Utangulizi: Somo letu leo linaitwa “Kuzimu wanatoka, Jehanamu hawatoki”. Shetani amejikusanyia watu
wengi kuzimu kwa lengo la kuiniga nao jehanamu. Jehanamu ni moto alioandaliwa
tayari ibilisi na malaika zake. Hadi sasa hakuna mtu ambaye keshapelekwa
jehanamu, bali wote waliokufa wapo
kuzimu wakisubiri siku ya mwisho ya hukumu.
Mchungaji Adriano Makazi akifundisha kanisani Ufufuo na uzima Morogoro. |
1.
JEHANAMU
JINSI ILIVYOANDIKWA KATIKA BIBLIA
MATHAYO
5:21-22….[Mmesikia
watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi
nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu
akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya
moto.]…. Biblia imeitaja jehanamu
hii ya moto.
MATHAYO
5:29-30…[Jicho
lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa
kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 30
Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa
kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.]…Mtu
anaweza kutupwa jehanamu.
MATHAYO
10:28…[Msiwaogope
wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye
kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.]….
MATHAYO
18:9…[Na
jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia
katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum
ya moto.]….
MATHAYO 23:15….[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka
katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha
kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi
wenyewe.]….
MATHAYO 25:41…[Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni
kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na
malaika zake;]… Jehanamu ya moto imewekewa kwa ajili ya shetani na malaika zake.
Jehanamu haikuanadaliwa wanadamu.
UFUNUO 20:10…[Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la
moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa
mchana na usiku hata milele na milele.]….
UFUNUO 20:15…[Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha
uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.]…. Vipo vitabu
viwili: Kitabu cha Uzima na Kitabu cha Mauti. Wasiookoka wote wapo katika kitabu
cha mauti, na wale waliookoka majina yao yapo katika kitabu cha uzima. Kitabu
hiki cha uzima wa milele kinaandikwa na malaika, na si wanadamu.
2.
KUZIMU
JINSI ILIVYOANDIKWA KATIKA BIBLIA
Ni shimo la giza
amabapo ni makao makuu ya shetani. Kuzimu kama
ilivyo mbingu, nayo imegawanyika.
Je, tunajuaa je kuwa mbingu imegawanyika?
2KORINTHO 12:1-4…[Sina budi kujisifu, ijapokuwa
haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. 2 Namjua mtu mmoja
katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili
sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa
juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili
sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa
mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.]…
Mbingu ya tatu iliyoongelewa hapa ipo juu,na siyo chini. Mbingu ya tatu ndipo
akaapo Mungu, na siku moja ututaenda pale. Lucifer alikuwa nakaa mbingu ya
kwanza na ya pili, na ndiyo maana alitamani aende kukaa mbingu
ya tatu kwa mujibu wa maandiko.
UFUNUO 9:11…[Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake
kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.]…Lucifer
ndiye mkuu wa kuzimu. Kuzimu ina malango
(gates) yake.
UFUNUO 9:1…[Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka
mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.]…..
Kama kuna ufunguo wa shimo la kuzimu,
maana yake wapo wanaokaa humo, wanaolinda na kulimiliki. Huyu anayelimiliki
hili shimo anaamuru nani aingie huko.
ISAYA 14:12…[Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana
wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!]…
UFUNUO 12:7-9…[Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na
yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao
hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka
akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye.]… Ni nani aliyeshushwa hadi kuzimu? Shetani aliyekuwa malaika wa ngazi ya kerubi, akiitwa Lucifer, akikusanya sifa za
watakatifu na kuzipeleka kwa Mungu. Alipoacha makao yake yanayomhusu kwa
kutamani kutawala mahali pa Mungu, ndipo alipotupwa nje.
UFUNUO 9:2…[ Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni
kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi
wa shimoni. 3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa
nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.]…..
Mtu anapokufa akiwa
ameokoka, anaenda moja kwa moja paradise, mahali pa mapumziko. Endapo mtu
anakufa kabla ya kuokoka, huingia kuzimu. Mfano wa kuzimu ni sawa na selo ya
magereza, ambapo mhalifu yeyote huwekwa kabla ya kesi yake kuhukumiwa.
Jukumu letu kama Ufufuo na Uzima ni kuhakikisha kuwa jehsanamu anaingia
shetani tu na malaika zake na suoyo wanandanuy
walioumbwa kwa sayura na mfano wa Mungu.
LUKA 16:23…[Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso,
akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.]….
