PELELEZA KWA UNDANI NAFSI YAKO ILIPO

Na Geofrey Mwanza.


(1 Samweli 13:1-7, Sauli alikuwa na umri wa miaka kadha wa kadha hapo alipoanza kutawala;naye akatawala miaka kadha wa kadha juu ya Israeli. Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake.  Yonathani akaipiga hiyo ngome ya Wafilisti, iliyokuwako huko Gibea, nao Wafilisti wakapata habari. Naye Sauli akapiga tarumbeta katika nchi yote, huku akisema, Na wasikie Waebrania.  Waisraeli wote wakasikia habari ya kwamba Sauli ameipiga hiyo ngome ya Wafilisti, na ya kwamba Waisraeli wamepata kuwa makuruhi kwa Wafilisti. Basi hao watu wakakusanyika pamoja kumfuata Sauli huko Gilgali. Nao Wafilisti wakakusanyana ili wapigane na Waisraeli, magari thelathini elfu, na wapanda farasi sita elfu, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni. Hata Waisraeli walipoona ya kuwa wa katika dhiki, (maana watu walifadhaishwa), ndipo hao watu wakajificha katika mapango, na katika vichaka, na katika miamba, na katika mashimo, na katika mabirika. Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani, wakaingia nchi ya Gadi na Gileadi; lakini Sauli alikuwa akaliko huko Gilgali, nao watu wote wakamfuata wakitetemeka. ) 
Baada ya vita kati ya wafilisti na waisraeli kuzuka,waisraeli wakajiona kuwa taabani maana walikuwa wanashambuliwa vikali.Walianza kujificha.Wengine wakajificha mapangoni,wengine mashimoni,wengine kwenye miamba,wengine kwenye makaburi na wengine kwenye visima.Wengine walivuka mto Yordani mpaka katika nchi ya Gadi na nchi ya Gileadi."Vita vingi vya kidunia vimeinukia ulimwenguni ndugu yangu,ni wapi umejificha? Ni kwa ulevi,uasherati,ufisadi?Je,unaposema umeweka moyo wako mahali pasipo na vita,hebu peleleza vizuri tu polepole husije ukawa umejificha makaburini kumbe shetani amekumaliza!.Watu wengi wamepotea kwa kuchanganyikiwa.

Watu wengi tu wako katika misururu ya kujificha vita vya kishetani bali hawana ukanguzi mwafaka wa kujua jinsi ya kuzipinga hila za shetani.Amua leo uokoke na uombe maombi haya Yehova MUNGU akufunulie siri zote za ufalme wa giza.Sema "BWANA YESU MIMI NI MWENYE DHAMBI,NAJA KWAKO UNISAMEHE DHAMBI NA MAKOSA,FUTA JINA LANGU KWA KITABU CHA HUKUMU NA ULIANDIKE KWA KITABU CHA UZIMA WA MILELE.NIMEOKOKA NAKIRI KWA KINYWA KRISTO YESU NI BWANA.NIFUNULIE KILA SIRI YA KISHETANI INAYOJIFICHA.KWA JINA LA YESU NAOMBA NA KUOKOKA,AMEN
-For assistance "THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES 
-By Geoffrey Mwanza. -0724 656 653.

Comments