NUKUU MUHIMU KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU (Sehemu ya 2)

Mwl. Christopher Mwakasege.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze na kutiwa moyo na kukua kiimani kupitia Nukuu hizi za watumishi mbalimbali kutoka kwenye mafundisho yao au mahojiano. Na utaniambia wewe binafsi umependa Nukuu namba ngapi kati ya hizi Nukuu 12.

1.   Maana kwake MUNGU yote yanawezekana, nazo njia zake huanza mahali njia zetu zinakoma- By WALTER TROBISCH.

2.   MUNGU anakuwa vile sisi tutakavyo awe, ukitaka aponye mafua ataponya, ukitaka afufue aliyekufa atamfufua hivyo usimweke MUNGU ndani ya box, yaani aweze kuponya mgonjwa eti ashindwe kufufua?- By Pastor JOSEPHAT GWAJIMA.

3.   Kiwango cha mavuno kinaamuliwa na kiwango cha mbegu upandacho, Mungu hakulazimishi mahali pa kupanda  ndio maana akakupa aina za udongo( aumuzi ), Wapi pa kupanda ni juu ya mpandaji-By MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

4.   Daktari anatibu, YESU KRISTO anaponya-By GASPER MADUMLA.

5. Kumpenda MUNGU ni kupenda sheria zake, kama unampenda MUNGU bila kushika  sheria  zake hakika wewe humpendi MUNGU- By PETER M MABULA.

6. Kuomba maana yake ni kumwita MUNGU-By Mchungaji FLORIAN KATUNZI.

7. Usioe au kuolewa kwa sababu ya kumsaidia mtu fulani au kumuonea huruma, Ndoa ni kitu cha thamani zaidi kuliko mahusiano ambayo yamejijenga katika huruma-By Mchungaji PETER MITIMINGI.

8.   Ni heri sana kumfundisha mtu ile kweli ya BWANA kisha BWANA Yeye atende muujiza na kumfungua mtu huyo katika vifungo vyake,kuliko kumtaka mtu apokee muujiza pasipo kufundishwa ile kweli,sababu muujiza pasipo kweli yaani muujiza pasipo kufundishwa neno la MUNGU,ni kazi bure-By GASPER MADUMLA.

9. MUNGU ni Baba yetu mzazi maana alituzaa kwa neno lake(Yakobo 1:18), Lakini kama MUNGU  sio Baba yako mzazi lazima kuna vitu hawezi kukushirikisha, au hata ukimuomba asikupe. Sio, kwa sababu hakupendi bali kwa sababu Sio Baba yako mzazi- By NICKSON MABENA..

10.   Hoja kubwa ya wayahudi kumkasirikia YESU ni juu ya Sabato, na hadi leo hii kuna ubishani mkubwa juu ya siku ya sabato. Sabato maana yake ni puumziko, siyo siku, uwe na siku ya kupumzika uiheshimu. MUNGU alifanya kazi siku sita ya saba akapumzika hapa haoneshi siku bali alifanya kazi siku sita MUNGU akaona kazi ni njema, akapumzika. wewe unapumzika vipi kama hujamaliza kazi? wanadamu wengi leo wanapumzika bila kumaliza kazi-By Mtume na Nabii JOSEPHAT MWINGIRA.

11.   Watu wote tuliokolewa, tuko katika ufalme wa MUNGU. BWANA YESU ndiye Mtawala wetu. Upande wa pili, kwa jinsi hiyohiyo, watu wote ambao hawajaokoka, wako katika ufalme wa Ibilisi. Shetani ndiye mtawala wao.katika ufalme wa Shetani, watu hawa ni watumwa wa Ibilisi, ni mali yake Ibilisi, ni watoto wa Ibilisi ( 1 YOHANA 3:8-10; YOHANA 8:34 ). Watu hawa walioko katika ufalme wa Shetani, pia ni wafungwa katika gereza la Shetani, na Shetani hataki kuwaachia. Ni mpaka apatikane mwenye nguvu zaidi, wa kuwafungua ( LUKA 4:18 ) Wafungwa hawa wanalindwa vikali na Shetani ili kuhakikisha hawatoki katika nyumba yake, na anawaita VITU VYAKE, na mateka wake ( LUKA 11:21-22 ).Siyo hilo tu. Akili zao zimetiwa giza, wamepofushwa fikra zao na kujazwa kila namna ya ujinga ili isiwazukie nuru ya Injili ya wokovu ( WAEFESO 4:17-19;2WAKORINTHO 4:3-4 ).


12.    Uislamu umeanza 610 B.K wakati huo dini zingine kama Uyahudi , Ukristo kwa kuzitaja kwa uchache zilikwisha kuwapo. Je hao walikuwa hawali nyama? Na kama walikuwa wanakula walikuwa wanachinjiwa na nani Waislamu wakiwa hawapo? Nani aliyekuja kutangaza baadaye kuwa ni Waislamu tu ? Je ni serikali?-By DANIEL MWANKEMWA.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu Yako Peter M Mabula.
Maisha ya ushindi Ministry.
Mabula1986@gmail.com.
0714252292

Comments