KANISA LA EFATHA MWENGE: KUJITAMBUA NA KUKAA KWENYE KUSUDI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikxZ-K9hRK12TubU6xlU1_w19GMdKAz0sAciEE6J3XBxgS6eU-6RhGumjpvm2Z8L1BOM4FdobK32v3CeIk7gxco6VRNt7UskxYL9_F-HgDyXdSZfPnnVCgVdKyJTnRfq47BfD7tpchIYU/s640/10665183_644971452268380_8441659817106279636_n.jpg
Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa kanisa la Efatha Mwenge-Dar es Salaam

 KUJITAMBUA NA KUKAA KWENYE KUSUDI 
Tukumbuke kuwa huu mwaka ni mwaka wa mtembeo wa Mungu. Tumeletwa duniani kwa kusudi la Kimungu. 

Sasa tuone jinsi ya kukaa kwenye kusudi la Kimungu. 

1) Ujitambue Unatakiwa kujitambua wewe ni nani? Uliumbwa kwa kusudi gani?. Tukisoma Mwanzo 1:26, unatakiwa kuwa na nguvu ya kutawala, usipokuwa na nguvu ya Mungu hutaweza kutawala kwasababu utakuwa ni dhaifu. Kiwango cha kujitambua kinawezesha kutekeleza yale ambayo Mungu anatamani kukona wewe ukiyafanya. 

2) Unamjuaje Mungu? Tukisoma Ayubu 22:12, Unatakiwa kumjua Mungu sana ili uwe na amani. Ukiwa na amani unakuwa na changamko la moyo na kicheko. Ukisoma Zaburi 5:11, ukitaka kufurahi unatakiwa kumpenda Bwana. Ukitaka kumjua sana Mungu uanatakiwa kuwa na elimu ya Kimungu kwa kukaa darasani na kujifunzanNeno la Mungu kwa kupitia watumishi wa Mungu wanaokufundisha na uyatendee kazi. Ukisoma Mathayo 8:19, Kama umeokoka na kuingia darasani na kujifunza Neno la Mungu na kulifanyia kazi utaona mabadiliko katika maisha yako kiimani na kimwili. Ukiwa ndani ya nyumba ya Bwana utajua huduma yako uliyopewa na Mungu nah ii itakusaidia kukaa katika kusudi na utakaa kwa ukamilifu na uaminifu. Tukisoma Warumi 8:28, Mungu anafanya kazi na wale wampendao katika mambo yote. Ukisoma Methali 8:17, kumtafuta Mungu kwa bidii ni pamoja na kusoma Biblia na kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa, sikiliza Neno la Mungu kutoka kwa watumishi wake. Tukisoma Zaburi 32:8 Ukimtafuta Mungu na kumjua utaona unafanikiwa katika akili zako, afya yako inakuwa njema, na pia mafanikio ya kiuchumi TukisomaMethali 8:17, unapokuwa na pesa unakuwa ukiheshimika na wengi na ukiwa huna pesa utaona hakuna anayekuheshimu kwa lolote. Yesu anataka wewe ufurahi muda wote, kwahiyo tumika kwa nguvu zako zote, kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote, na hapo utahakikisha kusudi lako linakwenda mbele.

 Nabii na Mtume Josephate Mwingira mara nyingi amekuwa akisema, “Hakuna heshima pa kwangu pakavu” Tukisoma Isaya 48:17-18, Neno langu likikaa ndani yenu kwa wingi ombeni name nitawapa. Ukisoma Methali 3:1-8, Neno la Mungu linapokaa kwa mtu hatendi dhambi kwani dhambi inakutenga na upendo wa Mungu. Unapojitambua unaongeza utahamani wako. Tukisoma Zaburi 16:3, acha kujidanganya,bali kaa katika njia yako. Utakuwa Mtakatifu kama alivyomtakatifu Mungu wetu kama hutafanya dhambi. Mjue sana Mungu ili muwe na amani na watu wote. Kama mtu huna amani, mtangazie msamaha. Mbinguni hakitaingia kinyonge kwahiyo tunatakiwa kuwa watakatifu ili tuweze kuingia katika mlango wa uzima. Ukikosea basi omba msamaha na Mungu atakusamehe. Ukisoma Isaya 33:8-9, watu wasio safi hawatapita katika njia ya Bwana. Kama wewe ni mchungani au mtumishi wa Mungu, kaa pale unapotakiwa kukaa ukifanya kazi ya zako. Mpende Mungu akae na wewe. Soma Warumi 8:28, Mungu hufanya kazina wale wampendao. Kaa katika Neno na kuwa mtiifu kwa kutii kile kilichomo katika Neno. You might also like:

Comments