ILI UMPATE MKE AU MUME WAKO WA KWELI USIJARIBU KUMTAFUTA ULIMWENGU WA MWILI.


Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Jambo hili ni muhimu kulijua hasa kwako dada au kaka unayetaraja KUOLEWA /KUOA.
Nataka kusema nini, ukisoma Waefeso 2:6 anasema..."Akatufufua pamoja naye,akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu"
Pia linganisha na Waefeso 1:3 anasema ."Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni,katika ulimwengu wa roho,ndani yake Kristo Yesu'' unapata picha gani unaposoma mistari hii? Picha tunayopata hapa ni kwamba, TULIPOOKOKA tukaketishwa pamoja na Yesu katika ULIMWENGU WA ROHO.Je, ni nani "AMEKETISHWA"? Aliyeketishwa ni yule mtu wa "ROHONI"
Hivyo mtu huyo wa rohoni ambaye ni wewe, kuna BARAKA tayari umekwisha barikiwa (unazo katika ulimwengu wa roho) moja wapo ya baraka hizo ni MUME / MKE mwema uliyekwisha kuandaliwa tayari. Maandiko yanaposema...."NYUMBA NA MALI NI URITHI MTU APATAYE KWA BABAYE; BALI MKE MWENYE BUSARA MTU UPEWA NA BWANA" Mithali 19:14.
Mke wa Adam aliandaliwa mapema mke wake katika ulimwengu wa roho. Alipoumbwa Adamu Hawa naye aliumbwa, Mwanzo 1:27 Anasema...."Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba " Hii ni sura ya kwanza inayozungumza maandalizi ya kuwaumba Adamu na Hawa katika ulimwengu wa roho. Lakini aliyeanza kuja ulimwengu wa MWILI ni Adamu. Anaposema akamtoa Hawa katika UBAVU wa Adamu maana yake anamtoa yule mwanamke waliyeumbwa pamoja naye katika ULIMWENGU WA ROHO.
Najaribu kukupa mfano wa namna hiyo ili ujue kabisa swala la MKE /.MUME ni swala la ulimwengu wa roho,kama hutajua siri hii na ukaamua KUOA / KUOLEWA na yeyote kisa unaona hakuna anayekutamkia KUKUPENDA sasa unaamua kujilahisisha mwenyewe, uwe na uhakika hiyo NDOA yako inaweza kukushinda kwa sababu siyo mpango wa Mungu uwe na huyo.
Kama ''UMEKETISHWA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO " fahamu na mke /mme wako "AMEKETISHWA ULIMWENGU WA ROHO " Swala ni wewe tu kumuomba Mungu akupe kwa kumtoa katika katika ulimwengu wa roho ambaye pia ni BARAKA moja wapo aliyobarikiwa mtu wa rohoni (wewe uliyeokoka) na kumdhihisha ulimwengu wa damu na nyama. Nakwambia ukimwona kwa mara ya kwanza moyo wako utasema tu...."SASA HUYU NI MFUPA KATIKA MFUPA YANGU, NA NYAMA KATIKA NYAMA YANG....."

UBARIKIWE SANA

Comments