BWANA YESU ASIFIWE NDUGU
ZANGU karibu leo tusifunze kidogo chimbuko la neno la MUNGU. MUNGU
aliejuu na akubaliki unapoendelea kujifunza pamoja nami.Roho wa BWANA
atusaidie, karibu.....
BIBLIA ni maktaba ya NENO LA MUNGU iliyosheeni ujumbe na mapenzi ya
MUNGU kwa wanadamu hiyo ni pumzi ya ni PUMZI ya MUNGU 2Timothio
3;16-17. Biblia ina vitabu sitini na sita vilivyoandikwa na waandishi
arobaini, kwa muda usiopungua miaka elfu moja mia sita. (1600). Karibu
Agano la Kale lote liliandikwa kwa lugha ya Kiebrania isipokuwa mafungu
machache kwenye kitabu cha Danieli,EZRA na yerimia yaliyoandikwa kwa
lugha ya Kiaramu Danieli 2:4 sehemu zilizoandikwa katika kiaramu ni
hizi: Ezra 4:8 – 6:18:7:12 – 26 Danaeli 2:4 – 7:28 Yeremia 10:11 . Agano
Jipya limeandikwa kwa lugha ya kiyunani na pengine Kigiriki kwa kuwa
ilikuwa lugha iliyojulikana kwa karibu na watu wote ingawa katika nchi
hiyo ya Israel kiaramu kilikuwa ni lugha ya nyumbani zamani za Bwana
Yesu kristo.
Waandishi baadhi yao walikuwa wafalme kama Daudi na Sulemani na wengine walikuwa waganga na wataalamu kama Isaya na Luka. Wengine walimu wa dini kama Ezra na Paulo wengine maafisa wakubwa wa Serikali kama Musa, Danieli na Nehemia, wengine wakulima na mafundi Amosi na Yohana , wengine wavuvi kama Petro , wengine watunga muziki kama Asafu na watoto wa Kora wengine manabii kama Ezekiel, Yoeli na kadharika. Wengine kati ya waandishi hawakujuana kabisa, waliishi katika nchi tofauti tofauti wengine palestina (baadhi ya manabii) wengine Babeli kama Danieli na Ezekieli na wengine wakisafiri katika Nchi za mbali Paulo na Mitume wengine na mmoja wapo aliandika akiwa kifungoni katika kisiwa cha Patmo.{Yohana} Kwa kweli Biblia iliandikwa kwa njia ya pekee kuliko vitabu vingine vyote.
Kutokana na kufifia kwa lugha ya kiebrania mpaka kufikia mwaka 200 K.K na lugha hii kusahaulika na wengi na kutotumiwa na wengi ndipo ilibidi Agano la kale litafsiriwe katika lugha za mataifa mengi kama vile Kiaramu, Kisuria, Kigiriki, Kiarabu, Kimisri n.k. SEPTUAGINTI YA KIGIRIKI Mwaka 300 – 200 K.K .
Wataalamu wa Biblia hufanya kazi ya kuchunguza na kuunganisha miaka
na nyakati ya wafalme wanchi mbalimbali KWA MFANO Luka 3:1 – 2 “Mwaka wa
kumi na tano wa kutawala kwake kaisari Teberio Pontio Pilato
alipoalipokuwa liwali wa Uyahudi na Herode Mfalme wa Galilaya na Filipo
ndugu yake Mfalme wa Itulea na nchi ya Trakoniti Lisania Mfalme wa
Abilene wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa.Neno la Mungu lilimjia
Yohana mwana wa Zakaria jangwani.” Hii ni kutokana kwamba kila nchi ina
hesabu yake yenyewe ya miaka. Theologia hawakubaliani katika mambo
yote kuhusu miaka, hivyo katika kutaja miaka tunatumia neno “Kama” kwa
sababu hakuna anaejua mwaka kamili ila hufanya makisio baada ya kufanya
utafiti kwa kina. Kalenda tunayotumia sasa iligunduliwa na mtaalamu
mmoja mtawa anaeitwa Dionysius Exiguus. Warumi walihesabu miaka tangu
kujengwa kwa Rumi. Miaka kabla ya kuzaliwa kwa Kikristo huhesabiwa kwa
kurudi nyuma toka kwa Yesu Kristo kurudi nyuma na inaitwa K.K / BC na
baada ya kuzaliwa kwa Yesu huhesabiwa toka kwa Yesu kwenda mbele na
inajulikana kama BK/AD Agano la kale lilitafsiriwa kama lugha ya
Kigiriki iliitwa Septuaginti. kwa sababu inasemekana ilitafsiriwa na
watu 70.
SABABU HIYA HAPA. MUNGU akitaka kuzungumza na watu
hatumia lugha wanayoijua wenyewe hatumii lugha ngeni hutumia lugha
inayofahamika kwa eneo hilo kwa waliojazwa na roho mtakatifu nathani
wananielewa ukisoma Petro ameandika:...... Wanadamu walinena yaliyotoka
kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2PET 1:20-21).hivyo walipata
ufunuo kwa lugha rahisi waliokuwa wanaifahamu.Kiebrania kilikuwa
kimeenea na kutambulika mahali pengi ndani ya Islael kipindi cha Agano
la kale pia katika kipindi cha Agano jipya lugha kama kiaramu kiyunani
na kigiliki ni lugha ambazo hata YESU ALIZOKUWA AKITUMIA na hata mitume
wake na alivyopaa agano jipya likaandikwa LUKA 1;1-3 kwa lugha
niliokunyesha hapo juu.
SIKILIZA ....MUNGU ameleta neno lake
duniani kwa ajili ya uthamani wako mwanadamu anakupenda zaidi
unayofikili anakuthamini zaidi ya unavyodhani harakati zote amefanya kwa
ajili yako amemtuma YESU ili akukomboe aingie na neno la uzima kwako
ili huishi maisha ya furaha yasiyo ya uzuni kamwe anakuomba kwa upole
ndani ya moyo wako tazama niko mlangoni nabisha odi mtu akifungua mlango
nitaingia kwake na kuka pamoja nae.chagua kuwa na YESU NA UMPINGE
SHETANI.KARIBU KATIKA MAISHA YA WOKOVU.ONGERA YAKO UNAEENDELEA KUDUMU
KATIKA IMANI.
UBARIKIWE ULIESOMA UJUMBE HUU MUNGU NA AKUHUDUMIE
SAWASAWA NA ITAJI LAKO
kwa msahada zaidi wa kiroho wasiliana nami
GODFREY MAKOKO
NO 0752508662 au
0782362588
email;g.makoko@yahoo.com au
makokogodfrey@gmail.com

Comments