AINA MBILI ZA WAKRISTO

Na Baraka Kiponda.
1.WENYE MSINGI WA KANISA LA KWANZA.

 Hawa ni Wale ambao wanafuata Msingi wa Kanisa la Kwanza la Kina Petro,Wanaposikia Anguko au Mapito ya Mtumishi Fulani Mfano.Mchungaji,Mwalimu,Mwinjilisti,Mtume,Nabii,Shemasi,Muimbaji nk.Wao huingia Magotini na Kumlilia MUNGU na kuomba tena kwa Mzigo,Watu wa aina hii hawapo tayari kusikia habari za Nje..Kwani habari zingine ni za kizushi za kutengenezwa zimejaa chumvi na ujinga Mwingi.. 

Wenye Msingi huu wanajua wajibu wao wa kuongea na MUNGU tu.Kwani hawaamini Kumtegemea Mwanadamu katika mambo yao,hautawakuta wakiwa na wazo la kutoa Rushwa ila utawakuta wakikesha na kuomba. Matendo 12:5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. 

2.TOLEO JIPYA (WASIOFUATA MSINGI WA KANISA LA KWANZA.

 Aina hii ni wale ambao wapo tayari kusikia na kukubali habari za kizushi,wengi wao wamejaa udhehebu,ushabiki na uzushi mkubwa hawapo tayari kuchekecha PUMBA NA MCHELE.na hawana hata muda wa kusugua Magoti kumuomba MUNGU,Wanazisikiliza habari za kutengenezwa zaidi kuliko kumsikiliza MUNGU.Wanaisikiliza Mizimu zaidi,hata wakiwa Serikalini wapo Tayari kumpendeza bossi wao ambaye ni Mwanadamu mwenzao,Hawana Muda na MUNGU. 

Esta 6:1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, nayo yakasomwa mbele ya mfalme. 2 Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero. 3 Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo? Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna alilofanyiziwa. 4 Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari. 5 Basi watumwa wa mfalme wakamwambia, Tazama, Hamani yupo, amesimama behewani. Mfalme akasema, Na aingie. 6 Basi Hamani akaingia. Mfalme akamwambia, Afanyiziwe nini yule ambaye mfalme apenda kumheshimu? Hamani akasema moyoni mwake, Ni nani ambaye mfalme apenda kumheshimu kuliko mimi? 7 Basi Hamani akamwambia mfalme, Yule ambaye mfalme apenda kumheshimu
 Wakristo wa aina hii wamejaa lugha chafu,hawawezi kumtia moyo mwenzao ni Mashabiki wa upande Fulani.Ni wagumu pia kuamini Biblia.Wapo tayari kuamini Magazeti na taarifa zingine za kizushi.. Wewe huko wapi?? Usinijibu..

Comments