SIFA MBILI ZA WANA WA MUNGU


Na Alex Makuli.
Bwana YESU asifiwe.
Zipo sifa nyingi za wana wa MUNGU, lakini kwa leo tuangalie sifa hizi mbili za wana wa MUNGU.

1:UPENDO

Upendo ni sifa mojawapo mhimu kwa wana wa MUNGU.

Tunakuwa na upendo kwa sababu MUNGU ni pendo na alitupenda sisi kwanza(Yoh 3:16, Yoh 13:34-35).
Pia tunakuwa na upendo kwa sababu MUNGU ametuagiza tupendane sisi kwa sisi(Mt 22:38-39, 1Yoh 4:20-21, 1Yoh 2:9-11).
Hebu tuangalie hili andiko lifuatalo;-
1Yoh 2:9-11 YEYE ASEMAYE YUMO NURUNI NAYE ANAMCHUKIA NDUGU YAKE, YUMO GIZANI HATA SASA YEYE AMPENDAYE NDUGU YAKE AKAA KTK NURU.
Kumbe ukisema kwamba wewe ni wa nuruni lazima umpende ndugu yako, na kama ukimchukia ndugu yako wewe bado uko gizan.

Upendo ndio kila kitu(1Kor 13:1-8).

2:UTAKATIFU

Utakatifu ni sifa nyingine mojawapo ya wana wa MUNGU.
Mwana wa MUNGU lazima uish maisha ya kumpendeza MUNGU.
"EBR 12:14 TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE NA HUO UTAKATIFU AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO".

Ni hayo tu kwa leo, 
Barikiwa sana
By Alex Simion Makuli.

Comments