BAADHI YA KWELI AMBAZO NI MSAADA KATIKA MAISHA YA WOKOVU Sehemu ya 1.

Na Nickson Mabena.
Utangulizi
Mpendwa katika Bwana, karibu sana tujifunze Somo hili,
Namwamini Mungu kwamba hutakosa kitu cha kujifunza utakapolisoma na kulitafakari!,
Roho Mtakatifu yopo hapo karibu kukufundisha zaidi
.
Ukiona umepata jambo la kukusaidia unaweza ukamshirikisha na Mwenzako, ili tubarikiwe Pamoja!

Somo Hili limeandaliwa ili Kujenga Msingi Imara katika suala la wokovu na kutunza kibali kwa kutumia hekima yaKiKristo, Maana vita ni vikali.
Umetumika mtindo wa Mithali na Mafumbo lakini yenye maana pana sana, Pia kuna misemo ambayo inaweza inaweza kusaidia kujua kweli husika. Karibu tena tujifunze pamoja ili tupate Maarifa yatakayotusaidia kushinda.
1.UPENDO HAUSHINDWI KAMWE.
1Kor 13:4-8.
Kwenye Maandiko hayo zimeelewa sifa nyingi sana za Upendo. Zingine huonekana ngumu sana kwa baadhi ya watu!, Lakini naomba kwanza tuangalie aina za Upendo, ambao zitatusaidia kuelewa vizuri kweli hii kwa mapana yake!.

AINA ZA UPENDO
Mara zote unapotajwa Upendo, inaweza ngumu kujua kwa haraka ni upendo gani hasa unaomaanishwa! Lugha ya Kiswahili imekosa kutoa tufauti za Pendo kama zinavyotakiwa kutumiwa na mtumiaji, kwa sababu hiyo imekua ngumu sana leo hii kwa Kijana wa Kiume kumwambia binti NAKUPENDA, kwani binti ataanza kujiuliza sana, Ananipenda kivipi!?, na jibu atakalopata ni aina moja tu, ya Upendo!.
HUBU NIANZE NA UFAFANUZI KWA KIFUPI KUHUSU AINA ZA UPENDO!.
Zifuatazo ni Aina za Upendo;-
a) Upendo wa Kimwili (Mke na Mme, au wa kimapenzi).
b) Upendo wa Kawaida (Kirafiki)
c) Upendo wa Nasaba (Wa kidini, kikabila, kiukoo n.k)
d) Upendo wa Agape (Upendo wa Mungu)

Upendo ambao Mungu ametuagiza ni Upendo wa AGAPE, Upendo Usio na Sababu, yaani kama yeye alivyotupenda sisi!!.
Mwingine anajiulia, ntampendaje Adui yangu!?, inaweekana sana kuwapenda adui zetu kutokana na Upendo huu wa Kimungu ambao Mungu huuachilia mioyoni mwetu kwa Roho wake Mtakatifu aliyetupa Sisi (Rumi 5:5).
Sifa za Upendo huu wa Agape ndio zipo kwenye hayo maandiko (1KOR 13:4-8).
Usipozijua aina hizo za Upendo, huwezi kumuelewa Paulo alichomaanisha kwenye maandiko hayo, hebu mwenyewe jiulize Biblia ina maana gani inaposema “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha masikini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu” 1Kor 13:3
Kwani kutoa mali kwa ajili ya masikini sio UPENDO!?, Jibu ni Upendo, lakini ni Aina Ipi ya Upendo!?

Ndugu kumbuka, amri kuu ni UPENDO, hata Amri 10 ambao Musa alipewa (KUTOKA 20:1-17)., alipokuja Yesu akazigawa katika Makundi Makuu mawili (AMRI KUU MBILI).
Hebu tusome Mathayo 22:35-39) “Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; Mwalimu katika Torati ni Amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Umeona mgawanyo huo wa Amri 10?, pengine hujaelewa, ona;
a) .Mpende Bwana Mungu wako (AMRI YA 1 hadi 4)
b) .Mpende Jirani yako kama nafsi yako (AMRI YA 5-10).

Ndugu, tumeagizwa Upendo (YOH 13:34), kama vile Yesu alivyotupenda tungali wenye dhambi, hata kama umetendewa nini, tupendane kwa upendo wa Yesu! Utashinda tuu,
kwenye Chuki weka Upendo, kwenye machafuko, kuonewa, ugomvi wewe weka Upendo na Utamwona Mungu!!.
“MUNGU NI PENDO, ndiyo maana Kweli hii inasema Upendo haushindwi yaani maana yake ni MUNGU HASHINDWI”.
2. BILA MAUMIVU HUWEZI KUPATA.
RUMI 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.
Kujitoa ndiyo pointi kuu kwenye maandiko hayo, lakini Mungu ameweka msisitizo kwenye kujitoa baada ya kusema
“itoeni miili yenu iwe dhabihu”. Dhabihu ikitolewa huwa hairudishwi kwa aliye itoa, sasa Mungu anachotaka tujue hapa, ni KUJITOA KIKAMILIFU BILA KUJIONEA HURUMA.
Kwa hiyo ibada yenye maana kwetu ni kuitoa miili yetu iwe Dhabihu!
Lakini Mungu ameahidi kumlipa mtu huyu anayejitoa kwa MAUMIVU, kwani “Kila atoaye hupokea”.

Kitu chochote unachotaka kupata ni lazima upitie Maumivu flani, ndiyo maana hata ukitaka kumwona Mungu kwenye Maisha yako lazima Umtafute kwa BiDII.
Neno linasema hivi, “Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona”. MITH 8:17

Maana yake ni hii, unaweza ukataka kumwona Mungu, lakini usipomtafuta kwa BIDII huwezi kumwona!. Ndiyo maana watu wengi sana wana Kiu ya kumuona Mungu, lakini wanashindwa kumuona kwa sababu hawataki kuingia gharama(PAIN) ya kumtafuta kwa BIDII ili wamuone!.
JE! Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wengi bado wanakimbiakimbia, kuzunguka kutafuta miujiza!?, Kwa nini wanataka kutafuta kuombewa na Sio KUOMBA!?
Mungu anaweza kumtumia kila Mtu,
Ongeza bidii kwenye Kumtumikia Mungu, Mtafute yeye siku zote (1Nyakati 16:11), hata kama changamoto ni nyingi kwa sasa, lakini Mungu ni mwaminifu lazima ataonekana kwako

Muombe Mungu akupe stamina (Nguvu za rohoni), ili unapokutana na maumivu usirudi nyuma.
Usijali hata kama maendeleo yanachelewa kwako, Mungu anasema “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”. Mith 13:11
Mungu akuzidishie kwa Jina Kuu La Yesu Kristo!

Hichohicho kidogo unachopata kwa maumivu makubwa ridhika nacho kwani “Kidogo alichonacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi” Zaburi 37:16
Uberikiwe kwa kuusoma ujumbe huu!
........Somo,litaendelea......

Comments