BWANA YESU asifiwe ndugu yangu, Leo nimefundisha hapa mtandaoni somo linaloitwa UKIWAJUA MAADUI WA SIRINI UTASHINDA. Watu wengi sana wameguswa na nimeandika maombi ya kuomba ambapo unaweza kuomba kama mimi ninavyoomba hapo chini au pia unaweza kujifunza jinsi ya kuomba na wewe ukaomba kulingana na maadui wa sirini wanaokufatilia.
Omba maombi haya kulingana na hitaji lako.
JEHOVAH MUNGU katika jina la YESU KRISTO, Ninakuabudu na kukutukuza, asante BWANA kwa uzima na asante kwa mamlaka yako uliyoiweka ndani yangu ili niombe. BWANA ulinipa funguo ukisema ''Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.-Mathayo 16:19''. BWANA MUNGU kwa ufunguo huo ambao unapatikana katika jina la YESU KRISTO ninafunga kila ajenda za maadui wa siri zile zinazoendelea dhidi yangu, nina haribu maadui wa siri wote na mipango yako, nawaharibu kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai. Nabomoa viti vya enzi vya kipepo vinavyotuma mawakala wake ili waniumize sirini, kila adui wa sirini na mipango yake yote naangamiza kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO. MUNGU BABA umesema kwamba utamseta shetani chini ya miguu yetu kama neno lako linavyosema katika Warumi 16:20 Kwamba '' Naye MUNGU wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya BWANA wetu YESU KRISTO na iwe pamoja nanyi. [Amina.] ''. Sasa kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO, ninawaseta shetani na mawakala wake wote ambao ni maadui wa sirini, nawasema maadui wote wa sirini na nawakanyaga kwa jina la YESU KRISTO, Namkanyaga adui yule ambaye husikiliza kila jambo kunihusu mimi na yeye anakuja kinyume changu ili nisifanikiwe, namharibu kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO, Namharibu rafiki mnafiki ambaye simujui vizuri na kila siku nampa siri zangu na yeye ananiendea kwa waganga, namharibu kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO, Namharibu kila jini anayejigeuza mbu, nzi au mnyama yeyote ili achukue siri zangu na kuzipeleka katika madhabahu ya kishetani, namharibu kwa jina la YESU KRISTO. Kwa jina la YESU KRISTO najitenga na kila laana iliyotamkwa kwa ajili yangu, najitenga na kila kusudi la shetani lililopangwa ili linipate, najitenga na kila laana iliyotamkwa ili inipate, najitenga na yote hayo kwa jila la YESU KRISTO. Najitenga na kila mpango wa shetani, kila adui wa sirini aliyechukua kitu kwangu na kukipeleka kwa madhabahu za shetani namponda kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO, Kila kitu changu kilichochukuliwa na maadui wa sirini nakigeuza kiwe moto huko kwenye madhabahu za shetani na wateketee wote wanaohusika, adui wa siri aliyechukua pesa yangu ili niwe maskini namponda kwa damu ya YESU KRISTO na mabaya yote aliyoyapanga kwangu, naharibu kila aliyechukua nguo yangu na kuipeleka kwenye madhabahu za shetani ili nisioe/kuolewa, naharibu mipango hiyo yote kwa jina la YESU KRISTO. Kila aliyechukua sauti yangu na kuipeleka kwa waganga ili mabaya yanikute namharibu yeye na mganga wake na kila jambo walilolikusudia ili linipate mimi halitanipata, yote yawarudie wao kwa jina la YESU KRISTO.
Kuanzia leo nafunga milango yote ambayo adui wa sirini anaitumia kuingia kwangu, ninafunga kwa jila la YESU KRISTO, BWANA YESU ulisema '' Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.-Mathayo 18:18 '', Kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninafunga milango yote ambayo adui wa sirini huitumia ili kuingia kwangu. BWANA YESU nakushukuru maana kuanzia leo ni ushindi wa kimbingu kwangu. Jina la BWANA YESU lihimidiwe, tangu sasa na hata milele, Ni kwa jina la YESU KRISTO yote haya nimeomba .
AMEN AMEN.
Hakika umeshinda kwa jina la YESU KRISTO.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Comments