BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la Uzima.
Leo nazungumzia jambo la muhimu sana.
Wokovu uko katika YESU KRISTO.
Watu wengi hujisahaulisha na kuona kawaida tu kwamba muda wa kutubu kwao na kumpokea YESU labda bado kwao haujafika kumbe wameshupaza tu shingo zao ambazo mwisho huwa ni kuvunjika.
Ndugu,Usijisahaurishe Bila Kutubu Maana Uovu Wako Unakumbukwa Na MUNGU Na Usipotubu Uovu Huo Utakupeleka Jehanamu(Hosea 7:2,Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu. ).
-MUNGU anakumbuka uovu wa kila mtu, ukitaka MUNGU asiukumbuke uovu wako basi tubu na kumpokea BWANA YESU maana huo ndio pekee mpango wa MUNGU wa kuwaokoa.
-Mtu anayeutafuta uzima wa milele hawezi kujitenga na YESU. Lazima tu awe katika Wokovu wa KRISTO.
Kila Alifanyalo Mwanadamu Linaonekana Mbele Za MUNGU(Mithali 5:21-23, Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari. Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake. ).
-Hii ni tahadhari kubwa kwa kila mwanadamu.
-Kila akifanyacho mwanadamu kinaonekana kwa MUNGU.
-Kuishikilia dhambi ni kushikwa na kamba za dhambi ambazo usipotubu unaweka ukafa bila kutubu na ikawa hasara kuu.
-Ni heri mtu akapokea maonyo na akaamua kubadilika na kutubu.
Ndugu zangu, kumbukeni kwamba dhambi huwa haijiondoi yenyewe ila inaondoka baada ya mtu kutubu katika KRISTO YESU.
Dhambi ni hatari sana na imeleta madhara makubwa kwa mwanadamu katika nyakati zote.
Dhambi Imepunguza Hata Kiwango Cha Umri Cha Kuishi Mwanadamu(Zaburi 90:10, Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara. ),.
Akina Nuhu Waliishi Miaka Mara Kumi Ya Miaka Ya Mwanadamu wa leo Na Miaka hiyo ndio miaka Mingi Kwa Kizazi Chetu.
Unaweza ukajiuliza, kwanini akina Nuhu waliishi miaka 950? harafu leo mtu ambaye ana umri mkubwa zaidi ni miaka 90, kwanini? Maovu ya mwanadamu yalizidi.
MUNGU leo anasema Tubuni Maana Ufalme Wa wake Umekaribia(Mathayo 3:2,Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. ).
Ndugu Tubu Na Kurejea, Msisitizo wa MUNGU unawataka wanadamu kutubu na kuacha dhambi (Matendo 3:19, Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; ).
BWANA YESU Anawasubiri Wanaotubu Na Kumpokea Ili Majina Yao Yaandikwe Kwenye Kitabu Cha Uzima.
Ndugu Usikubali Kuondoka Duniani Bila Kuokolewa Na BWANA YESU.
Wakati Wa Kuokoka Ni Sasa (2 Kor 6:2,Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa ).
KWANINI MUNGU ANATAKA WANADAMU WATUBU SASA?
=Ni kwa sababu Baada Ya Kifo Ni Hukumu(Waebrania 9:27-28,Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; kadhalika KRISTO naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu. ).
=Ndugu zangu, kuna hukumu mbeleni, Kuna Hukumu Ya Kutisha Sana Huko Mbeleni(Waebrania 10:27, bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. )
Hivyo Ni Heri Na Vyema Tuhimizane Katika Kutenda Mema Huku Tukiwa Ndani Ya KRISTO, Tena Tusiache Kwenda Kanisani (Waebrania 10:24-25,tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. ).
BWANA YESU Yuaja Na Ujira Mkononi Mwake Ili Kumlipa Kila Mtu Sawasawa Na Matendo Yake.
YESU KRISTO Anakupenda Sana ndugu yangu na hataki kabisa upotee bali anataka ubaki katika Nuru yake ya ajabu.
Liishi neno la MUNGU na usikubali kuambatana na wapinga Wokovu.
BWANA yuaja na atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake.
BWANA YESU anasema '' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. -Ufunuo 22:11-13 ''
Ndugu utalipwa nini YESU KRISTO akirudi?
Kuna watakaolipwa uzima wa milele na kuna watakaolipwa jehanamu ya moto milele.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments