HOSANA NI NINI?


"Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; wakatwaa matawi ya mtende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakipiga makelele, HOSANA! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!"
=> YOHANA 12 : 12-13

Siku sita kabla ya pasaka Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu
{YOH 12 :1}. Mji huu uliokuwa jirani na Yerusalemu yapata maili mbili hivi
{YOH 11 :18}, hii ni sawa na kilomita 3 na robo (mwendo wa kama saa moja kwa miguu). Ambapo alikaa na siku iliyofuata ndipo akakwea Yerusalemu.

Na wimbo wa HOSANA ndio ilikuwa ya mapokezi Yake. Neno hili imetokana na lugha ya kiebrania;
Yàsha ~ nâ => Tuokoe/Tukomboe/Tufanikishe sasa tunaomba.

"Ee BWANA, utuokoe, twakusihi; Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi".
=> ZABURI 118 : 25

Nayo ilipotumika kwa lugha ya Kiyunani ' Ho.san.na ' katika hali ya sifa ilimaanisha;
- Tunakusifu BWANA kwa kuwa utatuokoa.
- Tunakusifu BWANA kwa kuwa utatukomboa.
- Tunakusifu BWANA kwa kuwa utatuponya.
- Tunakusifu BWANA kwa kuwa utatufanikisha.
- Tunakusifu BWANA kwa kuwa utatutetea.

Hii ndio sababu, Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu watu waliokuwa wameona na walio kuwa wamesikia sifa za matendo Yake makuu; walimpokea wakipaza sauti zao wakisema, 'HOSANA!'. Naye kwa uaminifu alisimama katika nafasi ya kutimiza kilio chao.
Nasi tunapoitumia iwe kwa sifa au kwa kukiri tutamwona BWANA AKIJIDHIHIRISHA !!
" Amina".

MUNGU akubariki.
By Gidion Mwangaza

Comments