KUOKOKA NDIYO MWANZO WA KUABUDU?

Na Mwinjilist Jofrey Sanga.
Ndiyo kichwa cha habari hapo juu chahusika sana katika somo letu la leo. nimekuwa nikifafanua sana katika masomo yangu mengi yaliyopita kuhusu habari ya kuokoka yaani kuzaliwa mala ya pili, na sitaacha kufundisha habari ya kuzaliwa mala ya pili, kwamba ni hivi ukitaka kumuona MUNGU ni lazima uzaliwe mala ya pili, leo nataka nigusie kidogo umuhimu wa kuokoka, maana wakristo wengi kama wanavyojiita kitu hiki wanakipinga, wengine utasikia wanasema hakuna kuokoka duniani, mimi nasema hawa wamepotea na mafundisho ya uwongo na mapotofu, wanasema wanamwamini YESU wakati katika mioyoni mwao wanamkataa, mimi nakwambia kama na wewe uko hivi hebu badilika maana kuokoka ni lazima kwa mtu ambaye anataka kwenda mbinguni.
Wengi wanamwabudu Mungu lakini hawajamwamini mioyoni mwao, ngoja nikwambie kitu kimoja, mtu kabla ya kuokoka roho yake inakuwa imekufa, fuatilia masomo ya nyuma niliyofundisha nadhani tutaenda sawa, kifupi ni kwamba mtu ambaye roho imekufa, maana yake matendo ya mwili yanainuka juu na mtu huyu hawezi kumwabudu MUNGU kwa sababu yupo katika mwili maana MUNGU ni roho na wao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, ndio maana ni lazima uzaliwe mara ya pili ili roho yako ihuishwe na kuwa hai ndipo roho hiyo imwabudu MUNGU, naomba unielewe kwamba mwili hauwezi kumwabudu MUNGU, kinachomwabudu MUNGU ni roho pasipo kuzaliwa mala ya pili huwezi kumwabudu MUNGU kamwe.
Naendelea kufafanua kwamba huku kuzaliwa mala ya pili ndiko kumpokea YESU awe bwana na mwokozi wa maisha yako na ndiko KUOKOKA.Kuokoka ndiko mwanzo wa kuabudu narudia kusema kwamba huwezi kumwabudu MUNGU wakati hujaokoka. Neno kuokoka ndilo limezoeleka kutumika katika jamii yetu, kuokoka ndiyo mwanzo wa uhusiano wako na MUNGU.
Hivi unajua kwa nini wakristo wengi hawajui Neno la MUNGU? hata wakifundishwa hawaelewi? jibu ni fupi tuu ni kwamba hawa wakristo wanakuwa hawajaokoka, hivyo roho zao zinakuwa zimekufa bado. Neno la MUNGU ni roho, kwa vile ni roho, linapokelewa ndani na mtu linatakiwa lipokewe na roho. Neno la MUNGU likipokelewa na mwili haliwezi kueleweka na huyo mtu. Neno la MUNGU hueleweka tuu linapoingia ndani ya mtu ambaye roho yake imehuishwa na kuwa hai. Neno ni roho na ni chakula cha roho. kujifunza Neno la Mungu mtu ambaye roho yake haijahuishwa kuwa hai ni uwongo maana mtu huyu yupo katika mwili, mwili hauwezi kula chakula cha roho, mwili unakula ugali, mkate, samaki, nyama, na maandazi....
Mtu mwenye elimu ya juu sana ya kidunia kama hajaokoka hawezi kulielewa Neno la MUNGU. elimu na akili yake ya kidunia haiwezi kulielewa neno la MUNGU, na ni hivyo hivyo hata kwa mtu ambaye ameenda kusomea elimu ya dini na biblia kama hajaokoka hawezi kulielewa kamwe Neno la MUNGU, atakama atakuwa na PHD ya biblia mtu huyu hawezi kamwe kulielewa Neno la MUNGU kwa sababu hajaokoka, na nataka utambue kwamba watu hawa wanaosomea elimu ya biblia bila kuokoka ndiyo wanaotumiwa sana na shetani ili kulipotosha Neno la MUNGU, wanayageuza maandiko matakatifu na kuwa kinyume, watu hawa ni maajenti wa shetani, awezaye kumfudisha mtu NENO la MUNGU ni ROHO MTAKATIFU peke yake, maana biblia iliandikwa kwa msaada wa ROHO MTAKATIFU, ni muhimu kutambua kwamba wengi wamepotoshwa na mafundisho ya uwongo ya uposhwaji, shetani amewakamata wakuu wa dini mbalimbali na kupitia hao amewapotosha wakristo wengi sana walio katika madhehebu yao.
Watu wa MUNGU, ni muhimu sana kujua kwamba MUNGU anaandaa kanisa kwa unyakuo, hebu turudi kwenye kweli ya NENO LA MUNGU. Huu si wakati wa kushabikia mafundisho ya dini au dhehebu, ni wakati wa kujipigania roho yako mwenyewe. Hebu tuishi maisha matakatifu ili tustahili kumlaki BWANA YESU mawinguni.
YEYE ALIYE NA SIKIO NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA {ufunuo 2:7a}
ACHA KUABUDU KWA DESTURI NA MAZOEA, MUNGU ATAKA TUMWABUDU KATIKA ROHO NA PIA KWELI MAANA YEYE NI MTAKATIFU SANA.
ZIDIKUBARIKIWA SANA MTU WA MUNGU.

Comments