KANISA LA FILEDELFIA (UFUNUO 3:7-13): NA ASKOFU KAKOBE.

ZAKARIA KAKOBE

ASKOFU MKUU WA KANISA  LA FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP (F.G.B.F) TANZANIA.

             (UFUNUO 3:7-13)
           “Na kwa malaika wa kanisa lililoko filedelfia andika:
            Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu na wa kweli, aliye na ufunguo wa daudi,yeye mwenye kufunga wala hapana afunguaye, naye afungaye wala hapana afunguaye, nayajua matendo yako.Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza jina langu,wala hukulikana jina langu.Tazama, nakupa walo wa sinagogi la shetani, wasemao kuwa ni wayahudi nao sio bali wasema uongo.Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele yako na kujua ya kuwa nimekupenda.Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi name nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.Naja upesi.Shika sana ulichonacho asije mtu akaitwaa taji yako.Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu,wala hatatoka tena humo kabisa, name nitaandika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.Yeye aliye na sikio na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Vipengele:
     ( 1 ).  Mlengwa.
     ( 2 ).  Wasifu wa Yesu Kristo.
     ( 3 ).  Sifa njema za kanisa.
     ( 4 ).   Karipio.
     ( 5 ). Maelekezo ya jinsi ya kufanya.
     ( 6 ).  Ahadi.
     ( 7 ). Unabii kuhusiana na majira ya kanisa.


