JE UNATUMIKA KWA NANI?

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tule chakula cha uzima wa roho zetu.
Neno la MUNGU ni chakula cha roho zetu, ukiwa unakula chakula hiki na kushushia na maji safi ambayo ni maombi katika ROHO MTAKATIFU hakika lazima tu uwe na afya nzuri ya kiroho.

Je unatumika kwa nani?
Ni ujumbe ulio katika mfumo wa swali muhimu.
Kuna watu wanamtumikia MUNGU na kuna watu wanamtumikia shetani.
Kumtumikia BWANA sio kuitwa Mchungaji au Askofu bali kila anayedumu katika neno la MUNGU na kulitenda huyo ni mtumishi wa MUNGU.
BWANA YESU anasema ‘’ Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, BABA atamheshimu. –Yohana 12:26 ‘’
BWANA YESU anatafuta watumishi ili wamtumikie yaani wampokee na yeye atawaokoa, na pale atakapokuwapo yeye na wao watakuwa hapo hapo.

Mtumishi wa MUNGU humtii MUNGU na ukiona ameacha kumtii MUNGU tambua kwamba huyo sasa sio mtumishi wa MUNGU bali ni mtumishi wa shetani jambo ambalo ni baya.
Waliompokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yao hao ni watumishi wa MUNGU aliye hai.
Hao ni watumishi wa BWANA YESU, ni watu ambao MUNGU anawatafuta na anawapenda sana.

Ndugu yangu, chagua kumtumikia MUNGU leo kwa kuokoka.
Yoshua 24:15 ‘’ Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.’’
-kumbe kuna wanaomtumikia MUNGU aliye hai na kuna wanaomtumikia shetani.

Sio wote wanaojiita watumishi wa MUNGU kweli ni watumishi wa MUNGU wengine wana ajenda za siri ili kuwakwamisha watu wa kanisa hasa wasio waombaji, hilo ni jambo baya sana.
Ni heri kuwa mtumishi wa MUNGU wa kweli.
-Kuna wengine bado hawajaanza kumtumikia MUNGU hata kama wako kanisani, ho wanatakiwa kubadilika.
-Kuna wengine bado hawajaanza kumtumikia MUNGU hata kama huwa wako madhabahuni, hao wanatakiwa kubadilika.

Biblia hapo juu inatoa majibu ya wanadamu wa leo kwamba wanamtumikia nani.
Kuna wanaomtumikia BWANA MUNGU na kuna ambao wanamtumikia shetani.

Ndugu yangu, je wewe binafsi unamtumikia nani?
1 Samueli 12:14-16 ‘’Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, MUNGU wenu, vema! Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu.’’

-Kuna watu makanisani bado hawajaanza kumtumikia MUNGU maana wako upande wa shetani.
Ni jambo baya sana maana ni hasara kwao kama hawatatubu.
-Kuna watu humtumikia MUNGU kwa vinywa vyao tu lakini matendo yao yanamtumikia shetani.
Ni hatari na ni hasara maana wasipotubu na kurejea ni mbaya.
-Kuna watu humtumikia MUNGU kwa sadaka na matoleo tu lakini matendo yako bado wanamtumikia shetani.
Hawa wanajifurahisha tu katika udhalimu maana mbinguni wataingia watakatifu tu.
-Kuna watu humtumikia MUNGU wakiwa kanisani tu lakini wakitoka kanisani huanza kumtumikia shetani.
Je wewe unamtumika nani?

1 Nyakati 28:9 ‘’ …… mjue MUNGU wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele. ‘’
Watumishi wa MUNGU waaminifu ni wale waliompokea BWANA YESU na sasa wanaliishin neno la MUNGU, Yeye YESU KRISTO anasema neno hili juu yao ‘’ Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. –Yohana 14:3 ‘’

-kuna watu humtumikia MUNGU jumapili tu au jumamosi lakini siku zingine wanamtumikia shetani.
Ni hasara na mbaya sana maana haina majibu mazuri baadae baadae baada ya kifo.
-Kuna watu humtumika MUNGU muda tu ambao wao wanaimba lakini wakimaliza huduma huanza kumtumika shetani.
Hao kama wasipotubu BWANA YESU atasema siku ile kwamba ‘’Siwajui ninyi’’
Ndugu, MUNGU ni MUNGU na shetani ni shetani, usikubali kumchanganya MUNGU na shetani.

Zaburi 2:11-12 ‘’ Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora asije akafanya hasira, Nanyi mkapotea njiani,Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi,Heri wote wanaomkimbilia. ‘’
-Kuna watu humtumikia MUNGU kipindi tu waume zao au wake zao wakiwapo, lakini wakiondoka au wakifariki hurudi kumtumikia shetani.

Hao hawajajua wanalolifanya.
-Kuna watu humtumikia BWANA YESU kipindi wazazi wao wakiwa hai, lakini wakifariki tu hurudi kumtumikia shetani.
Hao hawajitambui na wanahitaji neema ya MUNGU.
Kuna watu humtumika MUNGI kipindi tu viongozi wao wakiwa hai lakini wakifariki huanza kumtumika shetani.
Ndugu zangu, wateule wa BWANA YESU ndio watumishi pekee wa MUNGU, Warumi 1:5-6 Biblia inasema ‘’ ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo; ‘’

Ona mfano huu
Waamuzi 2:19 ‘’ Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi. ‘’
-Hawa waisraeli ni mfano hai kwa watu wa kizazi hiki ambao humtumika MUNGU kipindi ambacho viongozi wao wakiwa hai lakini wakiondoka na wao huondoka katika BWANA YESU na kuiandama miungu na sanamu. Ni machukizo haya na ni kazi ya hasara sana.

Ni heri kuwa mtumishi wa KRISTO, 1 Kor 4:1 ‘’ Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU. ‘’
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments