UNABII WA MUNGU NI LAZIMA UENDANE NA NENO LAKE MUNGU.

Na  Mtumishi Geoffrey Mwanza.
(Kumbukumbu 13:1-3, Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;  wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. ).

Watu wengi wamezuka siku hizi wakiwapotosha wakristo kwa mafundisho ya uongo na yasioandamana na NENO la MUNGU--Mathayo 24:24"watatokea manabii/makristo wa uongo watakaofanya ishara kubwa na maajabu na kuwapotosha hata wateule"
-(Mathayo 7:15-Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajieni kama kondoo bali ni mbwa mwitu"

Nabii wa uongo hutumia nguvu za giza(Kumbu 13:1-4)Unabii wa ukweli uandamana na NENO la MUNGU-Ezekieli 12:25-28"Mimi Yehova nitatangaza yatakayotokea nayo yatatokea bila kukawia,nene nitakalolitamka nitalitimiza".

Umuhimu wa unabii umeelezwa kuwa ni kujenga watu,kuwatia moyo na kuwafariji(1Korintho 14:3-4)Hii ni kumaanisha unabii haistahili kutabiria mtu ukimwambia mchawi wako ni fulani au fulani jambo ambalo wenye kutolewa unabii hupenda kuambiwa.Pia katika kutoa unabii haistahili kuambia mtu kuwa mumewe ana mke/mume mwingine nje maana kufanya hivi nabii atakuwa amekiuka amri za kinabii 1korintho 14:3-4,bali kama nabii amefunuliwa jambo kama hili la ndoa,atumie hekima ya kumwambia mwenye kumwombea kuwa kuna vita kali kwa ndoa yake na maombi mengi zaidi ni muimu sana.Unabii umevunja ndoa nyingi za watu maana wengi wanaotoa unabii huu hawajasoma BIBLIA VIZURI

BIBLIA inasema (WAEFESO 4:11"Naye amewaweka wengine kuwa wa kwanza mitume,pili manabii,tatu wainjilisti,wachungaji na waalimu." Hizi ni huduma tano na hupeanwa na Roho mtakatifu.Unapoasi kwa kazi hizi,ROHO MTAKATIFU huondoka na mtu huanza kutumiwa na maroho ya shetani na watu wengi huenda wakakosa ufunuzi kama huu.Sifa zingine za nabii wa ukweli ni kuwa,yeye(hampingi nabii mwingine wa kweli bali nabii wa uongo humpinga yule wa kweli maana MUNGU hakuumba nabii mmoja tu(1Wafalme 22:24 Tunamwona Zedekia akimpiga kofi nabii wa MUNGU Mikaya)Peleleza vizuri kupitia maombi unapotaka unabii wa Yehova.
Asante kunisikiliza maana nimekiwasilisha alichonituma YEHOVA MUNGU.
By  Geoffrey Mwanza.
For Assistance call "THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES": O724 656 653.

Comments