      ( 1 ) Mlengwa.
            Mlengwa wa waraka huu ni kanisa la filadelfia.
Kanisa hili lilikuwa Asia ndogo maeneo ya Uturuki kwa sasa. Kanisa hili lilikuwa maili 30 kusini mashariki kutoka kanisa la Sardi.Mji huu wa filadelfia zabibu zilistawi sana hivyo mvinyo wa kila namna utokanao na zabibu ulipatikana hivyo kulikuwa na walevi wa kila namna.
     ( 2 )Wasifu wa Yesu Kristo.
        (Ufunuo 3:7) Yesu kristo hapa anajitokeza kama aliye mtakatifu na wa kweli, akimaanisha katika majira ya unabii wa kanisa ni katika kipindi hiki kanisa lingerejezwa katika utakatifu kama nyakati za kanisa la kwanza vilevile kanisa likarudia kweli, masomo ya utakaso, ubatizo wa maji mengi, ubatizo wa Roho mtaktifu n.k vikaanza kufundishwa tena. Vilevile anajitokeza Kama aliye na ufunguo wa daudi mwenye kufunga wala hapana awezaye kufungua tena mwenye kufungua wala hapana awezaye kufunga. Kinachozungumziwa katika ufunguo huu ni
  • §  Miujiza: kama Daudu alivyompiga goliath, ni katika majira ya filadelfia miujiza kwa jina la Bwana ikaanza kuonakana tena baada ya kukosekana kwa kipindi chote hicho ambavyo hata kipindi cha martin luther haikuwepo.Katika kipindi hichi Roho Mtakatifu alianza kufanya kazi tena na ule mvinyo uliokuwa mwingi katika mji wa filedelfia ulikuwa unaashiria  Roho mtakatifu (Efeso 5: 18), (matendo 2:13) Ujazo wa Roho mtakatifu unafananishwa na kulewa pombe kwa sababu pombe huondoa aibu,huleta ujasiri na Roho mtakatifu hivyohivyo. Akifungua hapana awezaye kufunga, ni katika majira haya Injili ilifunguliwa sana na kweli ilidhihirishwa kipekee.
      ( 3 ). Sifa njema za kanisa.
       (ufunuo 3:7) – wamelitunza neno la Bwana pamoja na kuzungukwa na makanisa           
                         mengi yaliyozungukwa na makanisa yenye mafundisho ya wanikolai na yezebeli kama Sardi na Thiatra.
     ( 4 )Karipio.
Hakuna karipio, kanisa hili lilikaa katika kweli, hata sisi tukikaa katika kweli, neno la Mungu kama lilivyo hatuwezi kuwa na karipio lolote, hawezi kuwa na neno juu yetu Yesu atakaa kwetu na Roho mtakatifu atatenda kazi pamoja na sisi hata ukamilifu wa dahari.
     ( 5 )Maelekezo ya jinsi ya kufanya.
(Ufunuo 3:11) kanisa hili walitakiwa kushika sana ulichonacho, kushika sana neno (ufunuo3:10-11)
      ( 6 ). Ahadi.
(Ufunuo 3:8) – Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele zako, maana ni kwamba kanisa hili lilikaa katika hili hivyo lilifunguliwa mlango wa kuhubiri injili hata leo sisi tukikaa katika kweli Bwana atafungua mlago.
(Ufunuo 3:9)- tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani, wasemao kwamba ni wayahudi, nao sio, bali wasema uongo maana yake ni kwamba pale ambapo kanisa lina juhudi ya kukaa katika usafi na utakatifu wa kristo nitakupa watu wanaojifanya wameokoka(wayahudi) kumbe sio, hao watasujudu mbele ya watu waliokoka maana yake watakiri  na kushushwa chini ya watakatifu.
(Ufunuo 3:10)- Kwa kuwa umelishika neno la subira, mimi name nitakulinda.
(ufunuo 3:10)- atalitoa kanisa halitakuwapo katika dhiki kuu.
(ufunuo 3:12)- watakatifu watakuwa ni nguzo mbinguni watang’aa kipekee watatengwa, watafahamu jina jipya la Mungu, Yesu, mbingu mpya hayo yote tutapata kujulishwa tukishinda.
     ( 7 ).  Unabii kuhusiana na majira ya kanisa.
Majira ya kanisa katika unabii yaliashiria jinsi kanisa litakavyokuwa miaka ya 1750 mpaka 1905. Baada ya Martin Luther kuwa amemaliza kazi nzuri katika majira ya kanisa la Sardi(wale wananotoroka) na kuanza kukaa katika kweli wanayofunuliwa, alipotoka Martin luther katika kanisa lake la Evenjilical Church likaja kanisa la Anglican, ambayo ilitokana katika mambo ya kitawala baadaye ikagawanyika vipande viwili High church(ilikuwa kama katholic na sanamu, low church(ilifanana na lutheran) likiwa na tofauti ndogo baadaye likaja Moravian. Katika kipindi hiki kweli nyingi zilianza kufunuliwa na kukawa na mafundisho mengi sana na wahubiri wa kila namna ambao walifundisha mafundisho hayo, na kuyasimamia eg:
JONATHAN EDWARDS: Huyu alifariki 1758, alijifunza masomo ya akina Martin Luther akawa ameokoka, katika mafundisho yake alifundisha kuwa watu wenye sehemu katika kanisa lazima wawe ni wale waliookoka tu, na watu ambao hawajaokoka hawana sehemu katika kanisa hawawezi kuhesabika kama mshirika sawasawa na (matendo 2:17).
ii) GEORGE WHITEFIELD: Huyu alifariki 1770, kabla ya kufariki huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza kufanya mikutano ya hadhara ya injili ambayo leo inafahamika kama crusade, mpaka kipindi chake watu waliamini mahubiri na mafundisho sio hadharani ni kanisani, ilikuwa kama kichekesho, vilevile huyu alikuwa wa kwanza kuhubiri bila majoho kamaYesu na mitume waliohubiri kwenye maboti,gerezani n.k jambo hili halikuwepo katoliki wala kipindi cha martin luther. George Whitefield alihubiri sana kiasi kwamba ilifikia mahali katika mikutano yake ya injili ilifikia kuwa na watu 8000 kila siku mwezi mzima, baadaye alifikia kuhubiri kusanyiko lenye watu 20,000 na linakumbukwa sana kusanyiko moja lililokuwa na watu 20,000 ambalo aliwapelekea kushiriki meza ya Bwana hadharani. Pamoja na kazi ya injili kubwa aliyokuwa na ifanya bado injili yake ilikuwa na mgogoro alifundisha habari za Election and pre-destination kwamba Mungu katika mpango wake tangu mwanzo amewachagua watu wa kwenda mbinguni.
