NJIA KUU NA NJIA

Na Geofrey Miyonjo.

“Na hapo patakuwa na NJIA KUU, na NJIA, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo”
BWANA YESU asifiwe,
Kila aliye hai chini ya jua na ayafahamu maneno haya.

Kila aliye na nia ya kumpendeza Mungu na aelewe hivi, kuwa kuna NJIA KUU NA NJIA.
Na mara baada ya kulijua hili, ingekuwa heri kama kila mmoja angechukua hatua, kwa kufanya hivi Mungu atafurahi sana, kwa maana imeandikwa “mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda” YOHANA 13:17.
Biblia inaposema kuwa patakuwa na NJIA KUU, na NJIA haizungumzii habari ya siku zijazo.
Bali biblia inazungumzia habari ya siku hizi tunazoishi.
Inazungumzia mwelekeo wa imani za watu, inazungumza vile watu walivyo hivi leo.
Maneno haya tafsiri yake ni hii, YESU KRISTO ndiye NJIA KUU, na SHETANI ndiye ile NJIA.
Yesu ndiyo hiyo njia ya utakatifu, na waionao hiyo njia wanaiendea na kujitenga na uovu, nao waelekea mbinguni.
Imeandikwa “NJIA KUU ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye aishikaye njia yake huihifadhi nafsi yake” MITHALI 16:17.
Mtu aliye NJIA KUU (kwa YESU) ndiye aliyeihifadhi nafsi yake, ndiye aliye na mwelekeo sahihi.
Na shetani ndiyo ile NJIA, nao waifuatao waelekea upotevuni/jehanam.
Inajulikana kuwa Mungu anatupenda sote, wala hapendi hata mmoja wetu apotee, kama ilivyoandikwa “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” YOHANA 3:16.
Mungu anataka kila mmoja wetu akae NJIA KUU, ili asiwe na mashaka na safari yake ya kuelekea mbinguni.
Nami kama mtumishi wa Mungu ninatamani kila mmoja akae NJIA KUU,
Ninayasema haya nikijua kuwa kila mmoja wetu pale alipo (kwenye dini) anajiona kuwa yupo katika njia, lakini mimi nataka tujue kuwa pana NJIA KUU, na NJIA.
Kila mmoja anapofanya ibada na ajiulize kuwa yupo NJIA KUU (Amemwamini YESU na kujitenga na uovu)?
Kama wewe bado haupo NJIA KUU (yaani una dini lakini hauna YESU/Haujaokoka),
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa…………………………………………………..
ondoke huko upotevuni, njoo NJIA KUU leo ili uwe na mwelekeo sahihi.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu).

Comments