JINSI GANI TUNAWEZA KUISHI MAISHA YA USHINDI DHIDI YA DHAMBI.

Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Mungu akubariki wewe uliyesimama katika NEEMA ya Kristo Yesu ambayo ndiyo tumaini letu sisi tuaminio. Pia maombi yangu kwa Mungu ni kuona Mungu anazidi kukuhudumia kupitia mafundisho ya NENO LA MUNGU. Maana maandiko yanatwambia,"UWATAKASE KWA ILE KWELI; NENO LAKO NDIYO KWELI" Yohana 17:17.
Kwa kadri unavyolisoma Neno la Mungu na kuliweka moyoni kila siku lina kutasa na kukutenga na DHAMBI na hapo unafikia kiwango cha kuwa MTAKATIFU mbele za Bwana.
Tuangalie somo letu ambalo Roho Mtakatifu anataka atufundishe siku ya leo.
Kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti kwa watu juu ya kuishi maisha ya kushinda dhambi, na kuwafanya wengi kuwa "WATUMWA" wa dhambi.
Lakini natakaujue kuna NGUVU ya kumtuo mtu kwenye dhambi na akawa "HURU" ndivyo maandiko yananiambia,,"Basi Mwana, mtakuwa huru kweli kweli," (Yohana 8:36) kwa maneno hayo nikutie moyo kwamba yupo Yesu mwenye funguo za gereza la utumwa wa dhambi, endapo utampokea atakufungua utoke kama vile Rais alivyo na ufunguo wa mamlaka kuwafungulia wafungwa wakawa huru basi Yesu Kristo ni zaidi.
NINI KINA MFANYA MTU ATENDE DHAMBI?
>Ni Roho ya mtu kutokuzaliwa Mara ya pili, au kutokulishwa neno la Mungu. Maana hili Neno la Mungu Lina kazi kubwa ya kukuanda ukiwa hapa duniani kwa ujio wa Yesu Kristo. 1 Thesalonike 5:23 "Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati WA kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo," Katika maneno haya Paulo anapoliambia kanisa la Thesalonike juu ya "UTAKASO" wa "NAFSI, ROHO, NA MWILI" alizungumzia juu ya NENO linalotakasa. Mtu hawezi kupata utakaso nje ya Neno la Mungu, hayo ndiyo maombi aliyoyaomba Yesu kwa wanafunzi wake akisema,"MIMI SI OMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU; BALI UWALINDE NA YULE MWOVU....UWATAKASE KWA ILE KWELI; NENO LAKO NDIYO KWELI," (Yohana 17:15,16)
Sasa Anglia jambo hili lilivyo, unapokuwa hapa ujue shetani yupo, na kama yupo kazi yake ni kutaka kukuchafua NAFSI YAKO, ROHO YAKO NA MWILI WAKO ili Yesu anapokuja uwe na lawama mbele zake siku ile. Sasa linganganisha maombi ya Paulo na maombi ya Yesu utakuta wanalenga jambo moja la kwamba, Mungu anatukasa kila siku kwa NENO lake ili tusije tukakosa kuingia mbinguni. Nenda kaanfalie watu ambao hawana NENO LA MUNGU ndani yao hawana hofu ya kutenda dhambi miiyoni mwao, maana hakuna NENO la kuwatasa ndani yao na shetani amewachafua "NAFSI,ROHO NA MWILI" watu hawa Yesu akija lazima wawe na lawama mbele zake.
HATUA ZIFUATAZO ZITA
KUSAIDIA KUSHINDA
SHAMBI.

SOMA NENO LA MUNGU
Wakolosai 3:16 "Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu..," Hivyo ni muhimu ujaze "KWA WINGI" Neno la Mungu moyoni mwako. Lakini ujijaza "MITANDAO YA KIJAMII" moyoni ujue kwako wewe kushinda dhambi ni kukugumu. Kinachomchafua mtu ni kile kiingiacho moyoni mwako.
Zaburi 119:11 "Moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi," unaweza kuwa na DINI na ukawa mtumwa wa dhambi, lakini ukiwa na NENO utashinda dhambi.

TAFAKARI NENO LA MUNGU MUDA MREFU
KILA SIKU

Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku...,". 1 Timotheo 4:16 "Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo.." Yakobo 1:21 "Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu"
USITAZAME VITU AU PICHA CHAFU NA MIZIKI MIZIKI YA KIDUNIA ISIINGIE AKILINI MWAKO.
Warumi 12:2 "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa nia zebu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kupendeza, na ukamilifu"
Ukifuata mfumo wa namna hii katika maisha utaona unashinda kwako. Lakini ili uweze kushinda lazima uwe "UMEOKOKA" kama unataka kuokoka na uishi maisha ya ushindi tunaweza kuomba pamoja(hakuna umbali katik maombi) piga sasa tuombe pamja na Yesu atakuokoa.
0712-660766
0758-103103
0689-124215


MUNGU AKUBARIKI

ekamalamo@gmail.com

Comments