JE UMEMKANA YESU AU UMEJIKANA KWA AJILI YAKE.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Kwenye Biblia Kuna Maneno Mawili Nataka Niyazungumzie. KUKANA Na KUJIKANA. 
2 Kor 4:2 ''lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU.''
Jambo la kujua na kuzingatia ni kwamba ''BWANA anataka tusimkane ila tujikane kwa ajili yake''
Usiwe unayemkana YESU bali uwe uliyejikana kwa ajili yake.
=KUKANA ninakokuzungumzia mimi Ni Kumkataa MUNGU Hadharani. 
Mtu Anamkataa MUNGU Kwa Njia Ya Kueleza Hadharani Kwamba Yeye Si Mtu Wa MUNGU.
Anamkana kwa matendo yake, au kwa imani yake au kwa maneno yake.
1 Yohana 2:22-23, Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa YESU ni KRISTO? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye BABA na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye BABA; amkiriye Mwana anaye BABA pia.
-Ndugu yangu, jambo la kwanza nataka ujue ni akina nani wanaomkana MUNGU na wanamkanaje.
Biblia imeweka wazi kabisa kwamba wanaomkataa YESU hao wanamkana MUNGU na kumkana MUNGU ni kuukana hata uzimawa milele.
-Kama kuna mtu anasema yeye anaye MUNGU huku anamkataa YESU kuwa Mwokozi wake, huyo hana MUNGU bali ana jini tu.
-Anayemkana YESU huyo anamkana MUNGU mwenyezi.
-Aliye na YESU huyo ana MUNGU.
Swali; Je wewe una YESU hata useme una MUNGU?
Kama Huna YESU wewe huna MUNGU.
Kumjua YESU ni kumjua MUNGU aliye hai milele.
Biblia inasema kwamba KRISTO ni siri ya MUNGU ,
Wakolosai 2:2b ''wapate kujua kabisa siri ya MUNGU, yaani, KRISTO;''
-Kumjua KRISTO ndio kumjua MUNGU. Kukataa YESU ni kuukataa uzima wa milele.
Watu wengi leo wanamkana MUNGU kwa sababu ya kushika mafundisho ya manabii wa uongo.
2 Petro 2:1-2  '' Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata BWANA aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. ''
-Kuna watu leo kwa sababu ya kushika mafundisho ya uongo leo wanamkana YESU na kudhani kwamba  kuna mwingine anayeweza kuwaokoa kumbe hakuna.
-Kuna watu hudhani tu kwamba YESU ni nabii na kuna watu hudhani tu kwamba YESU ni ishara ya siku ya mwisho, kumbe wamesahau kwamba YESU ndiye mhukumu na yeye ndiye atawahukumu watu wote na hata sasa kila mtu anajua kwamba atakaerudi siku ya mwisho ni YESU ila wanasahau kwamba atakuja kufanya nini, shetani amewapofusha na hawajui kwamba Hukumu yote ina YESU KRISTO. Watu hata wamemkana YESU na MUNGU pia. 
 Ndugu, unatakiwa ujiulize je YESU ni nani kwako. Je unakana YESU? 
kuna jinsi nyingi za kumkana YESU na kumkana MUNGU aliye hai.
-Kuna watu wamemkana MUNGU kwa sababu ya kushika mafundisho ya mashetani.
Wagalatia 2:20 ''  Nimesulibiwa pamoja na KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali KRISTO yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa MUNGU, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. ''
Andiko hilo hapo juu ndio sifa ya mtu ambaye hamkani YESU bali anamtii kama BWANA na MKOMBOZI wake. 
-Lakini watu wamemkana MUNGU kwa kuikataa kweli yake.

 -Kutenda Dhambi Ni Kumkana MUNGU Tena Ni Kuikana Imani Ya KRISTO
Tito 1:16,Wanakiri ya kwamba wanamjua MUNGU, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. 
-Ndugu, hakikisha hutendi dhambi maana kutenda dhambi ni kumkana MUNGU.

Ndugu, jambo la kujua ni kwamba Ukimkana BWANA YESU Na Wewe Utakanwa Usipotubu
Mathayo 10:33 '' Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za BABA yangu aliye mbinguni.''
-Kumkana YESU ni kuukana na kuukataa uzima wa milele. 
-Ndugu, katika maisha yako usije ukamkana YESU iwe kwa matendo yako au hata kwa matamshi yako.

 2 Timotheo 2:11-13''  Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. ''
-MUNGU wa kweli hatakiwi kukanwa kwa jinsi yeyote bali tunatakiwa kama watu wake tujikane sisi kwa ajili yake.

= KUJIKANA Maana ni  Kukataa Ubinafsi. 
Mtu anatakiwa kujikana Kwa Ajili Ya KRISTO Akikubali Maisha Yake Yatawaliwe Na KRISTO Badala Ya Kujitawala Mwenyewe. Anaahidi Kumtii KRISTO Siku Zote Hata Kungekuja Mabaya
Mathayo 16:24-27,Wakati huo YESU aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa BABA yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 

 -Watu Waliounganika Na KRISTO Lazima Wajikane, Lazima Wajikane Kwa Njia Ya Kuacha Tabia Na Tamaa Za Dunia, Na Kuisha Maisha Ya Kumcha MUNGU.
 Wakolosai 3:5 ''Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;''.
Anayetii hayo ambayo Biblia imesema kwenye andiko hapo juu, huyo hakika amejikana kwa ajili ya KRISTO na kwa ajili ya uzima wa milele.

Hii ya waliojikana kwa ajili ya KRISTO YESU na kwa ajili ya uzima wa milele.
Tito 2:11-13 '' Maana neema ya MUNGU iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu; '' 
-Ndugu, je umejikana kwa ajili ya KRISTO au umemkana?
Ni saa ya kujikana na sio kumkana. kama ulimkana miaka iliyopita tubu na hakikisha kuanzia leo unajikana kwa ajili yake, kataa dhambi, ogopa dhambi, ikimbie dhambi na usifanye dhambi; huko ndiko kujikana.
 ''Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. -2 Kor 5:17''
 -Ndugu, hakikisha unakuwa mpya ndani ya KRISTO ukiishi maisha ya bila kumkana wala kutenda dhambi, bali jikane wewe kwa ajili yake ili umpendeze siku zote.

Ndugu Yangu, Usikubali Kumkana YESU Na Hakikisha Unajikana Ili Umpendeze MUNGU. 
Usitende Dhambi Maana Kutenda Dhambi Ni Kumkana BWANA YESU. 
Ukidumu katika mema bila kumkana YESU utafanya vyema.
Yeye BWANA YESU anasema ''  Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. -Yohana 10:28 ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments