JIEPUSHE NA MAKANISA AMBAYO HAWAMHITAJI YESU KRISTO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima 
Yohana 4:24 ''MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.'
Andiko hili halihitaji maoni wala ushauri bali kama tu mnataka kumwabudu MUNGU Mwenyezi lazima mmwabudu katika roho na kweli.

Heri kuondoka kwenye kanisa ambalo mafundisho yake hayakupeleki mbinguni bali jehanamu, kuliko kubaki kwenye kanisa hilo linalokupotosha huku viongozi la kanisa hilo wakikufariji kwamba utaenda mbinguni wakati mafundisho yao sio ya jinisi ya KRISTO. huku wakisema kwamba roho ya kuhama hama madhehebu ni mbaya.Kama wanafundisha uongo harafu wanakutisha kwamba usihame hao wahafai, mimi mtu akihubiri kristo mwingine tofauti na BWANA YESU KRISTO  huko naondoka siku hiyo hiyo maana hao ni wapotoshaji kabisa.
Usiwavumilie hao maana watakupeleka tu jehanamu kwa mafundisho yao ya kuigeuza Biblia ili iwafuate wao wanavyotaka kuliko wao kuifuata Biblia inavyotaka.

2 Kor 11:3-4 ''Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa KRISTO. Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! ''


inahitajika kuomba maombi kama haya 
''BABA MUNGU wa mbinguni tupe kuona kama uonavyo wewe maana macho yetu ya kibinadamu yanatupotosha hata hatuoni ukweli. ''

Ndugu zangu, tunakiwa tuichunguze kila roho kama inatokana na MUNGU au mashetani, 


 'Biblia inasema 
''Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili yatokana na MUNGU.  Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani- 1 Yohana 4:1-3

kuna watumishi wana mapepo ya utambuzi, mtu kama huyo akikuambia jambo lako ambalo ni la kweli unaweza ukadhani ni ROHO wa MUNGU amemfunulia kumbe mapepo ya utambuzi ambayo ni mawakala wa shetani na lengo lao ni kukunasa na kukupeleka kwenye mafundisho yao ambayo wala hayako kwa jinsi ya KRISTO.

Mathayo 24:4-5 "YESU akajibu akasema angalieni mtu asiwandangaye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo nao watadanganyika wengi."

 Kuna gazeti la kidini moja ukilisoma unaweza hata kupata kizunguzungu maana wanasema YESU alikuwa roho na kazi yake iliishi katika kizazi sijui cha ngapi na sasa mtumishi wa kanisa hilo ndiye kristo wa wakati huu. ni ushetani ambao hata mtoto mchanga atakukatalia lakini cha ajabu kanisa kama hilo kuna waumini maelfu na wana akili timani kabisa.



2 Thesalonike 2:3-4 ''Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho MUNGU ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. ''
-kumbe wapinga KRISTO wengine watakate hadi kwenye hekalu la MUNGU. Ni nyakati mbaya sana hii.
Ni wakati wa  kumwambia BABA wa mbinguni atupe macho ya kuona, atupe macho ya ndani ambayo shetani akija tu anaonekana, kama yuko kwa mtumishi anaonekana vile vile vile.

Kuna waumini hata Sijui wanasoma Biblia gani maana BWANA YESU anatukanwa hadharani kanisani kwao na wao bado wapo huko na wanajiita wakristo.
BWANA alituonya mapema.

Mathayo 24:23-26. "Wakati huo mtu akiwaambia tazama kristo yuko hapa au yuko kule msisadiki maana watatokea makristo wauongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza yamkini hata wateule. Tazama nimekwisha kuwaoya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani msitoke; yumo nyumbani msisadiki." 

 Makanisa mengi leo hudhani kwamba makanisa ambayo viongozi wao wanaitwa mitume au manabii basi ndio hao manabii wa uongo ambao BWANA YESU aliwasema. wengi hudanganywa na kudhani kwamba katika wale waitwao sasa mitume au manabii basi nabii wa uongo ni mmoja katika wao, kumbe wala haiko hivyo.
Ndugu zangu inawezekana kabisa baadhi yao ni watu wasio upande wa MUNGU kama tu wanafundisha kinyume na KRISTO YESU lakini walio wengu tunawasingizia maana tu wanaitwa ''Nabii'' au ''Mtume''. Nabii wa uongo ni yule mtumishi halijalishi anaitwa askofu, mwinjilisti, mchungaji, mtume au nabii anayefundisha uongo. uongo wa injili yake ndio unaomweka kwenye kundi la manabii wa uongo hata kama hajiiti nabii. Lakini kuwa na manabii leo ni sahihi kabisa Kiblia na hakuna ubaya wowote maana MUNGU amewaweka wengine kuwa na huduma za kitume, wengine kinabii, wengine walimu, wengine wachungaji na wengine walimu. 
1 Kor 12:28-31 ''  Na MUNGU ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora. ''

