WATANZANI TUWE MAKINI TUSILETE LAANA JUU YA ARDHI YA TANZANIA KWA MAUAJI YA ALBINO.



Na Emmanuel Kamalamo
Kila aliyezaliwa katika ardhi ya Tanzania anayo haki ya kimsingi ya kuishi. Na kuishi kwa kila Mtanzania yeyote awe TAJIRI, MASIKINI, KIPOFU, KIWETE, ALBINO nk kuna tokana na UHAI unaotoka kwa Mungu.
Mwanzo 2:7 "BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Hivyo PUMZI iliyo ndani ya mwanadamu yeyote ni SEHEMU YA NAFSI YA MUNGU maana imetoka katka nafsi ya MUNGU.
UHAI UNAOTOLEWA KWA NGUVU ZA MWANADAMU UHAI HUO UNALIA KATIKA ARDHI HIYO NA KUACHA
MADHARA KATIKA NCHI.
Uhai umo katika damu, na mtu unapo MUUA mwenzako ile damu itamwagika katika ARDHI na kutoka katika hiyo ARDHI sauti ya ule UHAI inalia mbele za Mungu.
Mwanzo 4:10-11 "Akasema, umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako"
Watanzania mlio na roho za ukatari msio na utu wa kibinadamu mnao mwaga DAMU ZA WATU wakiwemo ALBINO mjue ya kwamba katika MIKONO YENU damu hizo mtadaiwa na mnadaiwa mpaka SAA YA MWISHO kama MSIPOTUBU NA KUACHA NJIA HIYO.
Na hapo nchi yote ya TANZANIA inaingia katika LAANA inayotokana UHAI wa watu wanaokufa kupitia mikono ya WATANZANI wasio na utu wa kibinadamu. Mwanzo 4:11 "BASI SASA, UMELAANIWA WEWE KATIKA ARDHI.."
Hivyo LAANA inapoingia inaanzia kwako mpaka mpaka kwa wote wasio fanya DHAMBI hiyo, maana ARDHI YOTE IMEBA LAANA.
Laana ikiingia katika Nchi basi ujue uharibu wa aina yoyote unaingia katika nchi kwa sababu haina ULINZI WA MUNGU maana tumemkorofisha Mungu kwa watu wale wanaoutoa UHAI (PUMZI YA MUNGU) kwa watu aliowawekea Mungu.
AGIZO
WALE WOTE WANAOJUHUSHA NA
UUAJI WOWOTE NA WALE WANAO
WADANGANYA KUWAUA ALBINO
KUWA KUNA UTAJIRI KUPITIA WAO

Watoto wazuri kama hawa Albino wanatafutwa kuangamizwa kwa sababu ya tamaa tu za pesa na madaraka.
=MTU HIYO NI DHAMBI=
MAANDIKO YANASEMA...."MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI" (Warumi 6:23)
WOTE WANAOWAUA WENZA MJUE
MNATENDA DHAMBI KWA MUNGU NA
KAMA MNATENDA DHAMBI BASI
MJUA KUNA MALIPO MTAYAPOKEA TU.

USALAMA WENU NI KUMRUDIA MUNGU NA MUNGU ATAWASAMEHEE
WATU WA MUNGU
(WALIOOKA)

TUSISAHAU KUOMBA TOBA KWA NCHI
YETU, VIONGOZI WETU, NA WATANZIA
WOTE .

(2 Nyakati 7:14 "Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha , na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi , niyasikia toka mbibguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao")
MWENYE MASIKIO YA KUSIKIA........!!

Comments