NIRA YA KRISTO NI MUHIMU SANA KWA KILA KIJANA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze ujumbe mzuri wa kuleta mabadiliko.
Leo nazungumzia vijana.


Vijana Ndilo Kundi Ambalo shetani Analitaka Sana Alitumie. Pia Vijana Ndio Wanaotakiwa Zaidi Kumtumikia MUNGU. Hakuna Wakati Mzuri Kumtumikia MUNGU Kama Wakati Wa Ujana. Biblia Inashauri Mwanadamu Aichukue Nira Wakati Wa Ujana Wake(Maombolezo 3:27,Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.  )
 Nira Inayozungumzwa Hapo Ni Nira Ya Kumpokea BWANA YESU, Yeye Anasema Katika Mathayo 11:28-30 '' Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. ''  
 -Nira Ya YESU  Ni Laini Na Hivyo Twende Kwake Sisi Wote Tusumbukao Na Wenye Kulemewa Na Mizigo Mbalimbali. Hakuna asiye na mzigo, awe ni kijana au ni mtu mzima lazima awe na mzigo. 
-Nira ya kwanza kwa kila mwanadamu ni kupungukiwa na utukufu wa MUNGU. Hata kama unajiona unatenda matendo mema lakini kama hujampokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wako, wewe bado hujaivaa nira ya BWANA. 
Baada ya nira hiyo pia zipo nira nyingine nyingi tu.
-Kuna Wengine Wana Mizigo Ya Uchungu Wa Kuachwa Na Wachumba Wao, Hayo Yote Hufanyika Mara Nyingi Wakati Wa Ujana. 
-Kuna Vijana Hawana Mwelekeo Wa Maisha Baada Ya Kufiwa Na Wazazi Wao, Hiyo Yote Ni Mizigo Na Inatakiwa Tuipeleke Kwa YESU.
 Kukosa Nira Ya KRISTO Kumewapeleka Pabaya Vijana Wengi. Kuna Vijana Hata Walijidhuru Kwa Sababu Ya Mambo Ambayo Wao Ndio Chanzo Maana Hawakufuata Ushauri Wa Biblia Kwamba Wanatakiwa Wawe Upande Wa MUNGU Wakati Wa Ujana.  Waebrania 13:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu.   ''
MUNGU atawahukumu wazinzi, hivyo kijana lazima aepuke dhambi hii mbaya ya uasherati.
Kijana lazima ajitenge na ngono wakati wa ujana wake na maisha yake yote. 
Habari Za Kwamba Nitaokoka Nikiwa Mzee Hazitakiwi Kutamkwa Na Kijana Mwenye Malengo Ya Kwenda Uzima Wa Milele.

Dunia na yaliyomo yamewaangamiza vijana wengi.

 -Wadada Badala Ya Kujipamba Kwa Utu wema Na Maombi Na Upole Wao Wanajipamba Kwa Nywele Bandia Na Kuongeza Makalio Ya Mchina. 
-Wakaka Badala Ya Kujipamba Kwa Utuwema Na Utakatifu Na Ucha MUNGU Wao Wanajipamba Kwa Tatoo Na Mitepesho. 

Ndugu zangu ukiipenda dunia huwezi kumpenda MUNGU, Dunia sio ya kuikimbilia maana  Dunia Iko Jumping Jumping, No Position.Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. - [Mithali 28:13]

Kila kijana anawaza jinsi atakavyoingia kwenye ndoa , ni wazo zuri kabisa lakini lazima kijana amtii MUNGU na akubali kuwajibika kwa MUNGU, Kuwajibika kwa MUNGU ni pamoja na kutii maonyo nyake.
-Asilimia 90% Ya Mawazo Ya Vijana Wengi Wanawaza Kuingia Kwenye Ndoa. Sijajua Asilimia 90% Ya Wanandoa Wengi Wanawaza Nini?
Walio wengi wa wanandoa wanaowaza kutoka katika ndoa ni kwa sababu ya misingi mibovu ya chanzo cha ndoa zao. Wakati wa ujana wao walikataa kuwasikiliza watumishi wa MUNGU na ushauri wao mzuri.
Lakini pia  Sehemu Kubwa Zaidi Ya Mafundisho Ya Ndoa Ni Vitisho Na Tahadhari ndio maana hilo nalo linasababisha Vijana Wengi Wanaogopa Kuoa/kuolewa Wakati Ndoa Ni Paradiso Ndogo.

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na BWANA’'.
-Kuoa au kuolewa ni mpango kamili wa MUNGU.
- Zipo sababu nyingi za kwa nini unahitaji mke au mume Moja unakuwa umejipatia kibali kwa BWANA, Unakuwa umepata msaidizi na mlinzi.
-Kibiblia mke /mme mwenye busara mtu hupata kutoka kwa BWANA, maana yake MUNGU ndiye anayehusika na kumpa mtu mke/mme. MUNGU pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa na fulani halafu ndiyo anayekupa huyo mtu. 
-Kijana sio kila binti mrembo anafaa kuwa mke wako.
-Binti sio kila kijana anafaa kuwa mmeo.

Kwa Maoni Yangu kwa watumishi  Tungetoa Vitisho Kwa Wachumba Ambao Walianzia Bar Uchumba Wao, Tutoe Vitisho Kwa Wachumba Wanaojiita Boyfriend Na Girlfriend Huku Wakizini Kabla Ya Ndoa Na Tungetoa Vitisho Kwa Vijana Waliookoka Wanaotaka Kuchumbia/kuchumbia Na Mtu Asiye Na Hofu Ya MUNGU, Pia Tuwakemee Wale Wanaotaka Kuolewa Na Mtu Ambaye Muda Wowote Anaweza Kuongeza Mke Wa Pili Maana Mila Na Desturi Yake Inamruhusu maana KRISTO sio sehemu ya maisha yake.

Vijana wacha MUNGU Tuwatie Moyo Na Kuwaambia Uzuri Wa Ndoa Maana Ndoa Takatifu Iko Mzuri Aisee.
Kijana hakikisha unamuomba MUNGU na yeye atakupa mtu aliye wako.
 Mwanzo 1:27-28 '' MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. MUNGU akawabarikia, MUNGU akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.


Comments