Na Godfrey Mwanza, Mombasa Kenya. |
Leo tunajifundisha vitu viwili tofauti ambavyo mwanadamu anaweza kuvipokea kutoka Madhabahuni pa Yehova Mungu.Madhabahu ni mahali patakatifu Hekaluni ambapo watu hutolea dhabihu.Hekalu pia laitwa madhabahu Madhabahu za kale zilitengezwa kwa mawe na kuwa juu ya ardhi(KUTOKA 20:24-25).Nyingine zilitengenezwa kwa mawe ya kuchongwa au chuma kama ielezwavyo madhabahu katika Hekalu la Yerusalemu(1wafalme 7:48).Hii ni sehemu yenye uwepo wa MUNGU sana na watu wengi hupenda kuichezea sana.
Tuone mifano michache ya watu waliochezea madhabahu ya Yehova(1Samweli 2:12-17"Watoto wa kiume wa Eli Hofni na Finehasi walikuwa walaghai sana.Hawakumjali MUNGU wala vitu ambavyo watu walipaswa kuwapa makuhani...Dhambi hii ya wana wa Eli ilikuwa kubwa sana mbele za MUNGU maana vijana hao walimdharau MUNGU.
Baadaye kidogo kukawa na vita kati ya Waisraeli na Wafilisti(1Samweli 4:11"Sanduku la agano la Mungu likatekwa na pia wale watoto wawili wa Eli,Hofni na Finehasi wakauawa"Kunao watu wengi hupenda kufanyia dhambi madhabahuni,wengine ni washerati na kisha wako madhabuhuni ya MUNGU,wengine wanadanganya na bado wako hekaluni(Matendo 5:3-5"Petro akamwuliza Anania mbona shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho mtakatifu...."Anania aliposikia hayo akaanguka chini akafa.Baada ya muda wa saa tatu hivi mke wake Safira akaja bila kufahamu mambo haya naye pia akadanganya na akafa.Wokovu umefanywa na watu wengi kuwa ni wa Jumamosi na Jumapili,wanadanganya Mungu kwa kumkaribia Mungu wakiwa najisi,mioyo chafu,dhabihu chafu,mawazo chafu,wengine wenye mawazo chafu,baada ya ibada wengine huwa wana mipango ya kwenda kukutana na wapenzi wao,kwenda kuua kiroho na kimwili pia,HII NDIYO SAUTI YA YEHOVA:"REKEBISHENI MIENENDO YENU NA MATENDO YENU NAMI NITAWAACHA MWENDELEE KUKAA HAPA HEKALUNI"(Yeremia 7:3-4)
Nimemaliza na kabla sijaenda nataka kukupa majina yetu.Sisi tunaitwa "THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES"-Call us on 0724 656 653.
Comments