MATOKEO YA NGUVU YA YA NENO ANALOTAMKA MTU WA ROHONI.

Na Emmanuel  Kamalamo

Bwana Yesu asifiwe!
Tumesika mara nyingi neno hili likitamkwa na watu, na wakisema.."MTU WA ROHONI"
Nami napenda kukueleza habari za huyo mtu wa rohoni anavyotenda kazi katika ulimwengu usioonekana ( Ulimwengu wa roho). na akasababisha matoke( majibu) ya ulmwengu wa roho yatokee ulimwengu wa mwili.

Paulo analiambia Kanisa la Efeso manene hata,"Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu...hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani mmeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu" (Waefeso 2:1,5-6)
Nataka ufahamu maneno hayo ili upate kumjua mtu wa rohoni. Mtu wa "ROHO" ni mtu aliyetolewa katika hari ya "KUFA KIROHO" ( aliyekuwa hana mahusiano na Mung) na akampokea Yesu, mtu huyo ( mtu wa ndani) ana fufuliwa kutoka kwenye hari ya "KIFO CHA KIROHO" na anaketishwa pamoja na Yesu katika ulimwe wa roho.
Lakini kwa namna ya "MWILI" pia mtu huyo (wa rohoni/aliye okoka) anaishi ulimwengu wa damu na nyama akiwa kwenye mwili. Na kwa na mna ya "KIROHO" ataishi pia katika ulimwengu wa "ROHO"
Hivyo, ni mtu mmoja (aliye okoka) anaishi ulimwengu wa ROHO na MWILI kwa wakati mmoja.
Ndiyo maana Paulo anasema,,"KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA; BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA,JUU YA WAKUU WA GIZA HILI,JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO" (Waefeso 6:12)
Sasa angalia lile neno,"ULIMWENGU WA ROHO" ulimwengu huo hauonekani kwa jinsi ya mwili, hivyo anayeweza kuujua ulimwengu huo ni yule mtu wa "ROHONI" na ndiye anaweza kupigana vita katika ulimwengu huo. Ili uweze kuweka mabadiriko mahari ambapo "UTAWALA WA SHETANI UMETAWALA" Lazima uanze kuharibu/ kupambana na utawala huo katika ulimwengu wa roho, na ndipo utafanikiwa ulimwengu wa mwili.
Ndiyo maana kila uharibifu unatokea mahari chanzo ni "ULIMWENGU WA ROHO"

UNALITUMIAJE HILO
NENO NA WAPI?

fuatana nami.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA,BAADA YA KUFA NI HUKIMU.(Ebrania 9:27)
MUNGU AKUBARIKI
ekamalamo@gmail.com

Comments