Mitume wa ukweli wapo na mitume wa uongo pia wapo.
Binafsi ukiniambia jina ninalolipenda napenda kuittwa mwinjilisti lakini siwezi kujiita mwinjilisti kama huo uinjilisti hauko ndani yangu na wala sijawahi kumshuhudia hata mtu mmoja juu ya WOKOVU wa BWANA YESU.
 siwezi kujiita jina ambalo MUNGU hajanipa, siwezi kujiita Mwalimu au mchungaji, siwezi kujiita nabii wala mtume maana sitaki kuwa muongo. haiwezekani ujiite nabii au mtume wakati hujafungua tawi la kanisa lako hata moja. utume ni kuwafuata watu kila kona ili wamjue MUNGU aliye hai na waokolewe na BWANA YESU. Siwezi kujiita mchungaji wakati sina hata kondoo mmoja ambaye namchunga, huo ni uchungaji gani?
Kama wewe ni mchungaji hata kama umesomea, kama huna kondoo hata mmoja wewe bado sio mchungaji. Hivyo unatakiwa uwe mchungaji kwa kuwashuhudia watu habari njema za ufalme wa MUNGU ambao pekee unapatikana katika KRISTO YESU.

Biblia inawaitwa wanaofundisha uongo kwamba watakuja na dhihaka zao.


2 Petro 3:3 ''Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,''
  -Kanisa wanafundisha uongo, wanaabudu sanamu na midoli, wanamkataa KRISTO Kwanini uendelee kuwa muumini wa huko?
-Kama kanisa wanaigeuza Biblia na  na kugeuza majalada ya Biblia kwa uongo wa kutaka watu wajue kwamba wao ndio watakatifu, unasubiri nini huko?
-Kama kanisani kwenu KRISTO ni ziada tu katika mahubiri kila siku, unasubiri nini huko?
-Kama kanisani kwenu imani mmeiweka kwa mtumishi wenu  na kudhani kwamba mtumishi huyo  ana nguvu kuliko YESU KRISTO, Mnasubiri nini huko?
-Kama kanisani kwenu ni waabudu shetani, unasubiri nini huko?

Kuna makanisa viongozi wakuu wa huduma hiyo ni watu wazuri na wako sahihi kabisa ila wachungaji wasaidizi ni vipandikizi vya shetani. Hapo ndio kazi ipo.
Siku moja niliitwa sehemu fulani kanisani nilipofika kuna mchungaji msaidizi mmoja akaniita na kutaka kuweka mkono kichwani kwangu ili aniombee, nilikataa maana hakuwa mtu mzuri hata kama nilionana nae kwa mara ya kwanza siku hiyo hiyo. maana mikwara ni mingi kuliko Neno, mara anasema  mara aombe kiganja chako ili akiangalie na kukuambia yaliyoshika nyota yako. niliona ni uongo wa hali ya juu na hata mimi nina ROHO MTAKATIFU na sidanganyiki. kwanza sikwenda pale kuombewa maana hata mimi mwenyewe najua kuomba na nimewaombea wengi sana na BWANA YESU amewatendea makuu.
Yuda 1:17-18 '' Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa BWANA wetu YESU KRISTO, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu. ''

Ni heri kanisani ulipo mchungaji wako labda alishawahi kuanguka dhambini au anajikwaa mara nyingi lakini akageuka na kutubu huku akimhubiri YESU KTISTO aliye hai, Huko heri kuliko kwenda kuabudu kwa mawakala wa shetani.

Kiongozi mkuu wa kanisa ni muhimu sana kwa MUNGU na kwa shetani pia. 
Kiongozi huyo kama yuko upande wa shetani mtataabika sana, hawezi kuwa mwabudu sanamu harafu akafundisha somo linalokataza kuabudu sanamu. Waabudu sanamu wameandikwa mara nyingi sana kwenye Biblia, madhara ya kuabudu sanamu yameaandikwa mara nyingi sana kwenye Biblia lakini nyie kanisani kwenu hata siku moja halijawahi kusomwa andiko linalokataza kuabudu sanamu kwa sababu tu kiongozi wenu ni kipofu na yuko upande wa shetani, ndugu, huko unasubiri nini?
-Kama kongozi mkuu wa kanisa lenu ana pepo la ngono lazima tu ahalalishe na kuweka kwenye katiba ya kanisa lenu kwamba kuoa wake wawili ni sali maana yeye yalimshinda. anawatendesha dhambi na nyie ambao hata Biblia huwa mnasoma jumapili tu tena kanisani tu. anataka uzinzi wake uawateke wote kanisani, Kama kweli ni agizo zuri hilo la kuoa wake wawili basi hata wanawake awaruhusu waoelewe na wanaume wawili kwa wakati mmoja.

Ndugu zangu, BWANA YESU KRISO anatuonya akisema.
'' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho-Ufunuo22:11-13''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili. MUNGU Akubariki.

Comments