SHUHUDA KUTOKA EFATHA MWENGE.

Mtume  na Nabii Josephat Mwingira, Efatha
USHUHUDA
Naitwa Vicent Sungura.
Mimi napenda kumshukuru Mungu kwa yale aliyonitendea, Baba alisema tukagombee nafasi mbalimbali kwenye maeneo tunayoishi nikagombea ujumbe wa serikali ya mtaa, mtaa wa mabibo, katika kura za maoni nilishinda kwa kishindo mpaka kusimama kuwa mjumbe. Pia napenda kumshukuru Mungu kuwa nilikwenda nyasa kwetu kutangaza nia ya kugombea udiwani nilipofika songea mjini nikapigiwa simu kwamba kuna kazi ya ICT Kigoma, baadaye nilipigiwa simu nikaambiwa kuna kazi nyingine Mwanza. Wakati naingia Efatha nilimuamini mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira nikaamua kushika maneno anayotufundisha nikaazimia mambo matatu, nilisema nitakuwa mwimbaji nimuimbie Mungu, imekuwa. Pia nilisema kwa namna yeyote nitasoma Mungu ni mwema nilipata mfadhili Naibu waziri wa miundo mbinu nimesoma mpaka chuo kikuu, nikasema nitafanya kazi nitakayoichagua yenye maslahi. Namshukuru Mungu leo hii nachagua kazi, naenda Mwanza nikiona maslahi siyo mazuri naenda Kigoma. Ukiwa ndani ya Efatha jitahidi kushika Neno la madhabahuni Mungu atalithibitisha Neno lake, Amen.

Vicent akishuhudia


 Naitwa Felista Benjamini, napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kujifungua bila upasaji, ilikua si rahisi lakini kwa neema yake Mungu wakati wakujifungua ulipofika niliambiwa njia haionekani japokuwa mtoto alikuwa kageuka kwa ajili ya kutoka haikuwezekana kwani njia ilikuwa haionekani. Ikabidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili, nilipofika daktari wa kunifanyia upasuaji hakuwepo, alikuwa kufanya upasuaji kwa mtu mwingine. Mimi sikuacha kuomba nikimsihi Mungu nikamwambia Mungu kama Mama Maria(Yesu) alijifungua kwa upasuaji, basi na mimi nitajifungua kwa upasuaji. Kama Maria(Yesu) alijifungua kwa kuongezewa njia basi na mimi nitaongezewa, baada ya kusema na Mungu, ilikuwa kama muujiza kwangu nilimwambia Mungu kwamba mtoto anatakiwa atokee sehemu aliyoingilia. Basi niliendelea kumsihi Mungu kwa hilo baadaye nilipofikia zamu yangu kuingizwa chumba cha upasuaji nilimwambia Mungu nakuomba unipe nguvu ya kusukuma kwani Roho wa Bwana yu juu yangu! basi nilijikuta Napata nguvu ya ajabu nikasukuma na mtoto akatoka walishangaa kuona vile, lakini najua kwa kuwa huu ni mwaka wangu wa Mtembeo wa Mungu basi Mungu hakuniacha peke yangu Amina.
FELISTA AKISHUHUDIA KANISANI

Comments