TENGENEZA MAPUNGUFU YA IMANI YAKO LEO.


Na Godfrey Miyonjo.
“Kwa hiyo kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo kama mtasikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu……………” EBRANIA 3:7-8.
BWANA YESU asifiwe sana.
Utukufu na heshima anastahili kupewa mwokozi wetu kwa kazi kubwa na ya thamani ya ukombozi aliyoifanya pale msalabani.
Ni YESU pekee ndiye njia ya kumkaribia Mungu, kama ilivyoandikwa “Kwa maana kwake yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja”. EFESO 2:18.
Ni ukweli usiopingika kuwa mtu asiye na YESU (mtu asiyemwamini YESU kama BWANA na Mwokozi wa maisha yake) hawezi kuwa karibu na Mungu.
Japo kuna misemo mingi na maarufu duniani isemayo kuwa “hakuna mwanye haki chini ya jua”, “utakatifu ni mbinguni”, “wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”, N.K, lakini uwepo wa misemo hii hakuwezi kuubadili ukweli kuwa Mungu ni mtakatifu, na wote wamwabuduo imewapasa wawe watakatifu. 1PETRO 1:15-16.
Pamoja kuwa tunazo imani, lakini jambo la msingi ni kwamba, tujiulize, imani zetu zininampendeza Mungu?.
Kama jibu ni hapana, basi huu ndiyo wakati pekee kwetu sisi kuamua KUTENGENEZA IMANI ZETU.
Tunapaswa kufanya hivi kwasababu:
Mungu hafurahii kuona wanadamu tukiendelea kuishi dhambini
Mungu anataka wanadamu wote tuishi kwa mwongozo wa neno lake (tulitii neno lake).
Mungu hafurahii kuona watu tukitetea maovu, mfano kutetea masanamu, ulevi, uzinzi, uchawi, wizi, N.K.
Ndiyo maana Mtume Paulo katika ule WARAKA WA KWANZA kwa kanisa la wathesalonike aliyanena haya: “Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwasababu yenu mbele za Mungu wetu; usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi, tupate kuwaona nyuso zenu, na KUYATENGENEZA MAPUNGUFU YA IMANI YENU?” 1THE 3:9-10.
Mtume Paulo aliliandikia kanisa la Wathesalonike, ambalo lilikuwa ni la wakristo kuwa yeye (Mtume Paulo) alikuwa anafurahi sana mbele za Mungu na kumshukuru Mungu usiku na mchana pale alipoonana na wathesalonike na kuona wanakubali KUYATENGENEZA (KUYAONDOA) MAPUNGUFU YA IMANI YAO.
Kama Mtume Paulo alivyosema na wathesalonike nami Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaa…………………………………………………………
Tubuni leo kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu).

.

Comments