Wito wetu ni kuyafungua mashimo yote ya mashetani na
kuwaweka wote walioshikiliwa hhumo kwa
Jina la Yesu.
LUKA 16:25…[Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea
mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa
yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.]….Kuzimu
wanateswa, ni mahali ambapo waliopo kule wanaumizwa. Kumbe ukiwa kuzimu (baada
ya kufa) bado akili ya mtu inafanya kazi, hata kuweza kuweka kukumbuka mambo. Kumbe
waliopo paradise wanafarijiwa.
LUKA 23:43…[Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami
peponi. ]….Peponi
ni mahali wamapokaa watakatifu wakisubiri watakatifu wenzao hadi siku ile ya hukumu itakapowadia.
Kuzimu ni roho iliyotengenezwa kwa mfumo washimo. Na ipo
siku kuzimu nayo itatupwa jeheanamu ya moto.
MATHAYO 12:40…[Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika
tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na
usiku katika moyo wa nchi.]…Kuzimu nayo inafahamika kama “Moyo wa Nchi”.
1PETRO 3:18…[Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi,
mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake
akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19
ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;]...Yesu
alishuka kuzimu katika zile siku tatu
na kuzifuata funguo za mauti na kuzimu. Alikabidhi
funguo hizi kwa kanisa.
Maandiko kadhaa wa
kadhaa yanathibitisha kuwa kuzimu watu
wanatoka. ZABURI 30:3…[]…
Nafsi,fahari,wadhifa, vitu vya mtu
vyaweza kupelekwa kuzimu. Yawezekana mkono wako, nafsi, macho au miguu yako
imepelekwa na kuungamanishwa na kuzimu bila wewe kuwa na habati.
ISAYA 14:11…[Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako;
Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.]…
Ina maana fahari ya mtu yaweza kupelekwa kuzimu. Fahari ni nini? LUKA 4:5-6….[Akampandisha juu, akamwonyesha milki
zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii
yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama
nipendavyo.]… Mungu amekuumba mtu mwenye heshima, na wajanja wachache
wanaibia hii fahari na kushusha hadi kuzimu.
ZABURI 86:13….[Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu
na kuzimu.]….
ZABURI 16:10…[Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu
wako aone uharibifu.]…. Kilichopelekwa kuzimu chaweza
kurudishwa.
ZABURI 49:15…[Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu,
maana atanikaribisha.]… Maana yake kuzimu yaweza kuachia.
MATENDO 2:27…[Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa
Mtakatifu wako aone uharibifu.]…..
UKIRI
Imeandikwa
“Pozeni wagonjwa, fufueni
wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure”.
Leo Bwana ufufue kama ulivyosema, uwapooze wagonjwa kama ulivyosema,
uwatakase wakoma kama ulivyosema, na uyatoe mapepo kama ulivyosema, kwa Jina la Yesu. Amen.
|
Hapa duniani waliwahi
kuwepo watu wanaoyfanaya mashimo ili
kuwwazuia watu wakae humo. Mtu awekwapo shimoni, chochote alichokuwa anakifanya mtu
hupeperuka. Mtu huanza ujenzi wa nyumba lakini mwishowe haimaliziki. Hizi ndizo
dalili za walioshikiliwa mashimoni. Mbaya zaidi wewe bila kujua unamshirikisha
huyo mtu mambo yako yanapaharibika ukitaka ushauri wake, kumbe anakusikiliza tu
na moyoni anakiri kuwa lile jambo alilokutendea limefanya kazi sawasawa.
Wachawi, wasoma
nyota, wapiga ramli wamevaa nia ya kumtumikia shetani. Yapo mashimo yanayoshikilia watu.
UKIRI
Katika jina la YESU KRISTO, Mashimo
yoyote yaliyonishikilia nayawashia moto na kuyateketeza malango yake na makomeo
yake kwa Damu ya YESU. BABA wa
mbinguni ninakuja kwa Jina la YESU, nakuomba leo BWANA nipate wokovu wako,
kwaJina la YESU, kila mamalaka yoyote iliyonikamata na kuniweka chini, nakataa
kuwa mgonjwa, nakataa kuwa kwenye mateso, nabomoa madhabahu
ya kipepo iliyonishikilia, nabomoa kwa Damu ya YESU,
mahali popote nilipowekwa kwa namna yua uchawi, leo napabomoa kwa Jina la
YESU KRISTO. Ninavunja leo vifungo vyote
nilivyofungwa na watu wa karibu, vifungo vya utasa, vifungo vya umaskini, leo
navivunja kwa Damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO. Amen
|
Comments