DONDOO MBALIMBALI KUTOKA KATIKA MAFUNDISHO YA SEMINA ZA MCHUNGAJI PETER MITIMINGI.

Na Mchungaji Peter Mitimingi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Huduma ya VHM.
BWANA YESU asifiwe.
Karibu ujifunze kitu kutoka katika dondoo tu za masomo mbalimbali ya ndoa  kutoka kwa Mchungaji Peter Mitimingi wa The Voice Of Hope Ministry.

Hizi ni Dondoo tu.

KABLA WANANDOA HAWAJATENGANA KIMWILI HUANZA KUTENGANA KATIKA MAENEO 7 YAFUATAYO:
1. Kutengana Kimawazo
2. Kutengana Kimtazamo
3. Kutengana Kiimani
4. Kutengana Kimaono
5. Kutengana kimipango.
6. Kutengana Kifedha.
7. Kutengana kihisia
8. Mwishoni ndipo humalizia kwa kutengana kimwili.
Ukiwaona watu wanatengana kimwili leo, ujue matengano ya ndani kwa ndani yalianza miaka mingi iliyopita. Matengano ya kimwili ni hitimisho tu.


=BABA ANASAIDIA KUMFANYA MTOTO WA KIUME AWEZE KUWA MWANAUME.

Watoto wa kiume ambao wamekuwa bila malezi ya baba au mlezi wa kiume wana matatizo sana wanapofikia utu uzima. Kukua pasipo kuwa na baba au mlezi wa kiume ina madhara makubwa kwa mtoto wa kiume ambayo hudumu mpaka utu uzima wake. Watoto wa kiume wanahitaji kuwa na baba au mlezi ili waweze kujua namna ya kuwa wanaume. Bila kuwa na ushawishi huu katika maisha yao watoto wa kiume wana hatari kubwa ya kuwa wanaume ambao wana matatizo ya kitabia, msimamo wa kihisia na mahusiano ambayo itaathiri wengine na watoto wake pia.


 BABA AMEBEBA NGUVU ZA NDANI ZA MTOTO NA SIO MAMA!
Mitimingi na mkewe katika 1 ya semina.

Katika somo hili nitamzungumzia baba zaidi kwasababu imeonekana matatizo mengi ya tabia za watoto na makuzi yao yamechangiwa na nafasi ya baba zaidi ya nafasi ya mama.
Katika siku za nyuma ilijulikana kwamba mama wa mtoto ndio ananguvu za kumathri mtoto kwa sehemu kubwa sana kuliko baba. Lakini katika tafiti za hivi karibuni zimebaini kwamba baba wa mtoto anayo nafasi kubwa sana katika kujenga undani wa mtoto kwa kutokea ndani kuja nnje (a child well being). Wababa wengi sana hawajui juu ya ukweli huu kwamba wao wanasehemu kubwa sana ya mafanikio au kushindwa kwa maisha ya mtoto. Wanaume wengi wamewaachia wake zao kulea na kuwakuza watoto bila uhusika wao.


Mchungaji Peter Mitimingi akifundisha katika moja ya semina kwa wanandoa.

Comments