nao watalipwa sawa sawa na matendo yao.
-Wazinzi na waongo ambao hawakutubu walipokuwa hawajafariki nao watalipwa jehanamu.
-Kila mtu atalipwa sawa sawa na matendo yake aliyokua anayatenda.
-Waliokuwa maarufu duniani kama maraisi, wanamziki, wanasoka siku hiyo watakuwa wa kawaida tu kama walivyo omba omba leo na kila mtu atalipwa.
-Kila mtu atalipwa sawasawa na kazi yake, kazi yake ikiwa mbaya atalipwa jehanamu na ikiwa nzuri atalipwa uzima wa milele.
-Je unajua utalipwa nini? matendo yako ya leo ndio yanaweza kuamua utakacholipwa siku hiyo.

      2.  Hakika MUNGU Wetu Atakuja Na Kukusanya Kondoo Wake(Isaya 40:10-11,  Tazameni, BWANA MUNGU atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake. Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole. ).
-BWANA siku hiyo atakusanya kondoo wake kwa ajili ya uzima wa milele.
-Kondoo ni watu waliompokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wao(Yohana 1:12-13)
-Kondoo ni waabuduo halisi(Yohana 4:24)
-Kondoo ni waliowekwa huru na BWANA YESU(Yohana 8:36)
-Siku hiyo kutakuwa na makundi mawili tu ya wanadamu, kutakuwa na kondoo na mbuzi. Ni heri kuwa kondoo leo kwa kuokoka maana ni hatari sana kuwa mbuzi kwa kumkataa YESU. Biblia inasema Mathyo 25:31-34,41 ''   Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume(KONDOO), Njoni, mliobarikiwa na BABA yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto(MBUZI), Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;''

 -Ndugu Unajiandaa Kulipwa Nini? Maana kila mtu atalipwa sawa sawa na matendo yake (Zaburi 28:4,  Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe stahili zao.

-Kwa sasa MUNGU Anachunguza Moyo Wako Ili Akulipe Vizuri siku ile ikifika(Yeremia 17:10, Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. ). 

-Mteule Shika Ulichonacho Ili Asije Mtu Akakunyang'anya Taji Yako Ya Uzima Kwa Kukufanyisha Dhambi(Ufunuo 3:10-13, Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la MUNGU wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la MUNGU wangu, na jina la mji wa MUNGU wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa MUNGU wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. ). 

-Wema Wa MUNGU Unakuvuta Sasa Ili Utubu(Warumi 2:2-6, Nasi twajua ya kuwa hukumu ya MUNGU ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya MUNGU? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa MUNGU wakuvuta upate kutubu?  Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya MUNGU,  atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;

-BWANA Atakuja Na Atamlipa Kila Mtu Sawasawa Na Matendo Yake(Zaburi 62:12,   Na fadhili ziko kwako, Ee BWANA; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake. ). 

Asante BWANA YESU Kwa Neno Hili. NA UJE BWANA YESU, Ufunuo 22:20-21,   Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, BWANA YESU. Neema ya BWANA YESU na iwe pamoja nanyi nyote. Amina. 

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.


Comments