JOHN WESLEY: Huyu ndiye chimbuko la masomo ya utakatifu ni mtu ambaye anaheshimika sana alileta masomo ya utakaso katika kanisa ambayo yalikuwa yamesahaulika. Mwanzo wake kihistoria, alizaliwa 1703 alifariki 1791, akiwa na miaka 6 aligundua Mungu ana makusudi yake baada yakusahaulika kwenye ghorofa lililowaka moto ambalo hatimaye alipona aliopopewa ngazi na wazazi wakeashuke kupitia dirisha tangu wakati huo aliona Mungu alimuita awahubirie watu watoke katika Moto. Hatimaye 1738 aliokoka, Mungu alimuandaa sana alikulia Anglicana , alijifunza sana kwenye mafundisho ya George Whitefield lakini alipingana na mafundisho ya Pre-destination, and election hadharani, hatimaye George Whitefield akakubali  kujinyenyekeza na kumpisha Wesley awe mwalimu, afundishe naye akaacha kuhubiri katika kipindi hichi unyenyekevu ulikuwepo kutokana na unyenyekevu. John Wesley alihubiri sana walimwita kichaa, alifanya kazi kwa saa nyingi sana aliweka record ya kutembea maili 250,000 kutumia farasi, alitoa sermons (hotuba) 40,000. Aliweka mkazo mkubwa sana katika utakatifu na utakaso, alipata vita vikali sana, shetani alishindana sana na Wesley, alikutana na mateso mengi sana maudhi, alitupiwa mayai viza(yaliooza) sehemu nyengine alikuwa anrushiwa mawe: ilikuwa haipiti hata siku moja hajafanyiwa moja kati ya hayo, hakujali! Siku moja alihubiri bila kupata hayo yote hajarushiwa mawe wala kutukanwa akaogopa sana, akaingia kichakani kutubu, akijua ameshusha viwango alikuwa akitubu kwa sauti kwamba ‘Bwana bila shaka nimeanza kukosea ndio maana leo mpaka jioni sijapigwa mawe’ kwa sababu aliomba kwa kelele wakapita wahuni wakasikia sala ile wakamrushia mawe Wesley, Wesley baada ya kuona hivyo alimshukuru Bwana hapohapo akasema ‘Bwana asante kwa kuwa leo haijapita nimerushuwa mawe tayari’.Kanisa lake liliitwa Methodist.
WILLIAM CARY: Huyu ni mmishenari anayekumbukwa sana India baada ya kipindi cha Mtume Tomatho kufia huko mda mrefu, huyu aliweka msisitizo mkubwa kuhubiri injili ulimwenguni mwote akawakumbusha watu maneno ya Yesu kristo ya kuhubiri injili ulimwenguni kote, wakati huo injili inahubiriwa sana Uingereza, Marekani na nchi za kandokando alianzisha mashirika mbalimbali kufanya shughuli hiyo mashirika kama ‘London missionary society la mwaka 1795, Church missionary society (1799), British and foreign bible society lililosambaza sana Biblia (1804) matokeo yake wakatokea watu wengi ambao walisafiri kutoka nchi za mbali watu kama DAVID LIVINGSTONE kuja mpaka Afrika, CARY mwenyewe alienda mpaka India.
WILLIAM BOOTH: Huyu alianzisha jeshi la wokovu(Salvation army) akaweka msisitizo mkubwa sana katika mafundisho ya utii, na wakristo kama askari wa Yesu.Walikuwa wanitana askari mwanzo lilikuwa linaitwa Haleluya Army, watu wakawa wanapeana vyeo baadaye likaitwa volunteer army ndio likaja salvation army, wakiwa wanavaa uniform kama za askari.
CHARLES SPERGION: Huyu aliishi1784-1872 huyu anakumbukwa sana juu ya mkazo aliouweka katika mafundisho ya ubatizo wa maji tele, akapinga ubatizo wa watoto wadogo, mwaka 1863 ndio kulikuwa na mkazo mkubwa sana wa mafundisho hayo ya ubatizo.
DWITT LEAMAN MUDDY: Huyu alishi 1837-1899 anakumbukwa sana kama baba wa injili kule marekani huyu naye alihubiri kwa uzito mkubwa na kuwaleta watu wengi katka wokovu 1894.
Baadaye yakaibuka kwa ghafla juu ya Mafundisho ya ubatizo wa Roho Mtakatifu mji wa Sunderland, watu wakwa wananena kwa Lugha: kukatokea uamsho wa ajabu sana watu wakaanza kuombea bila kufundishwa na mtu wakaanza kutoa mapepobaada ya hapo akotokea mhubiri mwingine aliyeitwa:
SMITH WIGGLESWORTH: Huyu ni mmarekani aliishi1859-1946, baada ya kujifunza uamsho huo wa sunderland ambaye aliombewa akapona vidonda vya tumbo. Huyu ndiye mhubiri wa kwanza aliyehubiri mikutano ya injili kutumia ishara,miujiza katika injili yake vilema walitembea, wafu walifufuliwa, vipofu waliona.
Mpaka majira hayo vikawa vimerudi vitu vingi sana vilivyokuwa vimepotea tangu nyakati za kanisa la kwanza Eg: wokovu,ubatizo wa maji tele, ubatizo wa Roho mtakatifu,maombezi, mikutano ya injili ,utakatifu na utakaso na utii wa kijeshi wimbi hili liliitwa PENTECOSTALISM kwa sababu lilihusishwa na matendo ya mitume sura ya pili ya wakati wa mitume sku ya pentecoste.
Ilimgharimu sana Bwana Yesu kuturudusha tena kwenye kweli tangu mwaka huo wa 1905 mpaka leo kanisa linazidi kukamilishwa ambavyo havikuwapo nyakati zile eg: watu kurudi tena katika mafundisho ya MAVAZI ambayo yalipotea kwa mda mwingi kutoka kwenye giza la katholiki na miungu.
MAP OF FILEDELFIA
FILDEFIA
                                                                    OMBI LANGU KWAKO.
         Share ujumbe huu na  marafiki zako wa “facebook” na “twitter” kwa kubonyeza kitufechenye neno “share” hapa chini ya maneno haya. Ukifanya hivyo, utakuwa mmoja kati ya maelfu ya watu wengine watakaopokea baraka za Mungu kwa kusambaza somo hili kwa maelfu ya watu katika mitandao mbalimbali ya internet.
MUNGU AKUBARIKI SANA!!


Neno la uzima kutoka kwa askofu Zakaria Kakobe, tembelea.
Tovuti       : WWW.bishopzacharykakobe.org
Facebook : WWW.facebook.com/bishopkakobeministries
Youtube   : WWW.youtube.com/user/bishopkakobe

Comments