MAOMBI YA KULETA USHINDI.

  BWANA YESU asifiwe.
'' Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7''
Kama muombaji unayehitaji matokeo mazuri baada ya maombi yako lazima uombe kwa imani huku ukiwa mtakatifu.
Haya ni maombi ya vita ambayo kama kikundi cha maombi tukikuwa tunaomba usiku.
Unaweza ukaona na kujifunza kuombea baadhi ya maeneo ambayo unadhani yanahitaji msaada wa BWANA YESU. Sio lazima uombe maombi kama sisi ila naamini MUNGU ataweka nyongeza yako ambyo ndiyo inayohitajika sana ili kupokea majibu yako mazuri ubarikiwe.
''mbeni bila kukoma;1 Thesalonike 5:17''

Siku ya jumamosi.

Leo Tunaomba Tukitumia Isaya 10:27 Biblia Inasema "Tena Itakuwa Katika Siku Hiyo Mzigo Wake Utaondoka Begani Mwako, Na Nira Yake Shingoni Mwako, Nayo Nira Itaharibiwa, Kwa Sababu Ya Kutiwa Mafuta".
Ndugu, Kwa Maombi Makali Kupitia Jina La YESU KRISTO Omba Kwa Imani Ukiondoa Mzigo Wa Shetani Aliouweka Maishani Mwako. Haribu Kila Nira Ya Shetani Iliyokukamata Na Kukutesa. Nira Ni Zile Kamba Anazofungwa Ng'ombe Kwa Ajili Ya Kutii Agizo La Aliyemfunga Kama Kulima Kwa Pilau Au Kubeba Mizigo. Shetani Nae Amewafunga Watu Nira Ili Awatumikishe Na Kuwatesa, Ndugu, Vunja Nira Ya Magonjwa, Nira Ya Umaskini, Nira Ya Hofu Na Mateso. Haribu Kwa Damu Ya YESU Na Kwa Jina La YESU KRISTO. Mzigo Unaoitwa Roho Ya Kukataliwa Uondoe Kwa Damu Ya YESU Na Kwa Jina La YESU. Baada Ya Kuvunja Nira Na Kutua Mizigo Yote Ya Shetani. Hakikisha Utabiri Ushindi Na Mafanikio, Panda Uzima Na Yafunike Maombi Yako Kwa Damu Ya YESU KRISTO. Kisha Mshukuru MUNGU Kwa Kukutia Mafuta Ya ROHO MTAKATIFU Kama Andiko Linavyosema.
Ubarikiwe.

 ''Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. -Yeremia 29:13''

Siku ya jumapili

Leo tunaomba maombi ya kumshukuru MUNGU kwa ajili ya kutulinda na kutubariki kwa wiki nzima na baada ya kumshukuru MUNGU tutaikabidhi wiki yetu ijayo mikononi mwa MUNGU wetu.
Kwa Maombi ya shukrani
Zaburi 136:1-4 Biblia inasema '' Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni MUNGU wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.Mshukuruni BWANA wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. ''
Kumshukuru MUNGU ni muhimu sana na leo , omba ukishukuru kwa MUNGU kukulinda na kukuepusha na hatari zote za wiki hii inayoisha leo, Mshukuru BWANA kwa kuwalinda ndugu zako na familia yako, mshukuru MUNGU maana hukupata habari mbaya na tena maadui zako wote wameshindwa kwa jina la YESU KRISTO.
Kushukuru ni muhimu sana, Wakolosai 4:2 Biblia inasema '' Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; ''

Baada ya kumshukuru MUNGU kwa ajili ya wiki inayoisha leo, anza pia kumwita BWANA kwa ajili ya wiki yako ijayo. Ikabidhi jumatatu yako kwa BWANA YESU, ikabidhi jumanne yako kwa MUNGU, ikabidhi jumatano, alhamisi, ijumaa, jumamosi na jumapili yako mikononi mwa BWANA YESU.
Sema ''Nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu-Wafilipi 4:13''
Sema wiki ijayo lazima nibarikiwe, lazima nishinde kila kikwazo, lazima niwe kichwa na sio mkia katika masomo na kazi.
Wiki ijayo mkabidhi BWANA YESU, Amini kuwa BWANA atakutia nguvu, Muombe BWANA akuwezeshe kuyashinda magumu yote, kiri kwamba unayaweza yote kwa BWANA YESU anatakayekushindia.
MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
Nami nakuombea ushindi katika jina la YESU KRISTO.
''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. -Marko 11:24''

 Siku ya jumatatu.
Maombi ya leo usiku.
Leo tunataka tuombe tukiharibu mipango yote ya adui.
Nahumu 1:9 Biblia inasema '' Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili. ''
-Omba kwa MUNGU kupitia jina la YESU KRISTO, iite ahadi ya MUNGU ili itimie, amini matatizo yako yameisha na hayatainuka tena, kiri ushindi katika BWANA YESU. Magonjwa hayatainuka tena, huzuni haitainuka tena na kila masumbufu hayatainuka tena kwa jina la YESU KRISTO.

-Kemea mapepo yanayotumia sura za watu kukutsa ndotoni. Haribu mapepo yanayoweza kutumia sura yako katika mambo machafu. kemea mapepo yanayokufanya ushindwe kuishinda dhambi. yalipue mapepo hayo kwa jina la YESU KRISTO.
-Haribu mikutano ya kichawi kando ya nyumba yako, vunja mikutano ya kichawi katika maeneo ya biashara yako, kazini kwako, ofisini kwako na katika maeneo yako ya kazi. Pinga mikutano ya kichawi katika nchi,barabarani, njia panda,baharini n.k
Funika anga kwa na kila eneo la nyumba yako kwa moto wa ROHO MTAKATIFU.
Agiza ulinzi wa Malaika kukulinda na kulinda familia yako.

-Haribu mapepo au majini ya laana. Haribu mapepo yenye ushawishi wa kuharibu baraka zako, wapige majini wa ushawishi ili wewe ufukuzwe kazi au usipate kazi.
Vunja mapepo na majini yenye kubadilisha baraka kuwa laana.
omba maombi yote hayo kupitia jina la Mamlaka yote la YESU KRISTO.
MUNGU wa mbinguni akubariki sana na mimi Peter M Mabula nakuomba MUNGU akupe nguvu na ushindi wa kimbingu katika yote.


Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments