MATOKEO YA NGUVU YA NENO ANALOTAMKA MTU WA ROHONI. (SEHEMU III)

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Mungu akubariki sana ndugu unayependa kujifunza Neno la Mungu. Mungu azidi kukufunulia zaidi unapoendelea kujifunza somo hili.
Hii ni sehemu ya tatu ya mfululizo wa somo hili, hivyo ili uwezekujua zaidi tulipoanzia tafuta sehemu ya I na ya II ya somo hili utamjua mtu wa "ROHONI" na anaishi "ULIMWENGU UPI".
Tunaendelea sasa mahari tuliishi,Roho Mtakatifu akufunulie upate kuelewa katika Jina la Yesu.
EZEKIELI ALIPOIONA MIFUPA MIKAVU ALIKUWA WAPI?
Tunapo soma habari ya Ezekieli tunapewa picha ya "ULIMWENGU WA ROHO" ambayo alikuwako Ezekieli. Utasema,..."unajuaje?, Soma Biblia Ezekieli 37:1 anasema hivi, "MKONO WA BWANA ULIKUWA JUU YANGU,NAYE AKANICHUKUA NJE KATIKA ROHO YA BWANA, AKANIWEKA CHINI, KATIKATI YA BONDO; NALO LIMEJAA MIFUPA MIKAVU"
Sasa anglia pamoja na mimi lile neno.."NAYE AKANICHUKUA NJE KATIKA ROHO YA BWANA" utaona ya kwamba Ezekieli anatolewa kwenye "MWILI" na anaingizwa kwenye "ROHO" na huko ndiko anaweza kuzungumza na Mungu, Usisahau jambo chili (Mtu wa rohoni anauwezo wa kwenda mahari kokote atakako Mungu) ndiyo anaamishwa Ezekieli ili Mungu amuonyeshe picha ya Taifa la Israeli ilivyo katika "ULIMWENGU WA ROHO"
Ukisoma ule mstari wa 1-3 katika Ezekiel 37 utaona anaonyeshwa "MIFUPA MIKAVU" na anaulizwa swali na Mungu,,"...JE MIFUPA HII YAWEZA KUISHI? Angalia Ezekiel alivyo mjibu,,"Ee BWANA MUNGU,WAJUA WEWE" nini maana yake jibu hilo? maana yake Ezekieli hana mashaka juu ya Mungu wake, lakini asingekuwa kwenye "ROHO/ULIMWENGU WA ROHO" Ezekieli angesema haiwezekani jambo hilo, chukulia ni wewe sasa hivi unaletewa mifupa ya ng'ombe unaulizwa.."MIFUPA HIYO MIFUPA INAWEZA KUWA MG'OMBE? lazima utakataa maana kwa jinsi ya "MWILI" hawezekani.
Ezekieli alposema..Ee BWANA MUNGU WAJUA WEWE" Mungu alimuona Ezekieli "ROHONI" wakiwa pamoja maana alimchukua katika "ROHO" na ndipo ukisoma ule mstari wa 4-6 Mungu anampa "NENO ATAMKE JUU YA MIFUPA MIKAVU".
Kasome Biblia yako utaona Ezekieli analitumia "NENO" akiwa katika "ROHO/ULIMWENGU WA ROHO" kutamka mifupa iwe na uhai, ndipo mifupa,mishipa na nyuma vinaungana na kuwa na uhai na kuwa jeshi kubwa.
Hilo no jambo linafanyika katika ulimwengu wa Roho kwanza, na baada ya hapo aingie ulimwengu wa "MWILI". Mungu anamwambia hivi..."Basi tabiri, uwaambie,Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburiyenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu,enyi watu Wang, nami nitawaingiza katika nchi ya Israeli.(Ezekieli 37:12)
Israeli kwa jinsi ya mwili walikuwa nashida walipoteza matumaini,walijiita "MIFUPA MIKAVU" na matumaini yao hayakuwepo tena. Sasa ili Mungu asshughurikie hilo tatizo lazima apatikane mtu ambaye ataingia katika "ROHO" ili atumie "NENO" atakalopewa juu ya mifupa hiyo, ndipo Ezrkieli akachukuliwa katika Roho.
JE KWAKO KUNA JAMBO LIPI UNAONA KABISA HALIWEZI KUWA HAI?
Kama umeokoka lazima uingie katika ulimwengu wa roho "KWA MAOMBI" na huko utapewa NENO la kutamka katika shida hiyo. Kinachooneka shetani kakiua ulimwengu wa mwili,wewe unakitamkia "UHAI" katika ulimwengu wa roho.
Ulimwengu wa roho ukiweka majibu uwe na uhakika utaona majibu ulimwengu wa mwili.

Kama unaona mume wako hakupendi ghafla na haujui shida ni nini, usigombane naye, Huyo amefungwa na mtu apeteze "UPENDO" kwako,usipoingia katika ulimwengu wa roho ukamfungua uwe na uhakika atakuacha. Lakini ukipambana na roho zilizo mfunga katika.."ULIMWENGU WA ROHO" ataachiliwa na utaona anakubusu mwenyewe bila kuombwa,ambavyo umekaa miezi 5 hujui kiss ya mumeo, kadharika na kwa mwanamke ni vivyo hivyo.
Kwa mantiki hiyo usijaribu kutatua tatizo la "KIMWILI" katika mwili, bali anzia ulimwengu wa "ROHO" kama tu umeokoka. Maana shetani hufanya vita katika ulimwengu wa roho ili kuvuruga mambo yetu katika ulimwengu wa mwili.
ILI UWEZR KUSHINDA VITA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO LAZIMA UWE UMEOKOKA. KAMA INATAKA KUOKOKA PIGA SIMU TUOMBR PAOMJA.
0712-660766
0758-103103
0689-124215.

MUNGU AKUBARIKI
ekamalamo@gmail.com

Comments